Bajeti yetu lazima iakisi maisha ya waliowengi

karama kaila

Senior Member
Jan 30, 2015
122
60
Tunafahamu kuwa tayari bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 tayari imepitishwa na ipo katika hatua ya utekelezaji.

ACT Wazalendo kama chama cha siasa tunaowajibu wa msingi kuuelimisha umma wa watanzania kufahamu vizuri kuhusu bajeti na pia kuendelea kuishauri na kuikosoa Serikali katika yale mambo ambayo tunaamini hayatekelezwi katika msingi wa kutoa matokeo yenye tija kwa wananchi.

_"Bajeti ina maana gani kwa Wananchi?_

_Tunapotazama maana ya Bajeti kwa wananchi hatuna budi kuangalia mambo ya msingi kama bei za bidhaa za huduma._

_Iwapo shilingi 1000 aliyonayo mwananchi leo ingenunua bidhaa nyingi zaidi kuanzia Mwezi Julai mwaka 2016, tungesema hali ya maisha ya mwananchi imeboreka._

_Iwapo shilingi 1000 aliyonayo mwananchi leo inanunua bidhaa chache zaidi tangu kuanza mwaka mpya wa fedha tunasema hali ya wananchi imeporomoka._

_Serikali imepandisha kodi mbalimbali kwenye bidhaa zinazoagizwa kutoka nje na ushuru wa bidhaa mbalimbali. Hii inapelekea bei ya bidhaa na huduma kupanda na kusababisha mfumuko wa bei tofauti na malengo ya Serikali. Serikali inatarajia mfumuko wa bei kuwa katika tarakimu moja. Hata hivyo uchumi wetu unategemea sana uchumi wa Dunia kwa sababu tunaagiza zaidi ya uwezo wetu wa kuuza nje._

_Bei ya Mafuta katika soko la dunia imeanza kupanda taratibu na sasa imefikia $50 kwa pipa moja kutoka chini ya $30. Uzalishaji wa kilimo umekuwa hauridhishi kwani chakula ni sehemu kubwa ya mfumuko wa bei (huchangia takribani asilimia 52 ya kapu la bidhaa na huduma)._

_Kuna mwelekeo mkubwa kwamba mfumuko wa bei utaongezeka mpaka kwenye taratimu mbili na hivyo kupelekea hali za wananchi kuwa mbaya._

_Kodi za miamala ya kutuma fedha kwenye mabenki au simu za mkononi inabidi zitazamwe upya ili kuhakikisha kuwa malengo ya Serikali ya kuwaingiza wananchi wengi katika mfumo wa kibenki yanafanikiwa._

_Serikali imeamua kubana matumizi kwenye baadhi ya maeneo, ni jambo jema sana. Hata hivyo uamuzi huo utaendana na biashara nyingi kufungwa na watu wengi kupoteza ajira na kuingia mtaani. Hii inaweza kuongeza ugumu maisha kwa wananchi wengi wa kawaida."_

ACT Wazalendo inaitaka Serikali katika kutekeleza bajeti ya sasa ni lazima ihakikishe utekelezaji huo unalenga kuleta unafuu wa ughali wa maisha kwa wananchi wote. Matarajio ya wananchi wengi kwa Serikali yao ni kuona hali zao kimaisha zinabadilika. Ili hilo lifanikiwe ni budi Bajeti hii iakisi uhalisia wa maisha ya watanzania.
 
Back
Top Bottom