BAKWATA na Mauaji Arusha

Si busara kuwalaumu bakwata kwa sasa, nadhani wanawasiliana na arusha ili watoe taarifa yenye uzito na usahihi. Ni busara tusuburi tafakuri zao. Nadhani niwape angalizo, wasije wakajipa upange, wajiweke kwenye jamii
 


Usipoangalia unakaribia kupata ugonjwa unaowapata wengi wanaothamini dini kuliko haki unaoitwa fikramgandoosis. Unajua mission ya dini yoyote duniani? unapoona haki inakiukwa ni wajibu wa wapenda haki wote kukemea. kumbuka leo kwa mwenzio, kesho kwako. hakuna binadamu mwenye akili timamu awezaye kukaribisha hali hatarishi ya maisha ya viumbe wenye thamani kupita wote duniani-Binaadamu. Ni jukumu siyo la wapenda haki tu, bali la watanzania wote kulaani matumizi ya nguvu katika shughuli halali zenye haki za kikatiba ili kuilinda katiba yetu pamoja na mapungufu yake. Hapa natarajia hata viongozi wa serikali kulaani tabia za namna hii. hujasoma magazeti leo kwamba hata Rais Kikwete amesoneshwa na kilichotokea arusha na kuahidi kuwa hakitatokea tena? Hivi unadhani ni kwa nini serikali imefikia kuomba meza ya mazungumzo na wawakilishi wa wananchi-cdm kwa tukio la arusha? THINK THINK THINK kabla hujamwaga mawazo yako janvini
 

we b.w.e.g.e badala ya kumrekebisha mtuma post .
 
Habari ya mwembechai ilikuwa na maslahi kwa kundi moja katika jamii, habari ya Arusha ina maslahi kwa taifa zima

Mtu yoyote kuwawa sio kitu cha kufurahisha ispokua ni lazima tukubali mazingira aliyouwawa mtu yana mchango mkubwa ktk kufikia uamuzi kua aliuwawa kimakosa au hapana. Sidhani kua ni hekima kusema kua mauaji ya muembe chai yalikua ni halali kwa kua wale watu walipigania maslahi binafsi na maandamano ya juzi yalikua na maslahi kwa taifa zima.

Ni muhimu kua na utaratibu ktk ufanyaji wa mambo na ni lazima utaratibu ufuate, Ninafikiri kua maandamano yalizuiwa na serikali kwa sababu zinazohusiana na uslama, sasa kama kituo cha polisi kilitiwa moto na watu wengine walitaka kuwatoa watu ktk kituo cha polisi kwa nguvu. yoyote anaweza kuona kua hiyo haikukaa sawa.

Mpaka sasa tunapata sana information za upande mmoja ule unaolaumu kua umefanyiwa dhuluma, tusubiri serikali nayo itoe maelezo kua kwanini hali ilikua vile au mazingira gani yalipelekea ile hali kutokea.

Wengi hawaoni kua kuna change yoyote kubwa inayoweza kufanyika hasa ukizingatia ni juzi tu tumemaliza uchaguzi.
 

Sijasema mauaji ya Mwembechai yalikuwa halali. Nilikuwa namjibu mchangiaje anayeshangaa kwa nini maaskofu hawakulaani mauaji yale. Ndio maana nikasema, yale ya Mwembe yalihusu kundi moja ambalo linakinzana na maaskofu sasa wasingeweza kulitolea tamko. Kwanza waislamu walianza kuwakashifu hao maaskofu hivyo kuondoa uwezekano wa maaskofu 'ku-sympathise' nao. Hili la Arusha halina msingi wa dini yoyote na hivyo maaskofu ktk neutrality yao wametoa tamko kulaani, na hata Bakwata naamini wako njiani kutoa tamko kwa sababu kipenzi chao (Lipumba) ameshafanya hivyo.
 

nani kakuongopea? "muislam ndugu yake muislam" kwa vyovyote tutaipinga bakwata lakini hatutoisaliti ni tofauti za kawaida si kwamba bakwata haitakiwi na waislam. alafu yalipofanyika mauwaji kule pemba hao wagala wa kwanza kupinga tamko waliongea nini?
au ndo mkuki kwa nguruwe?
 
Muda bado upo kwa bakwata kutoa msimamo wao. Pia ianwezekana walishatoa lakini kwakuwa hawana redio wala gazeti ndio maana hamjawasikia. Pia inawezekana wameona ni busara zaidi kukaa kimya kwa kuwa hawana taarifa ya kutosha kuhusiana na vurugu hizo. Kama kuna wengine walihojiwa na kutoa misimamo yao, yeyote kati yetu anaweza kufanya appointment na viongozi wa bakwata akaenda kumhoji kujua mtizamo wao katika suala hili.

Kusema kwamba bakwata wanajali oic tu ni kauli ambazo zinaweza kutonesha hisia za kidini na kuleta tofauti kati ya wanachama wa jamii forum na wanachi wengine bila sababu.
 
Mimi natowa tamko la kuwalaani wote walioanzisha na kushadidia maandamano yaliyozuiliwa na polisi kufanyika.

Walaaniwe wote waliolazimisha ya fanyike na damu za hawa waliofariki ziwasute maisha yao yote.


Wewe ni nani? Swali limeuza Bakwata! nadhani husitumie uhuru wa kutoa maoni humu kutoa ushabiki wa mpira katika mambo ya msingi; kwanza hata hujui mstakabali wa Tanzania ni bora ukae kimya kwa mambo husiyo yajua; tulipo sema katiba nyinyi ndio kunguru wa awali kuimba kwamba sio tatizo leo Dunia nzima inakiri ni tatizo kubwa sana, si kila matatizo katika jamii yanashugurikiwa na jamii nzima tunajua katika yoyote kuna watu wa aina tatu, MOJA Shujaa ambao wao kwa Tanzania wamekuwa mstari wa mbele kudai haki na maslahi sawa kwa Watanzania tokea enzi za Mkoloni, wanakufa na kuzaliwa wengine kila siku na wanaendele kudai haki za watanzania kila siku, katika kundi hilo wamo Watanzania wengi na kwa sasa wengi wamejiunga kudai haki hizo kupia CDM, PILI waoga ambao wanayajua matatizo hawayataki wanayachukia lakini ni waoga kushiriki katika vuguvugu la kudai haki kwa kuogopa kupoteza maisha, vyeo, na riziki wanayopewa kutoka kundi la wanyaji, katika kundi hili mfano mzuri ni Spika Sitta na wanyonge wengine wengi ambao wapo serikali na vijijini, najua wapo Majeshini na katika vyombo vya Usalama vyote na Rais wako anajua na chama chako kinajua, hili kundi ni kubwa kwa sasa ndio maana kikwete anapata taabu, kundi hili ni muhimu kwa maana hawa wanapokomaa na kuamua uwa kundi la kwanza la uendelea kuishi katika kundi hiliTATU Punguani ambao wao hawajui lolote wala chochote kinachoendele kila kitu kwao ni sawa, kundi hili hawana cha kulaumiwa bahati mabaya wamezaliwa hivyo na watakufa hivyo hivyo, sitaogopa hasilani kukwambia wewe ni hili kundi la tatu hamna tofauti yako na ombaomba walioko BibiTiti/Moromoro rd kama unabisha taja jina lako halisi naujitokeze hadharani tukakupime akili!
 
Hivi KKT nao walilaani maiuaji ya MWEMBECHAI?

Sijasema mauaji ya Mwembechai yalikuwa halali. Nilikuwa namjibu mchangiaje anayeshangaa kwa nini maaskofu hawakulaani mauaji yale. Ndio maana nikasema, yale ya Mwembe yalihusu kundi moja ambalo linakinzana na maaskofu sasa wasingeweza kulitolea tamko. Kwanza waislamu walianza kuwakashifu hao maaskofu hivyo kuondoa uwezekano wa maaskofu 'ku-sympathise' nao. Hili la Arusha halina msingi wa dini yoyote na hivyo maaskofu ktk neutrality yao wametoa tamko kulaani, na hata Bakwata naamini wako njiani kutoa tamko kwa sababu kipenzi chao (Lipumba) ameshafanya hivyo
 

nadhani kuna mantiki kubwa katika uliyoyasema kaka. Niko pamoja nawe.
Pengine tujiulize; MBONA MAASKOFU HAWAKUTOA MATAMKO JUU YA WANACHADEMA WALIPOUA PALE MASWA?? AU ILE DAMU ILIKUWA MAJI?? NAONA DAMU ILE YA YULE JAMAA ALIYEUAWA PALE MASWA NDIYO IMEWAFUATA CHADEMA. MTENDA HUTENDWA!
naliyasema haya ndani ya JF ila kwa sababu ya mihemuko watu wakaniona mpuuzi. Kuna mtu mmoja anajiita "Josephine" akanitukana sana nikasema haya. ukisema nasapoti juu yako lakini ukweli umetimia. asiyesikia la mkuu kichwa hupigwa ngeu.

 
Cityboy hebu rudi tena.....Maaskofu wana ubia na CDM au wana 'memorandum of understanding' na serikali kama mlivyokuwa mnadai hapo awali?

Ndio serikali ina MOU na kanisa.MOU uliingiwa wakati wa mkapa na kanisa lilikua na sauti kuu juu ya serikali.Soma fact za Kadogoo hapo juu.Wakati huu wakristo na matamko ya kilaleo ili tu nafasi irudi huku wakitafuta mbadala ambao ni kupitia cdm.Tazama humo cdm kulivyo na udini,tena ukatoliki ukiwa zaidi ya waunga mkono wengine.Kanisa lina hangaikia nguvu za kuuangamiza uislam na JK amewasoma ndo maana mwaka2010 hakua chaguo la Mungu tena kwani mlivyoni ni wa kuburuza tu sivyo!Kampeni zenu tunazijua A to Z upo hapo?
 

Kwa hiyo MoU ukomo wake ilikuwa ni 2010?
 
Unataka kuniambia kuwa viongozi wa dini hawaruhusiwi kukemea uovu uliofanywa na vyombo vya Serikali, km Jeshi la Polisi, eti kwa hofu ya kuogopa kuchanganya dini vs siasa?

Rejea tamko la kanisa juu ya mauaji ya Zanzibar.Kama unakumbukumbu naomba unijibu. Zanzibar walokufa ni waislam.Kanisa na cdm lao moja! Upo?
 
Rejea tamko la kanisa juu ya mauaji ya Zanzibar.Kama unakumbukumbu naomba unijibu. Zanzibar walokufa ni waislam.Kanisa na cdm lao moja! Upo?

Na Bakwata je! Walitoa tamko mauaji ya pemba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…