Bajeti ya kwimba yapelekwa Dar kihuni.

mandago shululu

Senior Member
Mar 24, 2013
125
36
Vikao vya kupitisha bajeti ya Halmashauri ya wilaya ya kwimba kwa mwaka 2016-2017 vilianza tarehe 2 na 3/02/2016.

Kitu cha kushangaza makablasha ya bajeti yaliletwa huku tayari yakiwa yamesainiwa na Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya kwimba.

Vilevile,baada ya majadiliano kuanza watu muhimu kama Mkurugenzi,Mkuu wa Wilaya Pamoja na Afisa Mipango hawakuwepo ndipo wajumbe wakaomba muongozo juu kutokuwepo kwa watu muhimu kama hao wakati wa kupisha bajeti,lakini majibu yakiyitolewa na M/kiti wa Halmashauri yalikiwa siyo ya kuridhisha kwa wajumbe.

Kumbe jibu sahihi ni kwamba walikuwa wameshapeleka bajeti tayari kwa majadiliano ya bunge.

Kama huu ndio utaratibu wa kupitisha Bajeti Majipu hayataisha.

Mh,Rais,Mh Waziri mkuu,Mh Simba chawene njooni kwimba mtuondolee haya majipu yapo mengi mno yanazidi kuambukizana wala hayaogopi kuna kwamba sehemu zingine yanatumbuliwa,Tunayafahamu kwa Idara na kwa Majina.

Karibuni tutawapa ushilikiano ili tujenge nchi yetu pasipo na majipu.

Mh,Mandago/Diwani
K/Tibu Chadema (W) Kwimba
0765183733/0782270412
 
Kwimba ni Sugu,pale halmashauri panahitaji kutumbuliwa,kuanzia Idara ya elimu na kwingine ni uozooo.
 
Back
Top Bottom