Neno bahati mbaya hutumika mara( si zote) ili kuficha udhaifu wetu,kwa matukio yaliyo nje ya uwezo wetu neno hili hutumika kufariji basi. Matumizi sahihi ya nafasi uliyo nayo( chance,time,location,kipaji etc) kwa wakati mwafaka ni miongoni mwa vitu vinavyochangia kitu kinachoitwa bahati na kinyume chake ndio huitwa bahati mbaya. Wapo waliozaliwa ktk mazingira mazuri yaliyoruhusu matumizi sahihi ya nafasi ile kwa wakati ule. Kumbuka jambo jema/baya la leo unalofanya ndio utakaloingia nalo kesho,kwa hiyo unaweza kuvuta nuksi kwa kufanya mabaya au ukavuta bahati kwa kufanya mema,kumbuka sio lazima iwe kesho. Yawezekana mazuri ya babu yako wewe ndio unafaidi. Neno one day yes,lipo na ni kweli inategemea maandalizi ya hiyo one day yes yako unataka iwe positive au negative. Umekaa bila kuchakalika halafu unategemea one day yes ya vipi hiyo?
Kwa wanao amini neno la Mungu ni kwamba,kuna waliojaliwa na mola,yaani wao ni ku-shine tu. Na kuna wanao lipia laana ya babu/baba zao pia.
Nachangia hoja.