Fundisi Muhapa
JF-Expert Member
- Nov 25, 2013
- 4,422
- 2,115
Kuna neno Mwanaharamu. Kuna siku lilileta mtafaruku Redio one. BAKITA wakisistiza ndio neno sahihi kwa aliezaliwa nje ya ndoa, Mtangazaji wa redio one akilipotezea na kudai linadhalilisha baadhi ya watu.
Hivi vyombo vya habari vina unafiki mkubwa sana na ndio vinatupoteza. Wanafata tu matakwa ya bosi zao mara nyingi.
Mwaka 2001 nilihudhuria hafla ya walemavu iliyoandaliwa na Mengi huko Tanga Mkonge hotel. Alisisitiza sana kutotumia neno 'mlemavu' pekee na kushauri 'mtu mwenye ulemavu'...... ukitafakari, haina mantiki. Vyombo vyake vikaanza kutamka hivyo na hadi leo limeshika kasi. Hata Albino ni yeye alishauri wasiitwe zeru zeru... UNAFIKI!
Kujaribu kutumia lugha za nje, sio tu tunadhalilisha walemavu bali pia na jamii nzima kwani tunaonekana malimbukeni.
Lakini inaenda mbali zaidi......
Asilimia kubwa ya jamii zetu Tz na Afrika kwa ujumla wanaona ufahari kutumia majina ya kizungu au kiarabu ama kutokana na dini au elimu walonayo..... yote hiyo ni ulimbukeni kudhani cha jirani ni bora wakati "Titi la mama latosha".....
Kuna wakati niliambiwa huko mkoa kwamba watu wenye ulemavu wa miguu tuliozea kuwaita vilema nao hawalitaki hilo jina wanataka waitwe majeruhi wa vita.
Kiwete, kipofu, Zeruzeru, Kiziwi, Bubu,Kichaa, Mguu Mbovu, Mkono Mbovu n.k. Haya yote ni Maneno halali kabisa ya kiswahili, chakushangaza sasa hivi kumezuka mtindo wa watu wenye aina hizo za ulemavu kuyakataa majina hayo na kujipachika majina ya kiingereza eti, Albino, na wengine eti wanazunguka Mbuyu eti, Mlemavu wa Mguu badala ya Kiwete n.k
Huu ni ujuha si vinginevyo. Mwishowe hata watoto watakataa kuitwa watoto, wadai haki zao na wao waitwe Children.
kumwita MTU kama hapo pekundu ni kumfananisha na kitu..(ki) kijiko,kisu, kiti, kikombe nk...iwe hivi kipofu=ASIYEONA, kiziwi=ASIYE SIKIA, bubu=ASIYE SEMA mtiririko uwe hivyo....
Mzimu, hapo yanakuja maswala ya language attitude Zeruzeru ni neno la kiswahili tena fasaha (nakubaliana na wewe) ila kimtazamo lipo hasi kwa kiasi furani ukilinganisha na neno Albino (ingawa la kiingereza) lipo neutral, hata upande wa neno kiwete lipo hasi ukilinganisha na mremavu wa miguu, Kwa mtazamo wangu naona neno Albino tulikope na kulitumia kama neno la kiswahili, kwenye lugha inakubarika tu. (borrowing)Nimekua nikisumbuliwa sana na hili jina Albino wakati tangu nazaliwa karibia nusu karne sasa, Neno sahihi la kiswahili ni Zeruzeru. Sijaona ubaya wa neno hilo jamani. Albino sio neno la kiswahili, ni neno la kingereza.
Swali langu, ni kwanini BAKITA = BARAZA LA KISWAHILI TANZANIA, Wamekaa kimya tu kwa upotoshaji huu mkubwa sana.