Bajeti ya 20012/2013 na marekebisho ya kodi

JUDITH MGASSE

Member
Jun 5, 2012
17
4
Habari za jioni wana JR!
hapa nataka kuzungumzia kidogo bajeti ya 20012/2013 na marekebisho ya kodi ya magari!
yako hivi
a) hakuna excemption kwa wafanyakazi wa serikali,
b) Magari ya mashirika ya dini yatalipiwa kila kitu
c)magari chakavu yanapigwa penalty less than 8 years not 10 years kama ilivyokuwa
hii imepitishwa na ile wanaita general budget and imeanza kauwa implimented pale TRA!

Jamani hivi wafanyakazi wa kawaida wa serikali wana benefits gani! manake ilikuwa walau hii ya excemption kwa wale wachache walioweza kuchukua mikopo wananunua magari walau ya biashara ndogondogo sasa excemption imefutwa mfanyakazi gani wa serikali wa kawaida anaweza kununua gari kwa Tanzania! wabunge chondechonde msiipitishe hii kwenye budget ya wizara ya fedha bila kujali itikadi za kisiasa na bila kujali kuwa ninyi kwa sababu ya uwezo wenu wa kifedha mtaweza kutoa magari yenu! chonde chonde wabunge wetu sisi walalahoi wa serikali hapa hatutatendewa haki kiukweli!

Magari ya mashirika ya dini hasa vijijini ndo ambulence za wananchi akitokea mgonjwa wananchi wanakimbilia kanisani kuomba msaada wa gari! leo magari haya yalipiwe kodi mimi naona hii si sawa! tunawakilisha kero zetu!

Me nafikiri tukubali mzunguko wa shekeli nchi hii ni mdogo there is no equal distribution of money! watu wachache wanashikilia uchumi wa nchi sasa kama hizi sheria zikupitishwa maana yake mtu wa kawaida hawezi kuingiza gari nchini! aliyenacho ataongezewa ndipo tunapokwenda!

Mimi sidhani kama kwa kufanya marekebisho haya itasaidia kukuza uchumi wa nchi! Serikali ikusanye kodi kwa wafanyabiashara ukienda kkoo ni maduka mangapi hutoa risiti hana maduka hasa ya wahindi wanakupa bei mbili bidhaa pamoja na risiti ina bei yake na bila ina bei yake! hivi ninavyoongea kuna watu wameshindwa kutoa magari yao policy imebadilika gafla na watu hawajajiandaa wako frustrated! ni changamoto ki ukweli! Haya ni mawazo yangu lakini wabunge mliangalie hili kwa jicho la ziada! amen
 
Bajeti ya pombe mkuu sidhani kama tutafika unajua serikali imepeleka namba bungeni wakati hazina hakuna pesa.
 
Back
Top Bottom