Nami nko huku mbeya,jana nilimwomba mshikaji Ustadhi gari yake ndogo nkaitumia kutoka mbeya mwanjelwa kwenda Tukuyu. Wakati niko tukuyu nkawa na kiu nkapita sehemu nkapata moja baridi. Niliporejesha gari ikabidi nipite car wash mwanjelwa kuondoa harufu ya pombe ili ustadh asijenitoa nduki. Jioni nkamtafuta mshikaji wangu wa Tra mbeya. Tukakutana Shaba Pub Mwanjelwa. Nlipomwambia kuwa nlikuwa Tukuyu na usafiri wa Ustadhi,kumbe anamjua ustadh ni mshirika mwenzie,jamaa kanyanyua cm na kumtwangia ustadhi,ustadhi alikuja mbio na kashangaa kunkuta pale Shaba pub,Ustadhi kakata kiu Mpaka nimeogopa,mpaka saa8 usiku, ilikuwa ni mishikaki,castle,kitimoto,disco mwanzo mwisho. Ama kweli dini zimeingiliwa. Mchana ustadh,usiku mwenzetu!