Bakisha maneno kesho yetu hatuijui

kiroka

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2018
Posts
422
Reaction score
2,008
Ni Ushauri tu, tunaishi na watu ndugu jamaa na marafiki, kuna wakati wanakuudhi au kukera mpaka kiwango cha juu kabisa lakini chora mstari wa maneno yako au matendo yako kuna maneno usitamke wala matendo usifanye bakisha akiba kesho ipo

Unaweza ukagombana na mkeo au mumeo ugomvi mkubwa kweli lkn Siri na madhaifu ya mwenzako epuka kuyaanika kipindi cha ugomvi, maisha yanabadilika kesho unaweza kutamani mrudiane lkn maneno au vitendo vyako ulivotenda kipindi mkiwa wagomvi vikakuhukumu unarudije ni kweli mmesameheana lakn ukiwaza umeshatamka kua huo mume ulie nae alikua hakufikush kilelen leo mmesameheana mnata mrudiane lkn unarudije kwa mwanaume ambaye ushasema hakutoshelezi ndo maana tunasem kipindi cha ugomvi zuia ulimi wako kesho yetu hatuijui.

Unaweza ukagombana na rafiki yako saana ulishare nae Siri nyingi ukigombana nae weka mstari wa maneno na matendo yko kipindi cha ugomvi kesho yetu hatuijui unaweza ukapata shida mtatuzi akawa yeye lkn kwa maneno uliowahi kumtukan unaanzia wapi kwenda kwake kuomba msaada bakisha maneno

Hata ndugu wa kuzaliwa mnaweza gombana ugomvi mkubwa pia mkacharuana saana mkatukanan saana siku mkaitwa kupatanishwa na mkakubalian kuyamaliza lkn km mlitukanan mpk mwisho uhusiano wa mwanzo hauwezi kurudi hii inasababishwa na maneno mliyotamkiana wakati wa hasira

Kuna watu leo wanashindwa kurudisha mahusiano kwa sababu ya maneno waliowahi kutukanana kibinadamu kuna vitu havisameheki unaweza ukasema umesamehe lkn baado ukikumbuk maneno na kejeli zao moyo bado unauma

Hata kwenye vita vya mataifa na mataifa kuna silaha huruhusiw kuzitumia ingawa tupo vitani hata kwenye mahusiano pia ingawa tupo kwenye ugomvi kuna mstari unatakiwa usivuke maisha yana Siri kubwa kesho yetu hatuijui, idd mubarak
 
Kuna baadhi ya watu usipowaambia baadhi ya vitu wanajiona Mungu watu
Chagua maneno
 
Ukweli mtupu! Yaani mtu anakudhalilisha hata hasira zikiisha na kusamehe lakini huwezi kusahau hata siku moja tuweke akiba ya maneno!
 
Hakika, kuna maneno mengine unaweza ukayaropoka kwa hasira, baadae mkishasameheana ata kumuangalia au ukikutana nae popote unaona aibu. Tuchunge vinywa vyetu.
 
Hasa hasa hawa wanawake na ma~last born,hawanaga chujio la maneno!!
 
kama kesho yetu hatuijui ni bora kusema kilakitu, kwasababu unaweza ukafa kabla ya hiyo kesho.
 
NB:Kuweni making pia na maneno ya KUAMBIWA na watu hasa majirani kipindi Cha ugomvi wenu.asilimia 99 Ni waongo Sana.
Utasikia Eti mkeo alisema humfikishi,Eti mkeo alisema sijui nini I'll tu wakuchote akili zako wajue wewe unasema nini!
KUWENI MAKINI SANA.SIO KILA UNALOSIKIA NI LA KWELI
 
Ukweli mtupu! Yaani mtu anakudhalilisha hata hasira zikiisha na kusamehe lakini huwezi kusahau hata siku moja tuweke akiba ya maneno!
Maneno ya KUAMBIWA,changanya na zako.Wengi wanasema alisema hivi na vile ili kukuchota akili wasikie unasemaje.
 
Umeongea maneno yenye maana sana... Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…