Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,599
- 6,669
Mkutano wa wananchi wa kabila la Wabarbaig kutoka vijiji vya Fukayosi, Kidomole, Makurunge Bagamoyo na umeisha saa 4 usiku huku wakiamua kuwa hawatazika miili hiyo hadi uchunguzi utakapofanyika na Serikali itakapotoa majibu ya kuridhisha.
Miili hiyo imetokana na mauaji yaliyofanywa na askari wa Jeshi la Polisi 28 Februari katika kile kinachodaiwa kutofautiana kwa askari hao na wafugaji waliotaka kuhesabu mifugo yao kabla Polisi hawajaichukua kwenda kuifungia kwao kwa kosa ambalo halikutajwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika hadi usiku.
Waliouawa ni Zainga Ghambalele na Rumay Ghambalele, watoto wa familia moja.
KILICHOJIRI
Kabla ya maamuzi hayo kulitanguliwa na mkutano wa hadhara ulioongozwa na Injinia Evarist Ndikilo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani aliyewasili Kidomole relini saa 8:07 huku akikaa pembeni kuita wazee ili aongee nao kabla ya kuongea na kundi la wachache akiwaomba wakawaeleze kundi kubwa wakubali kuzika miili hiyo ili taratibu zingine ziweze kufuata..
Hadi Mkuu wa Mkoa anaondoka eneo hilo na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa hakuongea na wananchi wote isipokuwa kikundi kidogo pembeni.
Kabla ya kikao hicho Ndikilo alimwita Afisa Mtendaji wa Kata kueleza anachojua, ambapo alisema yeye anafahamu wananchi wafugaji waliuawa na askari kwa kupigwa risasi.
Amtupia IGP lawama za kutotekeleza maamuzi ya Tume aliyounda
Katika kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake kutochukua hatua dhidi ya askari aliyesababiaha mauaji miezi kadhaa iliyopita na wale waliosafirisha ng'ombe bila idhini ya wafugaji ambao walifia baharini Ndikilo alisema wa kulaumiwa ni Mkuu wa jeshi la polisi Ernest Mangu.
"Mapendekezo ya tume yaliletwa kwangu na tume niliunda mimi ila nimeyapeleka kwa IGP ndo achukue hatua " alisema Ndikilo.
Licha ya kushindwa kujibu kwanini aliunda tume ambayo hawezi kutekeleza mapendekezo yake, Ndikilo aliweka wazi kuwa kwa sasa askari-polisi watatu wanashikiliwa kutokana na mauaji ya wafugaji ya February 28.
Ndikilo alikataa kuwataja askari-polisi wanaotuhumiwa akisisitiza kuwa si vema kutaja watuhumiwa hadharani kabla hawajathibitishwa popote ni kuwakosea na kuwachafua kwenye jamii au kuwapa wakati mgumu ndugu zao wanaoishi nao.
Kabla ya kumaliza mkutano huo kwa upande wake Ndikilo na kuruhusu watu wajadili kukubali kuzika aliagiza kesho Halmashauri ya Bagamoyo itoe majeneza, gari ya usafiri na mchango wa chakula kwa waombolezaji.
AIBUA MTAFARUKU
Ndikilo alishindwa kuweka wazi kwanini askari-polisi aliyetuhumiwa na tume katika mauaji ya awali hajachukuliwa hatua, lakini walioua 28 Februari ndo wameshikiliwa na Jeshi hilo hali unayoonyesha kutokuwepo kwa usawa kisheria
Taarifa za uchunguzi wa miili zakanganya
Huku Ndikilo akiwaomba wananchi wakubali kuzika maiti hizo kwa kuwa taratibu za kiserikali zimekamilika ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa maiti hizo, uchunguzi unaonekana kuwa hadi saa 5 usiku maiti zilikuwa hazijafanyiwa uchunguzi.
Msemaji wa familia Alex Masha ameuambia mtandao huu kuwa uchunguzi utafanyika kesho saa 5 baada ya daktari Elisha Sanga aliyeteuliwa na wafugaji kufika hospitali ya wilaya ya Bagamoyo.
Tume ya haki za Binadamu na utawala bora wafuatilia kwa karibu
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora pia ulipiga kambi kijijini kufuatilia mkutano wa Ndikilo na wananchi ingawa hawakuongea kwa wazi licha ya msafara wa Kamishina na wajumbe wake kutambuliwa uwepo wake na Mkuu wa Mkoa. Wajumbe wa tume waliongozwa na Kamishina Rehema Ntimizi na wajumbe kadhaa alioambatana nao
Hofu yatanda kuhusu mikusanyiko
Licha ya kuahidi kuendelea kusubiri hadi waonane na Waziri wa mambo ya ndani na IGP Jumatatu wafugaji hao wameeleza kuwa wapo katika tahadhari baada ya wao kupata taarifa kuwa polisi wamejiandaa kuwatawanya kwa mabomu kwa kufanya mikusanyiko isiyo na kibali.
Hayo yamesemwa na mfugaji Kudufane alipokuwa akiwatahadharisha wafugaji kufuatia kauli ya Ndikilo kuwa wasipozika waache kukusanyika.
Ripoti yavuja
Ripoti ambayo Mkuu wa Mkoa katika mkutano huo alitumia kulaumu IGP kutochukua hatua imevuja, taarifa kamili itatolewa kesho.
Watch this space...