Gibiba
Senior Member
- Jun 22, 2016
- 114
- 27
Nianze kwa kuishukuru serikali ya rais Magufuli kwa kuthubutu kukabili miradi ya maendeleo kwa kutegemea vyanzo vya ndani.
Lakini zaidi niishukuru sana serikali kwa mara ya kwanza kuvunja rekodi kwa kutenga zaidi ya 40% ya bajeti hiyo kwa kuielekeza katika miradi ya maendeleo.
Hii tu ni ishara tosha kwamba ile dhana ya hapa kazi tu ni dhahiri kuwa ni elimu kwa vitendo na sii nadharia.Hapa Mh.rais "conglatulation"
Kikubwa nilichokibaini kwa watanzani ni genge kubwa la wakwepa kodi. Ikumbukwe kuwa kila kunapokucha mahitaji ya mtanzani yanaongezeka na itambulike kuwa vivyo hivyo gharama za maisha pia zitaongezeka.
Kwa watanzania wavivu na mawakala wa wakwepa kodi, hili limekuwa kinyume.
Binafsi nimeanza biashara tangu mwaka 2008 kama mjasiriamali mdogo na tangia hapo nimekuwa mlipa kodi mzuri na sikuona adha yeyote kwa maana natambua jasho langu ni sehemu muhimu katika ujenzi wa taifa. Hata hivyo viwango vya kodi vimeendelea kubadilika kila mwaka, mimi na wazalendo wengine tumeendelea kulipa kodi vizuri sambamba na hayo mabadiliko ya viwango vya kodi.
Kichekesho sasa ni kwa serikali ya hapa kazi,nimepata kugundua kuwa liko wimbi kubwa la watu hawakuwahi lipa kodi na hawako tayari kulipa kodi. Lakini kundi hili kwa tafiti tu za haraharaka ndio wa kwanza kupaza sauti kulia maisha magumu maana ni wavivu.
Kelele zimeibuka kila kona na hasa kwa wanasiasa ambao kazi yao ni kukimbizana na matukio.Hali hii pia imenifanya kugundua kumbe kundi kubwa la wenye nacho ndio walikuwa wakwepa kodi wakubwa, lakini zaidi walikuwa kwenye misamaha ya kodi isiyo na tija.
Viinua mgongo vya wanasiasa vilikuwa kwenye misamha ya kodi licha ya kwamba wao haohao ndio watunga sheria.Sasa sheria ni msumeno serikali ya hapa kazi tu imekuja na mifumo mipya ya ukusanyaji kodi.
Mawakala wa wakwepa kodi milango yao imefungwa, sasa ni kilio kila kona. mara ooo anabana demokrasia, mara ooo anaingilia mihimili mingine ya serikali na mengine makubwa kwamba yeye ni dictator uchwara.
Tungeyajua yoote haya kama sii umahiri wa Dr.Magufuli?Wako watu walikula kiulaini kwa kutegemea jasho la wenzao mf. wamiliki wa nyumba, MC na wengine. Sasa hivi wanalipa kodi licha ya kuwa wanalalamika.
Hivi ni kweli wao kutoza kodi kwa wapangaji ni halali lakini wao kutozwa na serikali sii halali?
Ndugu zangu! Ya Mungu mpeni Mungu na ya kaisari mwachieni kaisari.
Niwaombe watanzani wenzangu tujenge utamaduni wa kulipa kodi maana ni kitendo cha uzalendo na kwa kufanya hivyo utajijenga vyema kutumia cha kwako halali.
Na ukiujenga utamaduni huu, hutafikiri kuonewa na hali utaiona ya kawaida kabisa. Zaidi hapa ni kuthubutu na kumuunga mkono rais wetu katika mpango wa kulisukuma taifa kuufikia uchumi wa kati.
Sote tulipe kodi, tuache kulialia mitandaoni.