Bajeti ya pombe yazua zogo kubwa

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,769
10,650
Usiku huu nikiwa maeneo ya Gongola mboto katokeza jamaa mmoja amelewa tilalila. Akakatiza pale tulipokuwa tumekaa, ikabidi tumpe ushauri wa bure kwa jinsi alivyokuwa anapepesuka. Tukamshauri achukue japo bajaji kwa vile anaweza gongwa na gari. Ee bana eeh! Jamaa alituchana chana ile mbaya! "Hivi nyie mnaishi Tanzania gani? Bila sisi kulewa si mngetumikishwa na akina David Cameroon nyie? Majuha wakubwa msio na shukurani nyie." Mengine hayaandikik hapa. Kilichofuatia siwezi kisimulia kwa vile ni kujitwalia sheria mkononi kama kalivyo ka utaratibu ka watanzania.

Onyo: Walevi wapewe heshima wanayostahili.
 
Nakumbuka huko Zenji walishakataa udhamini wapombe. Sasa sielewi kwa nini ishu ya mapato ya serikali yanayotokana na pombe wanaipotezea!!
 
jiulize muungano wanautaka bado,ninavyoona wote wapo tayari kujinasua waishi kivyao ndio maana wakawa kimya na ishu hiyo
 
Mi naona kila,mchango ni lugha gongana, nitarudi baadae kuchungulia.
 
zanzibar na waislam wote waungane kukataa mapato yanayotokana na kodi za pombe ndo ntaamin kuwa wanafuata dini kweli kweli!
 
kwani kupandisha kodi ya pombe ina maana serikali inategemea wanywaji pombe??!!
mbona mnamtazamo mmoja tu.
kwa nini hamji na mtazamo kuwa serikali kwa kupandisha kwake kodi ya pombe inafanya bidhaa hiyo kupanda bei hivyo kuwanusuru wananchi wengi kutoiyendekeza kila wakati,badala yake hela zao za kulewea waziekeze katika kujenga familia zao,na taifa kwa ujumla.
 
fuatilia nchi za magharibi,ni mabilioni mangapi ya dola hulipwa na makampuni ya sigara kwa serikali kutokana na madhara ya bidhaa hiyo!
je ni kwa kuwa bajeti zao zinategemea faini hizo??!!
au ni kwa kuwa nchi hizo zinawajali wananchi wao??!!
 
Back
Top Bottom