Bajeti ya ofisi ya CAG kupunguzwa kwa asilimia 50, nini maana yake?

mcoloo

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
918
1,401
Screenshot_20190606-052508-707x950.jpg


Katika magazeti ya leo nimeona ofisi ya CAG imepunguziwa bajeti kwa asilimia 50℅, hii maana yake nini has a ukizngati kuwa ofisi hii ndio jicho la taifa na msema kweli pale kodi za wanyonge zinapo tumiwa vibaya na hao waliopewa dhamana.

Tangu ofisi hiyo iibue ufisadi mkubwa unaofanyika kwenye utawala huu, imezua nongwa kweli kweli, mara bunge hawataki kufanya kazi na CAG, mara aitwe kwenye kamati ya maadili ya viongozi. La ajabu kubwa sasa wameamua kuinyima ofisi fedha kwa lengi la kudhohofisha utendaji wa kazi.

Nchi hii tuna kwenda wapi mbona viongozi was awamu hii hawataki kukosolewa, mbona wanapenda sana kufanya mambo muhimu hasa yanayohusu fedha yasijulikane kwa wananchi?

Mawaziri wamebakia kusifu eti mambo yaliyo fanywa na awamu hii ijawahi tokea tangu nchi imepata Uhuru, inaweza kuwa kweli kwa sababu kadhaa , ambazo ni pamoja na wanchi kuingizwa kwenye umaskini , kama mtembeza mchicha ambaye mtaji wake ni sh 5000/= unambana anunue kitambulisho cha sh 20,000/=maana yake nini kama si kumletea umaskini tu.

Inawezekana kuwa awamu hii imefanya makubwa kwa wizi ambao toka awamu zote zilizopita haijawahi tokea, ndiyo toka awamu zote hakuna wakati ambao viongozi wamejimilikisha fedha kama awamu hii.

Huwa natafakari sana viongozi wetu wanaosifia sifia kila jambo hivi ikitokea leo mmoja wao apoteze kazi na aje aishi maisha anayo ishi mtanzania wa chini hivi atamaliza wiki kabla hajafa kweli? Ifike mahali viongozi wetu wawajali wananchi na sio kusifia sifia tu hata mambo yasiyo hitaji sifa.

Mimi nawapongeza wazimbabwe kwa kukataa misifa isiyo kuwa na maslahi kwa taifa lao.

Mungu tu atunusuru na hili janga.


=====

Bajeti Ofisi ya CAG yafyekwa

MAKADIRIO ya matumizi ya fedha katika Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa mwaka ujao wa fedha yamepunguzwa kwa Sh. bilioni 7.791 kulinganishwa na ya mwaka huu.

Kwenye ukurasa wa 175 wa kitabu cha hotuba ya makadirio ya bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka ujao wa fedha, inabainishwa kuwa kwa mwaka ujao, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi inatarajiwa kutumia jumla ya Sh. bilioni 61.377.

Kati yake, Sh. bilioni 55.077 ni matumizi ya kawaida (mishahara Sh. bilioni 14.084) na matumizi mengineyo Sh. bilioni 40.993) na Sh. bilioni 6.3 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Makadirio hayo yaliwasilishwa bungeni jijini Dodoma Jumatatu na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango na kuidhinishwa na Bunge siku hiyo hiyo.

Kwa mwaka huu wa fedha (2018/19), Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ambayo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ni mkuu wake, iliidhinishiwa na Bunge matumizi ya Sh. bilioni 69.106.

Kati yake, Sh. bilioni 55.394 zilikuwa za matumizi ya kawaida (mishahara Sh. bilioni 16.648 na matumizi mengineyo Sh. bilioni 38.746) na Sh. bilioni 13.712 zilikuwa za miradi ya maendeleo.

Hata hivyo, katika hotuba yake hiyo, Waziri Mpango, hajaeleza sababu za kupunguzwa kwa makadirio ya matumizi katika ofisi hiyo.

Akiwasilisha hotuba yake bungeni Jumatatu, Dk. Mpango aliliambia Bunge kuwa katika mwaka ujao wa fedha, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi itaendelea kuimarisha ukaguzi wa mapato na matumizi ya serikali kwa lengo la kuimarisha uwajibikaji na uwazi kwenye matumizi ya rasilimali za umma.

Katika kufikia malengo hayo, waziri huyo alisema ofisi imepanga kutekeleza vipaumbele vinane ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi wa mafungu ya mapato na matumizi ya wizara, idara za serikali zinazojitegemea, wakala na taasisi za serikali, sekretarieati za mikoa, mamlaka za serikali za mitaa katika mikoa yote nchini na mashirika ya umma.

Alisema Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi pia itakagua miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na wahisani, ifanye ukaguzi wa kiufundi kwenye maeneo yenye uwekezaji mkubwa wa rasilimali za umma kama vile ujenzi wa barabara na viwanja vya ndege, reli ya kisasa na miradi ya nishati (umeme).

Chanzo: Nipashe
 
Nimeipenda tu hiyo heading yako! Ha ha ha!

Naona sasa kwa sababu wameshindwa 'kumdhibiti' mdhibiti wameamua kumpunguzia bajeti ili kuhafifisha umuhimu wa kazi yake. Anyway, wala haitakuwa shida maana anaweza kutumia atakachopewa kufanya kinachowezekana tu!
 
Bunge dhaifu huilinda serikali dhaifu kutengeneza taasisi dhaifu

Sasa Ndugai roho yake kwatu.

Spika wahovyo kupata kutokea tangu tupate uhuru.

Maana yake Ndugai na serikali yake hawataki kukaguliwa, ili waendeleze wezi

Huwezi kupata ufanisi kama hujitathmini kupitia uchunguzi thabiti kama ule anaoufanya prof Assad
 
Hii yote ni kwa sababu ya 1.5 trillion na baadaye 2.4 Trilion. Na Wabunge wetu wa CCM Wamekubali, hawana aibu kabisa. Ndiyo maana nasema kila siku. Bila kuipumzisha CCM Tutazidi kuogelea ktk dimbwi la umasikini na huku kikundi kidogo kikiendelea kuitafuna Nchi kitakavyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom