Bado unazungusha bahasha yenye vyeti na cv?

Bado unazungusha bahasha yenye vyeti na cv?

Street vending na uchinga ajira isiyokuwa na purukushani nyingi zaidi ya afya yako na ka mtaji kidogo....ila ina dharaulika sana bongo...ingawa kwa serikali ya sasa hivi machinga wamepeta sana..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BADO UNAZUNGUSHA BAHASHA YENYE VYETI NA CV?

Pengine ni vigumu sana kutenganisha suala hili na siasa, lakini si nia yangu hapa kuzungumzia siasa! Lengo ni kukuamsha wewe uliye ndotoni kwamba siku moja utapata ajira!

Hebu kazia macho/hisia katika haya:

1. 70% ya watanzania milioni 55 ni vijana wa chini ya miaka 25
2. Wahitimu wa shule/vyuo ni kati ya 800,000 hadi 1,000,000 kwa mwaka!
3. Idadi ya wastaafu katika mfuko wa PSPF pekee mwaka 2017 walikuwa ni 9,552 (nisaidie kutafuta katika mifuko mingine)
4. Jumla ya watumishi hewa walioondolewa serikalini 2016/17 ni 17,201 (kwa mujibu wa gazeti la HabariLeo)


BADO UNALO TUMAINI LA KUPATA AJIRA?

Mnamo Dec 17, Sekretarieti ya Ajira imebainisha kwamba watanzania 587,746 sawa na asilimia 98.89 walioomba ajira serikalini tangu mwaka 2015 wamekosa ajira hizo. Ni watanzania 6,099 peke yake ambao wamefanikiwa kupata ajira serikalini!


Nisaidie kukokotoa ni asilimia ngapi ya uwezekano wa kupata ajira kwa takwimu hizo... Je, unajiona kuwa miongoni mwa wa asilimia hiyo 1%?

NI LINI UTAKUBALIANA NA UHALISIA KWAMBA DUNIA IMEBADILIKA?

RAI YANGU...

Kwa yule mwenye AJIRA... na aishikirie vema maana huko nje kuna mamilioni ya watu wanaitolea macho!
Kwako wewe ambaye hujapata... FUTA KABISA mawazo hayo akilini mwako na badala yake anza kufikiria ni kwa namna unaweza kutengeneza ajira kwa watu wengine!
Mwanafunzi uliyeko chuoni... kama ulichagua kozi kwa kigezo cha ajira basi ujue kwamba upo hapo kwa ajili ya kukua, kujenga network, kujifunza jinsi ya kuishi na watu, n.k. dhana ya kupata ajira iondoe akilini mwako. Anza kujipapasa mapema ujue qualities zako ni zipi!
Kwa mzazi... mwacheni kijana wako afanye kile anachodhani ni sahihi kwake! Hata kama yuko shule bado, kama anahitaji kuanza biashara yake... m-support. Ile lugha ya subiri umalize chuo kwanza, hachana nayo kabisa. Kumbuka hii ni karne nyingine kabisa.


DEAL KWA WAJASIRIAMALI!
Kwa wale ambao wameshabahatika kujenga systems na kupata customer base, basi huu ni wakati mzuri wa kupata cheap labor na hivyo kujilimbikizia faida kubwa.


SULUHISHO!!??
Matumizi MAZURI ya technolojia! Kwa imani yangu... teknolojia ndo zao pekee linaloweza kupunguza ombwe hili la ajira kwa takribani zaidi ya asilimia 70% endapo utaamua kuwa SERIOUS! Uzuri kuhusu Tech ni kwamba ina uwezo wa kutengeneza ajira nyingi sana lakini pia huo ndo ubaya wake #1... Inaondosha AJIRA katika speed ya mwanga.

Swala la msingi hapa ni kwamba ni unaitumiaje! Hapo ndo SIRI ilikojificha...

Swali ni Je, unawezaje ku-unlock hiyo SIRI?
Tafakari..
The question is how we can draw the dream into reality..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu wanafundisha jinsi ya kuanza kufanya biashara bila mtaji wowote ule . Vijana muwe makini sana na hizi fursa mnazoitiwa ,

Fursa ni kitu kilicho jificha inahitaji jicho la tatu kuweza kuivumbua na kuitumia kujipatia kipato .

Vijana fikirieni kujiajiri haswa ,,


Asante Mkuu kwa hii thread muruwa
Hapo kwenye bold ... kwani mtaji ni nini? Wanakosea kusema .. kitendo cha kijana kuwa na nguvu na maarifa - tayari huo ni mtaji.
 
BADO UNAZUNGUSHA BAHASHA YENYE VYETI NA CV?

Pengine ni vigumu sana kutenganisha suala hili na siasa, lakini si nia yangu hapa kuzungumzia siasa! Lengo ni kukuamsha wewe uliye ndotoni kwamba siku moja utapata ajira!

Hebu kazia macho/hisia katika haya:

1. 70% ya watanzania milioni 55 ni vijana wa chini ya miaka 25
2. Wahitimu wa shule/vyuo ni kati ya 800,000 hadi 1,000,000 kwa mwaka!
3. Idadi ya wastaafu katika mfuko wa PSPF pekee mwaka 2017 walikuwa ni 9,552 (nisaidie kutafuta katika mifuko mingine)
4. Jumla ya watumishi hewa walioondolewa serikalini 2016/17 ni 17,201 (kwa mujibu wa gazeti la HabariLeo)


BADO UNALO TUMAINI LA KUPATA AJIRA?

Mnamo Dec 17, Sekretarieti ya Ajira imebainisha kwamba watanzania 587,746 sawa na asilimia 98.89 walioomba ajira serikalini tangu mwaka 2015 wamekosa ajira hizo. Ni watanzania 6,099 peke yake ambao wamefanikiwa kupata ajira serikalini!


Nisaidie kukokotoa ni asilimia ngapi ya uwezekano wa kupata ajira kwa takwimu hizo... Je, unajiona kuwa miongoni mwa wa asilimia hiyo 1%?

NI LINI UTAKUBALIANA NA UHALISIA KWAMBA DUNIA IMEBADILIKA?

RAI YANGU...

Kwa yule mwenye AJIRA... na aishikirie vema maana huko nje kuna mamilioni ya watu wanaitolea macho!
Kwako wewe ambaye hujapata... FUTA KABISA mawazo hayo akilini mwako na badala yake anza kufikiria ni kwa namna unaweza kutengeneza ajira kwa watu wengine!
Mwanafunzi uliyeko chuoni... kama ulichagua kozi kwa kigezo cha ajira basi ujue kwamba upo hapo kwa ajili ya kukua, kujenga network, kujifunza jinsi ya kuishi na watu, n.k. dhana ya kupata ajira iondoe akilini mwako. Anza kujipapasa mapema ujue qualities zako ni zipi!
Kwa mzazi... mwacheni kijana wako afanye kile anachodhani ni sahihi kwake! Hata kama yuko shule bado, kama anahitaji kuanza biashara yake... m-support. Ile lugha ya subiri umalize chuo kwanza, hachana nayo kabisa. Kumbuka hii ni karne nyingine kabisa.


DEAL KWA WAJASIRIAMALI!
Kwa wale ambao wameshabahatika kujenga systems na kupata customer base, basi huu ni wakati mzuri wa kupata cheap labor na hivyo kujilimbikizia faida kubwa.


SULUHISHO!!??
Matumizi MAZURI ya technolojia! Kwa imani yangu... teknolojia ndo zao pekee linaloweza kupunguza ombwe hili la ajira kwa takribani zaidi ya asilimia 70% endapo utaamua kuwa SERIOUS! Uzuri kuhusu Tech ni kwamba ina uwezo wa kutengeneza ajira nyingi sana lakini pia huo ndo ubaya wake #1... Inaondosha AJIRA katika speed ya mwanga.

Swala la msingi hapa ni kwamba ni unaitumiaje! Hapo ndo SIRI ilikojificha...

Swali ni Je, unawezaje ku-unlock hiyo SIRI?
Tafakari..
Umekula like yangu mkuu vzr sana tena sanaaaa

Agiza balimi hapo ulipo ila utalipa mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi zipo,ajira ndio tatizo..
Lazima tukae tukifahamu ya kuwa hakuna siku itakayotokea serikali/taasisi yoyote Ile
ikaajiri wahitimu wote wa nchi,.never ever,..ukijua hili basi huwezi kuvuja jasho na bahasha yako ukapiga hodi kila ofisi kuomba uajiriwe,maarifa tuliyoyapata hebu tuombe hata kwa Mungu atupe hekima ya kutambua nini tufanye kujikwamua kiuchumi na kifikra vilevile,.huu ukungu unaotawala fikra zetu kuwa huwezi kutusua bila kuajiriwa ututoke kabisaa,.tujaribu kufikiri nje ya box,."ndani ya box tuliachie box lenyewe"
 
Wanafel kujua kua kazi ya serikali c kutoa ajira n kutoa elimu ya kukumsadia baada ya kutimu
Acheni kuishi maisha yakuigiza na kufikirika, hivi kwa kua mnakazi ndomana mnasema hayaa? Kijana kamaliza BVM SUA Hana mtaji ataanzaje kujiajili? Vifaa Hana, dawa Hana, kijana kamaliza civil engineering ataanzaje kujiajili ? Hivi ni rahisi kiasi hicho?

Daima toa bila kukumbuka na Pokea bila kusahau
 
Mimi nilishaacha na namshukuru Mungu kwa kunipa ujasiri wa kuachana na fikra za kuajiriwa.
Sijaweza kujiajiri ila nina matumaini na malengo kuwa na mimi nitajiajiri.
Mungu anisimamie na kuzidi kuniongoza katika hili nami nakaza buti nifike malengo.
Najua kitakuwa kidogo lakini changu na hicho hicho kidogo kitazaa kikubwa.
Maisha ya kuzunguka na bahasha na bado unakosa ajira yana stress sana.
Unazunguka mpaka ukikaa ukaamua kupiga hesabu nauli uliyotumia na muda unaopoteza kichwa kinauma.
Uliye na ajira ishikilie mtaani kugumu kwakweli.
Ambaye hujajaaliwa pambana kotekote usitegemee tu kwenye kuajiriwa.
Mimi najuta muda niliopoteza kutafuta ajira huku siangalii upande mwingine.
Ningelikuwa naangalia pande zote leo ungekuta nishajiajiri.
Tafuta kazi huku una kitu kingine kinakuingizia hata kama ni kidogo ili upande mmoja ukikwama mwingine unakuokoa


Sent using Jamii Forums mobile app
 
"DEAL KWA WAJASIRIAMALI!
Kwa wale ambao wameshabahatika kujenga systems na kupata customer base, basi huu ni wakati mzuri wa kupata cheap labor na hivyo kujilimbikizia faida kubwa"



Tukifikiria hivi wote tutakua maskini kwani cheap labour purchasing power yao pia ni cheap hivyo hata hivyo wanavyoproduce kutokea kwako utamuuzia nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua nimecheka sana! Rangi nyeupe unaongeza nyeusi juu yake!!!?
Naam, hebu jiulize utapata rangi gani? Andika lako ni zuri ingawa changamoto za ajira ni nyingi...
Tulipomaliza chuo 2015 wengi tulikua na mawazo ya kupata ajira govt, wengine tukabahatika kupata private company,
Kuna rafiki zangu wawili walifungua kampuni zao za Geotechnical, kwa sasa wapo mbali kimaisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ajira zipo ila zinakuja bila interview baada ya kuonesha uwezo wako

binafsi nina workshop ya kutengeneza custom tshirt..

mwaka jana tu kampuni 3 kubwa za printing zimenitafuta zinipe ajira.. nikaongoze team ya tshirts printing kwao.. ambazo nilikataa baada ya kuona mishahara midogo kuliko kazi nayoenda kuifanya. mimi nilikuwa naprint tu za wateja wadogo wadogo nazipiga picha napost insta.. kumbe kuna mabosi wanaona kazi zangu huko

page yangu insta ni hii

your mind tshirt (@tshirt_garage_mabibo_hostel) • Instagram photos and videos

kuna moja delfina mpaka leo inanihitaji... sema dau hawajafika nalohitaji..

bosi mhindi amekuja mpaka kwangu alijifanya mteja.. aone ubora wangu... akapagawa sana...

sijawai kuandika barua wala kuwaomba kazi . mi tshirt nafanya for fun tu wekend na jioni nipate hela ya mboga na mafuta ya gari.. maana nina ajira nyingine ya taaluma niliyosomea chuo kikuu

na kote huko mishahara ni zaidi ya 1m ila kazi unayoenda kuifanya ni kubwa sana.

ningekuwa sina mchongo ningeenda...

sio kama najisifia nilitaka waonesha vijana ajira zipo na zinakufuata bila interview ukionesha uwezo wako au ujuzi wako vizuri
Mkuu naomba niku PM kitu fulani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilishaacha na namshukuru Mungu kwa kunipa ujasiri wa kuachana na fikra za kuajiriwa.
Sijaweza kujiajiri ila nina matumaini na malengo kuwa na mimi nitajiajiri.
Mungu anisimamie na kuzidi kuniongoza katika hili nami nakaza buti nifike malengo.
Najua kitakuwa kidogo lakini changu na hicho hicho kidogo kitazaa kikubwa.
Maisha ya kuzunguka na bahasha na bado unakosa ajira yana stress sana.
Unazunguka mpaka ukikaa ukaamua kupiga hesabu nauli uliyotumia na muda unaopoteza kichwa kinauma.
Uliye na ajira ishikilie mtaani kugumu kwakweli.
Ambaye hujajaaliwa pambana kotekote usitegemee tu kwenye kuajiriwa.
Mimi najuta muda niliopoteza kutafuta ajira huku siangalii upande mwingine.
Ningelikuwa naangalia pande zote leo ungekuta nishajiajiri.
Tafuta kazi huku una kitu kingine kinakuingizia hata kama ni kidogo ili upande mmoja ukikwama mwingine unakuokoa


Sent using Jamii Forums mobile app
Umesomeka ... sisi zamani hatukusubiri kumaliza vyuo ndo tuanze kujichanganya kwenye kutafuta pesa - tulianza mapema. Mfano kama natoka Kanda ya Ziwa kila rikizo lazima niondoke na vitu vya kuwauzia wa Dar; kwa namna hiyo mtu unamaliza chuo tayari umeishakuwa na mtandao wa kuingiza fedha. Msingi wa utafutaji unatakiwa kujengwa mapema sana.
 
Back
Top Bottom