Bajeti yapitishwa kwa kejeli.

Bajeti yapitishwa kwa kejeli.

Naomba tuu wabunge wetu wa ccm, ninyi ni watu wastaarabu, wasikivu, waelewa mambo kuwa bungeni sio mahali pa mipasho. Tulidhani mipasho ingetokea upinzani kwani ni wageni wa bunge letu tukufu kumbe imekuwa tofauti??? cdm walikuwa wapi hapo bungeni mlipokuwa mnajadili?? Kwa nini msiwaache hivyo hivyo kwani ni mpaka muwakumbuke kwenye kupitisha mlichokijadili wenyewe? Wangepinga nini? Lakini, ili tuu sauti yako isikike, unaambiwa jadili matatizo yaliyoko kwenye jimbo lako, wewe unajadili maandamano yapigwe marufuku kuleeee. Mwehu hapa ni yupi? Huu sio wakati wa kujadili maandamano bali ni kupitisha bajeti jamani. Hawa Ghasia, mama yangu hivi kweli bajeti na mkoa wa kilimanjaro wapi na wapi?? Sielewi, ati wanataka kuwapima watu akili, huyu tutampima nini?? Hivi akili yake ilikuwepo kweli?? Dakika kumi zote unapoteza kuimba ngojera??
 
Back
Top Bottom