BAKITA lawashukia wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BAKITA lawashukia wabunge

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by EMT, Apr 14, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  BARAZA la Kiswahili la Tanzania (BAKITA) limewakumbusha wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutumia Kiswahili pekee badala ya kuchanganya na Kiingereza kwani linawafanya wananchi kutoelewa vizuri hoja zao.

  Akizungumza juzi na Dar Leo Ofisini kwake, Kaimu Katibu Mtendaji wa Bakita, Noel Karekezi, alisema wabunge wanatakiwa kulitambua hilo kila wanapochangia hoja zao ili waeleweke na wananchi. “Malalamiko yetu tangu awali ni uchanganyaji wa Kiswahili na Kiingereza. Unakuta wanajisahau kuwa wanazungumza wenyewe kumbe wanasikilizwa na wananchi wengi,” alisema.

  Amesema kuchanganya lugha hizo kunawafanya wananchi kushindwa kuelewa hoja wanazozitoa na hivyo kuwataka kujifunza kutumia Kiswahili wakati wakitoa hoja zao. Amekiri suala la uchanganyaji wa lugha hizo ni la kitaifa kutokana na mazoea yaliyojengeka katika jamii.

  “Wakati mwingine tatizo la kuchanganya lugha ni gumu kuliacha kwa sababu unakuta Kiswahili unatumia nyumbani na Kiingereza unatumia ofisini,” alisema. Ameongeza kuwa BAKITA ina azma ya kuwapa semina wabunge hao, lakini kutokana ufinyu wa bajeti wameshindwa kutimiza azma yao lakini bado wataendelea kuwakumbusha juu ya matumizi ya Kiswahili.

  Katika hatua nyingine, Kaimu Katibu Mtendaji huyo amesema wahisani wengi toka nje ya nchi wamekuwa wazito kukubali kufadhili uenezwaji wa lugha ya Kiswahili kwa kile alichodai kuwa wengi wanataka lugha na tamaduni ziendelezwe.

  Source: Darleo
   
Loading...