Bajeti ya magari ya Ikulu yapaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ya magari ya Ikulu yapaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyambala, Jun 17, 2010.

 1. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Bajeti ya magari ya Ikulu yapaa

  Source: Raiamwema

  BAJETI ya Serikali ilipitishwa juzi jioni huku matumizi kadhaa, yakiwamo ya Ikulu, yakiwa yamepanda kutoka Sh. bilioni 7.23 hadi bilioni 8.8, yakigusa posho, safari za nje, ununuzi vinywaji na vitafunio kwa ajili ya kukirimu wageni na matengenezo ya magari ambayo hivi karibuni yalikumbwa na matatizo wakati Rais Jakaya Kikwete akiwa katika ziara jijini Dar es Salaam.

  Ongezeko la matumizi hayo linakwenda sambamba na ongezeko la bajeti Sh. trilioni 9.5 hadi Sh trilioni 11.1.

  Hata hivyo, katika baadhi ya maeneo viwango vya fedha vilivyotengwa katika bajeti inayokwisha vimepunguzwa katika bajeti ya sasa ya mwaka wa fedha 2010/2011. Miongoni mwa maeneo hayo ni safari za ndani ya nchi ambazo fungu lake limekatwa kutoka Sh. milioni 732.4 hadi Sh. milioni 668.4 zinazokadiriwa kutumika mwaka mpya wa fedha.

  Fungu hilo la safari za ndani limeonyesha mwelekeo wa kupungua mwaka hadi mwaka na kwa Mwaka wa Bajeti wa 2008/2009 lilikuwa na Sh. 839,807,283.

  Katika eneo la matengenezo ya magari, ambayo hivi karibuni yalizua mtafaruku baada ya kung'oka matairi, mwaka jana zilitengwa Sh. milioni 120 ambazo katika mwaka huu wa bajeti zimepanda hadi Sh. milioni 167.4.


  Fungu kwa ajili ya posho limeongezeka kutoka Sh. milioni 611.9 hadi milioni 713.9 wakati matumizi kwa ajili ya mafuta na vimiminika vingine vya magari yameongezwa kutoka Sh. milioni 344.9 hadi milioni 389.8.

  Kwa mujibu wa bajeti hiyo ya Serikali iliyopitishwa na Bunge Jumatatu, bajeti kwa ajili ya matumizi ya kukirimu wageni ikiwamo ununuzi wa vinywaji, vitafunio na huduma nyingine aina hiyo Ikulu yameongezeka kutoka Sh. milioni 444.4 za mwaka unaokwisha wa bajeti hadi Sh milioni 566.44.

  Ununuzi wa mashuka, nguo, viatu na huduma (za utunzaji wake) umetengewa fungu la nyongeza kutoka Sh. milioni 116.4 hadi milioni 160.

  Kwa upande wa safari za nje makadirio yaliyopitishwa na Bunge mwaka huu yanaonyesha kuwa yamepanda kutoka Sh milioni 115. 9 za mwaka unaokwisha hadi milioni 164 . Mwaka wa bajeti wa 2008/2009, safari hizo ziliidhinishiwa Sh. milioni 77.8.

  Hata hivyo, inaelezwa kuwa kiwango kinachopitishwa cha matumizi ya Serikali wakati mwingine hutumika na kumalizika kabla ya wakati uliopangwa na matokeo yake ni ongezeko la matumizi ambayo yanalazimika kuidhinishwa kwa hati ya dharura na Bunge.

  Ofisi ya Makamu wa Rais fungu lake la matumizi limeongezeka kutoka Sh 4,492,974,000 za mwaka unaokwisha wa bajeti hadi Sh bilioni 4,542,109,000 zikigusa matengenezo ya magari kutoka milioni 144 hadi milioni 168.

  Hata hivyo, katika hali inayozua maswali mengi ofisi hiyo ya Makamu wa Rais katika bajeti mbili mfululizo Bunge limekuwa likipitisha fedha kwa ajili ya ukarabati wa mabomba ya maji na mfumo wa umeme.

  Mwaka jana na mwaka huu wa bajeti eneo hilo limetengewa kiwango kinacholingana ambacho ni Sh milioni 20, wakati mwaka juzi zilitengwa Sh milioni 17.

  Matumizi haya ya Serikali yameongezeka wakati kukiwa na maelezo miongoni mwa waziri kuwa Tanzania imeathiriwa kwa kiasi kikubwa na mtikisiko wa uchumi duniani, ulioanzia Marekani, Ulaya na baadaye kuathiri nchi za Afrika.

  Lakini pia matumizi hayo yanapanda katika wakati ambao wananchi wamekuwa wakilalamika na kuitaka Serikali kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na wakati huo kuwekeza zaidi katika maeneo ya miradi ya maendeleo inatajwa kuwa uwekezaji wake kutoka serikalini umekuwa dhaifu na kwamba kwa kiasi kikubwa miradi hiyo inategemea fedha za wahisani.

  Katika bajeti ya mwaka huu, nchi wahisani zimepunguza kiwango cha msaada wao kwa serikali ya Tanzania hali iliyolazimu Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Uchumi kuingia katika mazungumzo na Benki binafsi ya Stanbic, ili ikopeshwe kiwango cha fedha kufidia pengo la wafadhili. Serikali imepanga kukopa Stanbic Sh bilioni 346 katika lugha inayoelezwa na serikali kuwa ni kwa "masharti nafuu" ili kuhakikisha matumizi yake yanatimia.  My Take:

  Hii nchi yetu tunayosema masikini mbona inachekesha

  1. Mengi ya Magari ya ikulu ni mapya na hivyo yatakuwa na warrant, sasa ni matengenezo gani ambayo yatagharimu pesa kiasi hicho maana nnavyofahamu kwa gari mpya hadi service ni free.

  Wakuu sina uhakika ikulu ina magari mangapi lakini let's say 50 which sounds reasonable, in that respect bajeti ya matengenezo per car ni 167mn/50 = 3.34 Tshs milioni kwa mwaka. Unatumiaje hela hiyo kwa gari mpya kwa matengenezo?

  2. Mafuta na the so called vimiminika, I guess it's lubricants. 389mn/50 = 7.78 million Tshs per car per year. Kwa bei average ya 1700Tshs/ L = 4576.5 Lts. Kwa average ya 12 Lts per 100Km. Mafuta hayo yanatosha kutembea km 38,133.33. Kwa kumbukumbuku urefu wa reli ya Tazara ni km 1860. Hivyo basi kwa makadirio hayo bajeti ya gari ya ikulu kwa Mwaka ni sawa na kusafiri Dar - Kapirimposhi mara 38,133.33/1860 = 20.5. Really? are we serious. Hawa jamaa huwa wanasafiri kwenda wapi? Nimeacha lubricants makusudi kwa sababu hizi hubadilishwa bure wakati wa service kwa magari mapya.


  Well hela hizi si nyingi sana kwa nchi ambayo ina uchumi mzuri na inajitegemea. Lakini kwa nchi masikini ambayo bajeti yake 40% inategemea misaada kuna haja ya kufanya a serious turn around.
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hivi Tanzania angekuwa ni mtu (individual), mbona angekuwa ni kituko, yaani prioritizing ni sifuri kabisa!
   
 3. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Halafu baada ya matengenezo yote hayo linachomoka tairi.... duh, kazi kweli kweli...

  ..Siku gari la Ikulu lilipopata hitilafu, kwanza kuna dereva teksi mmoja alikuwa jirani na tukio lile tairi lililochomoka likagonga gari yake, alipoenda Chang'ombe polisi akaambiwa asifungue kesi maana yale magari hayana bima na kwamba atalipwa tu gari yake... lakini papo hapo akatokea fundi mwingine akasema, "jamani haya magari huwa hayafanyiwi service kabisa na watu wanaopewa jukumu hilo hupanga bajeti na kwenda Kariakoo kufanya "dili" na wenye maduka ya spea na kununua spea hewa. Nikakumbuka kuna siku nikiwa nanunua spea pake Kariakoo, nikakuta kuna mtu kavaa ovaroli la bluu, ana makatasi ya serikali (Ikulu) akawa anaandikwa ankara ndefu ya bei za spea na alikua ana cheki anakabidhi hapo dukani. Nikajiuliza je, ule utaratibu wa magari ya serikali kutengenezwa na karakana ya serikali umeishia wapi? hivi Wakala wa Magari ya Serikali imeanzishwa ya nini? Jamani huu ulaji (ten percent), undugunaizesheni katika ajira (hata IKULU) na uzembe (pamoja na wanaochekea wazembe) ni mambo yatakayotumaliza.
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Naona namba tu zinaongezeka ili watawala wetu wale vizuri.
   
 5. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,010
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Kuna anayeweza kuweka kuwa pesa hizo za matumizi ya ikuli ni asilimia ngapi ya bajeti nzima? Elimu, afya navyo ni asilimia ngapi ya bajeti?
   
 6. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Mhhhhhhhh no comment :A S-alert1:
   
 7. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,689
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hivi magari ya Ikulu si pamoja na Usalama wa Taifa etc?
   
 8. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  :angry:.....:embarassed2:....:A S-devil1:
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  I don't think so mkuu, maana uwt wako chini ya wizara ya sofia simba. Sema wale waliokko ikulu offcourse watakuwa wanatumia magari ya ikulu.
   
Loading...