Bajaji na ujinga wa RPC Mbeya

Nsimbi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
1,091
1,202
Natumia neno zuri "ujinga" sio upumbavu. Jana mkubwa wa polisi Mbeya aliitisha mkutano na waendesha bajaji wote.
Iliamriwa kwamba waendeshaji wote wasiendelee kusafirisha abiria wakati wote wa kikao na RPC huyo.

Inaelezwa kwamba kikao hicho hakikuwa na lolote jipya zaidi ya blabla na kupotezeana muda. Sikuona sababu ya kusimamisha usafiri huo kwa kutwa nzima wakati mmiliki au mwakilishi mwingine angeweza kuhudhuria kikao hicho na kuiacha bajaji ikifanya kazi.

Ona sasa RPC kawasababishia waendesha bajaji hasara kubwa kwani vijana hao hawakufanya kazi kutwa nzima. Wakati waendesha bajaji wakikosa riziki kwa sababu ya kikao hicho, mwenzetu RPC sidhani kama anajali kwani yeye mshahara wake uko palepale!!

Sina hakika kama afande huyo anajali adha waliyoipata wakazi wa jiji la Mbeya kwa kukosa huduma hiyo.
Hakika waendesha bajaji wanapaswa kufidiwa kwa hasara hiyo iliyosababishwa na ufinyu wa busara za viongozi. Wakuu wajifunze kujali shida za vijana hawa wanaojishughulisha kwa kazi halali.

Ni wakati wa waendesha bajaji kuungana kutetea haki zenu. Epukeni viongozi ndumilakuwili. Fagieni viongozi wote wasaliti hata ikibidi "kuwaloga"!!!
 
Uliona ameongea pumba kwa sababu ulikuwa unawaza pesa ya boss na mkate wa watoto.
 
Wewe mwenyewe haujitambui mimi kama abiria wa bajaji hapa Mbeya niliona ITV habari jana nikakubali kuwa yameongelewa ya maana mfano mmekatazwa kutembea na vile vikopo vyenu vya petroli ndani ya bajaji kwa usalama wetu na mmeambiwa kuanzia january muwe na leseni ndo mtaruhusiwa kuendesha bajaji nahisi hii pia imekugusa pole kwakutaka kupotosha umma
 
Ona sasa RPC kawasababishia waendesha bajaji hasara kubwa kwani vijana hao hawakufanya kazi kutwa nzima.


Kuna mbinu nyingi za kufanya uharibifu bila mnaoharibiwa kujua kwa haraka
 
wewe mwenyewe haujitambui mimi kama abiria wa bajaji hapa mbeya niliona itv habari jana nikakubali kuwa yameongelewa ya maana mfano mmekatazwa kutembea na vile vikopo vyenu vya petroli ndani ya bajaji kwa usalama wetu na mmeambiwa kuanzia january muwe na leseni ndo mtaruhusiwa kuendesha bajaji nahisi hii pia imekugusa pole kwakutaka kupotosha umma
Alas!! Mie sio mmiliki wala mwendesha bajaji. Nilikuwa nafikiria kwa sauti tu!! Binadamu ndiye kiumbe katili kuliko wote..... Wengi wamejaa usaliti. Pole dugu bhangu
 
Amini, amini nawaambieni... RPC ALIONGEA BLABLA. ( sijasema pumba)... Nawaonea huruma tu wenye bajaji mimi siendeshi wala kumiliki bajaji. Sikushangai ndugu, watu tuna ubinafsi sana.... Hatujali shida za wengine.. Kama destiny yako ni kwenda motoni, heri ungezaliwa mbuzi....!!!!
 
Back
Top Bottom