Bajeti ya Shamuhuna yapitishwa kwa ‘mbinde’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ya Shamuhuna yapitishwa kwa ‘mbinde’

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jul 13, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Bajeti ya Shamuhuna yapitishwa kwa ‘mbinde’ [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Tuesday, 12 July 2011 21:49 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Salma Said, Zanzibar
  WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wamepitisha kwa tabu bajeti ya Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati, baada ya wajumbe wengi kutaka ufafanuzi wa kina na kauli ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuhusu hatma ya mafuta na gesi asilia kutolewa kwenye orodha ya mambo ya Muungano.
  Akifanya majumuisho yaliyochukua muda mrefu, Waziri wa wizara hiyo, Ali Juma Shamuhuna alisema tayari mafuta na gesi asilia limemalizwa ngazi za uamuzi, msimamo ni kwamba suala hilo ni la Wazanzibari na wanasubiri hatua za kutayarisha sheria.


  Shamhuna alisema suala la mafuta limeshatolewa uamuzi tangu baraza lililopita na tayari Baraza la Mapinduzi, limejadili kwa kina hasa kwa kuzingatia linagusa Wazanzibari wote, huku mipango ikiendelea kuhakikisha linaondolewa orodha ya mambo ya muungano.Alisema moja kati ya mgogoro uliomo kwenye katiba ya Tanzania ni mafuta, lazima ushirikiano upatikane kuepuka baadhi ya wengine kuonekana wasaliti, kwani masuala kama hayo wapo wanaokuwa na misimamo tofauti.

  “Napenda kuahidi, katu sitorudi nyuma kwa suala la mafuta kama lilivyoamliwa katika baraza hili, nakupongezeni sana kwa kuguswa na suala hili, ujumbe wenu umefika kunakohusika na wameusikia wenzetu,” alisema Shamhuna.Kuhusu Katiba ya Zanzibar na Muungano, Shamuhuna alisema zote zina matatizo na ndiyo chanzo cha mgogoro unaoendelea juu ya umiliki wa mafuta na gesi, lakini aliwataka wananchi kuwa kitu kimoja kama Wazanzibari.

  Waziri Shamuhuna alisema wakati umefika kwa Tanzania bara kuwaachia Wazanzibari haki ya umiliki wa rasilimali zao, huku akisisitiza suala la mafuta kwenye bahari kuu ya Zanzibar lipo chini ya SMZ, haoni sababu za kuendelea kujadiliwa.

  “Vikao vilivyopita suala hili tayari tulikuwa tumelijadili na maoni ya wananchi kupitia wawakilishi wao serikali imeyafanyia kazi, lakini kubwa ni uamuzi wa kuondoa mafuta katika orodha ya mambo ya Muungano umekwisha,” alisema Shamuhuna.

  Licha ya Shamuhuna kueleza kwa ufasaha suala hilo, wawakilishi hawakuridhika na ufafanuzi huo jambo ambalo lililowalazimu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Othman Masoud na Waziri wa Katiba na Sheria, Abukakari Khamis Bakari, kusimama mara kwa mara kujibu hoja.Othman alisema suala la mafuta linahitaji umakini na kuwapo utaratibu maalumu, ili kuepuka machafuko kama yale yanayoshuhudiwa nchi nyingine, huku akiwasisitiza wajumbe kuwa na busara kwenye suala hilo.

  Alisema Zanzibar inahitaji kuunda sheria ya mafuta, kwani hivi sasa haipo na sheria ya mwaka 1951 imekufa baada ya mafuta kuiingiza kwenye orodha ya mambo ya Muungano.

  Naye Waziri Abubakari alisema serikali lazima ikae kutafuta mbinu ya kulitoa katika orodha ya Muungano kwanza, halafu hatua zingine zifuate.“Suala la mafuta limeshaamulia na Baraza la Wawakilishi, serikali inalishughulikia kwa maslahi ya wananchi wa Zanzibar, tunalishghulikia kwa nguvu zetu zote na katika hili msimamo wetu upo wazi kwamba tutaheshimu na kutekeleza maoni ya wananchi”, alisema.  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   

  Attached Files:

Loading...