Bajeti ya bunge yaongezeka na kufikia bilioni 70… | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ya bunge yaongezeka na kufikia bilioni 70…

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 1, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  April 1st, 2011

  Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda amesema kuwa bajeti ya bunge imeongezeka kwa mwaka wa fedha 2009/2010 na kufikia Zaidi ya tsh. Bilioni 70 kulinganisha na ile ya mwaka 2006/2007 ambayo ilikuwa zaidi ya tsh. Billion 26 ni sawa na asilimia 165.5.Pinda aliyasema haya leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Tume ya Utumishi ya Bunge, ambayo yeye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, na kusema bajeti hiyo imeongezeka kwa sababu ya kuuwezesha mhimili wa Bunge kutekeleza majukumu yake ya kikatiba na bila usumbufu.

  Aliendelea kusema pia idadi ya wabunge imeongezeka kutoka wabunge 295 mwaka 2005 hadi kufikia 360 kwenye bunge la sasa kwa maana hiyo ni lazima kasi ya utoaji huduma nayo iende sambamba na kuongezeka idadi ya wabunge, wabunge walio ongezeka ni vijana kati ya idadi hiyo kuna ongezeko la asilimia sita (6%) ya wabunge wanawake ambao hivi sasa wamefika jumla ya 126, kati ya wabunge 350 na hivyo kufanya idadi yao kuwa ni asilimia 36 ya wabunge wote.


  [​IMG]
  Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akizungumza wakati akizinduzia Tume ya Utumishi wa Bunge jijini Dar es Salaam.

  [​IMG]
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisoma risala kwa Mgeni rasmi Mhe. Mizengo Pinda.
  [​IMG]
  Waziri Mkuu akimkabidhi Spika wa Bunge cheti cha Utumishi bora.
  [​IMG]
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi cheti cha Utumishi bora Kamishna Mstaafu na Mpya Mhe. Abdulkarim Shah.
  [​IMG]
  Waziri Mkuu akimkabidhi cheti cha Utumishi bora kwa Bunge la tisa Mbunge Viti Maalum Mhe. Kidawa Saleh.
  [​IMG]
  [​IMG]
   
 2. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Haya mambo ya kupongezana wao kwa wao bila ya kuzingatia maoni ya watu hayawezi kutufikisha popote. Huyu mama wa viti maalum anayepewa cheti cha utumishi bora kwa bunge lililopita ametoe mchango gani? Kama wananchi wangelishirikishwa katika uteuzi huo, hapana shaka wengi wangelisema kwamba anayestahili kupewa cheti hicho ni rais wao wa moyoni Dr.Slaa na si mwingine.
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Oh yeah wanapongezana sababu wanajua hizo bil 70 pia zitafika kwenye matumbo yao
   
 4. 2

  250689 Member

  #4
  Apr 1, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wasijifikirie wao tu..watukumbuke na sisi walalahoi huku mitaani kwani wengi wetu hatujui hata kesho tutaamkaje,hali ni mbaya jamani.
   
 5. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Nor does gentlemen ever behave like this ..
   
 6. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sijui zitto ana wawasha nini hata
   
 7. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kweli Mheshimiwa Waziri Mkuu, Tanzania hii ni Bungeni tu kunakohitajika kutekelezwa mambo kwa kuhakikisha fedha zinatosha kwengineko NO hata mabomu yanaweza kusubiri.
  Najiuliza tu hili bunge ni la CCM peke yao wengine wanaojidai wana uchungu na wananchi hawamo humu?
   
Loading...