crabat kuna mambo mengi sana huyajui kuhusu uislam wa tanzania na mali zake,usiwe shabiki wa ki siasa tu na kukandamiza,Bakwata ndio wana mapungufu lakini unajua historia ya hayo maeneo? au wewe unaongea tu kishabiki udhuria vikao na makongamano ya busara ya waislam ndio utajua historia ya kweli na sio hizo siasa,
NA PIA NAKUONEA HURUMA KWA KUJIVUA NGUO HADHARANI,NA KUONGEA KITU AMBACHO HUKIJUI BALI USHABIKI TU,NA MBAYA ZAIDI MTU ASIYE MUISLAM ANAKUFUNDISHA HEKIMA NA USTAARABU,INSHAALLAH NAKUOMBA HUDHURIA MADARASA YA KIISLAM KATIKA MISIKITI ILIYO KARIBU NA WEWE THEN UTAELEWA NA SI KAMA AMBAVYO UMEFANYA,
USHASIKIA WAKRISTO WANAKUJA KUANIKA MAMBO YAO HAPA ???????
Prince Prince, Nakubali kwamba kuna mambo mengi kuhusu Uislam Tanzania na mali zake siyajui . Kwa hili sio mimi tu ambao tupo gizani bali waislam wengi.
kwanini tupo gizani ? Bakwata ndio walo rithi mali za EAMWS na pia mali nyengine za wakfu walizo toa waislam kwa ajili ya maendelo ya waislam. waislam hawa walikua na nia nzuri kabisa na pia kama sadaka yao . Kuna mali nyengine walipewa na serikali. HAKUNA HAKUNA ambacho bakwata wamenunua kwa fedha zao (labda magari yao) kama kipo utatujuvya tuelewe.
kulikuwa na nyumba Upanga moja mie naifahamu kabisa ipo mtaa wa Undali , hii wameiuza bila ya aibu ni wizi kabiisa. Kuna mali za waqfu viongozi hawa wame jiuzia wao na kuziuza .
kuna uwanja maaruf wa changombe mchicha jee ni sahihi kuutoa uwanja ule kwa vituo vya ptroli ? na wafyatuaji matofali ?
uwanja ule kama hawa watu ni waadilifu ni zaidi ya EKA 20 ! wanalishindwa nini kukusanya nguvu za waislam na kujenga shule ya kisasa na Hospitali Kubwa ya kina mama ambao huwa wanakwenda kuzalia hospitali zisizo kuwa na maadaili ya kiislam na kuzalishwa na wanaume? bila ya shaka wamekosa dira, wamekosa uadilifu , wamekosa nia ya dhati kuutumikia umma.
wazee wa mji huu kina Tambaza na Mwinyimkuu wametoa maeneo mengi kwa ajili ya uislam na waislam na yalobaki ni makaburi, ingekuwa nayo yanauzika basi makaburi ya mwiny mkuu wangesha yauza zamani,
Kuhusu madrassa na makomano....napenda kukufahamisha mimi si mjuzi wala sina elimu ya uislam lakini alhamdulilah..najua mengi na kwa siku natumia masaa zaidi 2 kujisomea makala na vitabu mbali mbaili ikiwamo uislam, hadith na mengineyo ya kidunia, nashukuru niko well informed.
Ama kuhusu kulisema Bakwata hadhara na kuli nganisha na wakristo kuwa huwakuti kuwasema viongozi wao ...jawabu yake ni hii:
hao wakristo wana ridhika na uongozi wa taasisi zao kwani zinawatumikia haswa na viongozi ipasavyavo na maslahi ya yanalindwa haswa.
sisi tasisi yetu haitusaidii kabisa, ni wafujaji wa mali
hawana vision yoyote
wanatuvuruga
wao ndio walofanya uchuro mpaka hoja ya Kadhi Court ikawa kiroja. wakati waislam wana jadili hoja hii kwa uweledi wao wakateua makadhi !!!!! yaani mambo ya ajabu kabisa. na kwa vile serikali inawatumia kuharibu issue yote ya Kadhi COURT na kinacho endelea kila muislam ana kiona ...
Ndugu yangu kuna tofauti kati ya kuumkosoa binaadamu hata akiwa kiongozi au tasisi anayo iongoza na kukosoa imani.
Bakwata haifai kuwaongoza waislam , ni taasisi ya kibaguzi , na iliundwa kwa misingi ya kibaguzi ati kuwapa watanganyika waafrika taasisi yao wenyewe, hilo ndio lilikua agizo la kuundwa kwa Bakwata , jee ndugu yangu msomi uislam unakubali kuwa na taasisi ya waislam waafrika pekeee?
hilo ndio likazaa taasisi za kikabila, yote yametokana na kuundwa kwa bakwata ya 'watanganyika' na muasisi wake anajulikana .
leo athari yake tuna Istiqama-ya waislam wa oman
tuna TYCC - Tasisi ya waislam wayemen
tuna bohora
tuna ismail
tuna shia Ithnaasheri
kila mmoja na lake..Taasisi hizi zote zilikua chini ya EAMW.
MWISHO KWA VILE BAKWATA NI TAASISA AMBAYO SERIKALI NDIO INAYO ITAMBUA KUWA INAWAKILISHA WAISLAM TANZANIA NA KWA VILE TAASISI YENYEWE HAIFANYI WAJIBU WAKE NA HAKUNA NJIA YA KUIBADILISHA IWAJIBIKE BASI TUTA ISEMA MPAKA ITAPO BADILIKA