Pikipiki za umeme za magurudumu matatu (bajaji) zilizoanza kutumika kwa mara ya kwanza katika Maonyesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), zimerahisisha usafiri kwa wageni na washiriki huku zikihamasisha matumizi ya nishatisafi
Tofauti na miaka iliyopita wageni walitegemea huduma zisizo rasmi na zisizo na uhakika za usafiri wa ndani, maonyesho ya mwaka huu yameleta usafiri wa kisasa wa umeme kama mbadala.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), kwa kushirikiana na Shirika la Posta Tanzania (TPC) na wadau binafsi,
imeanzisha huduma hiyo ili kurahisisha mtu kutoka eneo moja kwenda lingine
Kwa mujibu wa TPC, kuna zaidi ya pikipiki 20 na gari ndogo za kubeba mizigo na mabasi ya kifahari kwa ajili ya viongozi waandamizi
Pikipiki hizi zanapatikana kwa Sh5,000 kwa safari ya dakika 30 au Sh2,000 kwa safari ya kawaida kutoka sehemu moja hadi nyingine, huku magari yakibeba mizigo au bidhaa za ununuzi
Maonyesho ya mwaka huu yanatarajiwa kufunguliwa Julai 7 na Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi tofauti na miaka iliyopita yalikuwa yakizinduliwa mapema zaidi
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Selemani Jafo amesema jambo kubwa mwaka huu litakuwa uzinduzi rasmi wa nembo ya “Made in Tanzania,” kama mpango wa kitaifa wa kutangaza bidhaa za Tanzania katika masoko ya kimataifa