Boma,
''Wangetii Selikali'' ya nani? Usikuze mambo bila sababu, hivi kuruhusu Chadema au CUF kuandamana ni sawa na kuruhusu kila mtu kufanya anavyotaka? Chama au kikundi huomba maandamano na kuelezea maudhui ya maandamano hayo. Kisha waandaaji wa maandamano hubeba jukumu la kuhakikisha watu wao wanaelewa mipaka na misingi ya maandamano hayo. Baadaye polisi wanatakiwa kutoa ulinzi na kwa kuwepo kwenye maandamano hayo ili kudhibiti hali yoyote ya kukiuka mambo waliyokubaliana.
Kule Arusha hapakuwa na fujo yoyote hadi polisi walipoanza kuwapiga wananchi wasio na hatia. Wangeacha kuwapiga watu wala yasingetokea yaliyotokea. Hivo si vizuri kulaumu tu Chadema. Kumwagika kwa damu ni makosa ya moja kwa moja ya viongozi wa selikali. Sheria inatuzuia kuchukua sheria mkononi sote pamoja na polisi. Iundwe tume ichunguze hawa waliouawa ni kwa nini? Je walikuwa na silaha kiasi cha kutishia kuwadhuru polisi au hata kuwaua wasingewawahi? Walihatarisha maisha ya askari au raia karibu yao? Kwa nini polisi walichagua kuwaua hawa tu? na mengine mengi.