Bakili Muluzi Sec.School (aka Shule ya Komba).

Kisoda2

JF-Expert Member
May 30, 2008
2,475
745
Maringira ya yanayoizunguka shule hii yanahatarisha afya kwa wanafunzi na makazi ya watu wanaoizunguka shule hii iliyopo maeneo ya Mbeni.
Tatizo kuu ni ukosefu wa mifumo ya maji taka hasa mfumo mzima wa vyoo kwani maji taka hayo yamekuwa yakimwagika ovyo na kusambaa katika mifereji iliyopo kando ya barabara na kuwa kero kwa wananchi wakaazi wa eneo hilo.
Tatizo hili lilifika katika kamati ya ulinzi na mazingira eneo hilo na wakatumwa wawakilishi ili kwenda kuongea na uongozi wa shule lakini hawakuweza kuongea nao baada ya kujibiwa kuwa wao si wakaguzi ila wapo wanaoweza kujakuikagua shule,hivyo kiongozi mkuu huyo aliwataka waondoke eneo la shule.
Taarifa hizo alipewa DIWANI wa Mbweni Mh.Hashim Mbonde na kuahidi kutoa namba za wahusika wa jiji, kwa kamati ya mazingira.
Hadi sasa mazingira yako vile vile.Na hivi juzi tu,imeripotiwa kuwa El-nino Kuipiga Tanzania.

Je,kwa mazingira haya usalama upo kweli?
Je,hawa wanaokwenda kumkagua huyu kiongozi wa shule wana kagua nini ,na ni wa kutoka wapi?

Hali ndo kama inavyojionyesha katika picha hizi.

Naomba wadau mtusaidie tuwanusuru watoto wetu na maradhi ya mlipuko.
 

Attachments

  • Shule na mazingira 007.jpg
    Shule na mazingira 007.jpg
    25.6 KB · Views: 117
  • Shule na mazingira 006.jpg
    Shule na mazingira 006.jpg
    19.8 KB · Views: 109
  • Shule na mazingira 005.jpg
    Shule na mazingira 005.jpg
    37 KB · Views: 109
Hivi mabwana afya mwisho wa kukagua usafi ni manzese tu?
 
Waafrika tuna matatizo. Pale Jangwani kuna nyumba nzuri sana zimejengwa lakini mabomba yake ya ****** yanamwaga uchafu kwenye mfereji ambao hatua tano hadi kumi tu mbele yake wakulima wa mboga mboga wanachota uchafu huo huo na kumwagia mboga zao kama nyanya, biringanya na kadhalika tunavyonunua mitaani huku tukiambiwa tusivicemshe sana ili tusiaharibu chembechembe zake za uhai sijui nini!!!!
 
Back
Top Bottom