Bado unazungusha bahasha yenye vyeti na cv?

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,618
BADO UNAZUNGUSHA BAHASHA YENYE VYETI NA CV?

Pengine ni vigumu sana kutenganisha suala hili na siasa, lakini si nia yangu hapa kuzungumzia siasa! Lengo ni kukuamsha wewe uliye ndotoni kwamba siku moja utapata ajira!

Hebu kazia macho/hisia katika haya:

1. 70% ya watanzania milioni 55 ni vijana wa chini ya miaka 25
2. Wahitimu wa shule/vyuo ni kati ya 800,000 hadi 1,000,000 kwa mwaka!
3. Idadi ya wastaafu katika mfuko wa PSPF pekee mwaka 2017 walikuwa ni 9,552 (nisaidie kutafuta katika mifuko mingine)
4. Jumla ya watumishi hewa walioondolewa serikalini 2016/17 ni 17,201 (kwa mujibu wa gazeti la HabariLeo)

BADO UNALO TUMAINI LA KUPATA AJIRA?

Mnamo Dec 17, Sekretarieti ya Ajira imebainisha kwamba watanzania 587,746 sawa na asilimia 98.89 walioomba ajira serikalini tangu mwaka 2015 wamekosa ajira hizo. Ni watanzania 6,099 peke yake ambao wamefanikiwa kupata ajira serikalini!

Nisaidie kukokotoa ni asilimia ngapi ya uwezekano wa kupata ajira kwa takwimu hizo... Je, unajiona kuwa miongoni mwa wa asilimia hiyo 1%?

NI LINI UTAKUBALIANA NA UHALISIA KWAMBA DUNIA IMEBADILIKA?

RAI YANGU...

Kwa yule mwenye AJIRA... na aishikirie vema maana huko nje kuna mamilioni ya watu wanaitolea macho!
Kwako wewe ambaye hujapata... FUTA KABISA mawazo hayo akilini mwako na badala yake anza kufikiria ni kwa namna unaweza kutengeneza ajira kwa watu wengine!
Mwanafunzi uliyeko chuoni... kama ulichagua kozi kwa kigezo cha ajira basi ujue kwamba upo hapo kwa ajili ya kukua, kujenga network, kujifunza jinsi ya kuishi na watu, n.k. dhana ya kupata ajira iondoe akilini mwako. Anza kujipapasa mapema ujue qualities zako ni zipi!
Kwa mzazi... mwacheni kijana wako afanye kile anachodhani ni sahihi kwake! Hata kama yuko shule bado, kama anahitaji kuanza biashara yake... m-support. Ile lugha ya subiri umalize chuo kwanza, hachana nayo kabisa. Kumbuka hii ni karne nyingine kabisa.

DEAL KWA WAJASIRIAMALI!
Kwa wale ambao wameshabahatika kujenga systems na kupata customer base, basi huu ni wakati mzuri wa kupata cheap labor na hivyo kujilimbikizia faida kubwa.

SULUHISHO!!??
Matumizi MAZURI ya technolojia! Kwa imani yangu... teknolojia ndo zao pekee linaloweza kupunguza ombwe hili la ajira kwa takribani zaidi ya asilimia 70% endapo utaamua kuwa SERIOUS! Uzuri kuhusu Tech ni kwamba ina uwezo wa kutengeneza ajira nyingi sana lakini pia huo ndo ubaya wake #1... Inaondosha AJIRA katika speed ya mwanga.

Swala la msingi hapa ni kwamba ni unaitumiaje! Hapo ndo SIRI ilikojificha...

Swali ni Je, unawezaje ku-unlock hiyo SIRI?
Tafakari..
 
ajira zipo ila zinakuja bila interview baada ya kuonesha uwezo wako

binafsi nina workshop ya kutengeneza custom tshirt..

mwaka jana tu kampuni 3 kubwa za printing zimenitafuta zinipe ajira.. nikaongoze team ya tshirts printing kwao.. ambazo nilikataa baada ya kuona mishahara midogo kuliko kazi nayoenda kuifanya. mimi nilikuwa naprint tu za wateja wadogo wadogo nazipiga picha napost insta.. kumbe kuna mabosi wanaona kazi zangu huko

page yangu insta ni hii

your mind tshirt (@tshirt_garage_mabibo_hostel) • Instagram photos and videos

kuna moja delfina mpaka leo inanihitaji... sema dau hawajafika nalohitaji..

bosi mhindi amekuja mpaka kwangu alijifanya mteja.. aone ubora wangu... akapagawa sana...

sijawai kuandika barua wala kuwaomba kazi . mi tshirt nafanya for fun tu wekend na jioni nipate hela ya mboga na mafuta ya gari.. maana nina ajira nyingine ya taaluma niliyosomea chuo kikuu

na kote huko mishahara ni zaidi ya 1m ila kazi unayoenda kuifanya ni kubwa sana.

ningekuwa sina mchongo ningeenda...

sio kama najisifia nilitaka waonesha vijana ajira zipo na zinakufuata bila interview ukionesha uwezo wako au ujuzi wako vizuri
 
Ni kweli ndugu...wengi wa vijana wanadhan kuwa ipo siku serikali itatoa ajira kwa wahitim woote...wasahau....maana kila siku miradi mipya itagunduliwa na hakuna suala la ajira kwa wote litaongelewa.

Ule mda wa kutumia akili za kimaisha ndo huu..vyeti na cv tuweke pemben....

Umiza kichwa kubuni kitu cha kkuingizia pesa

Kama huna mtaji ongea na ndugu..jamaa na marafiki...ikiwezkana hata taasisi za mikopo

Weka pemben kidogo mapenzi(wengi tunafeli kwa sababu ya mahusiano hasa yasiyo na masilah kweny maisha yetu)

Piga kazi....ongeza bidii plus juhudi na lugha nzuri

Tutafika tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ona hii ...
Maarifa wanayo tayari ...
Rasirimali zipo za kutosha ...
Hekima ndo inakosekana (Hekima ni uwezo wa kutumia maarifa uliyo nayo kupata kile unachokihitaji). Eti mtu kwa kuwa ana digrii hawezi kufundisha chekechea, siwezi kulima, siwezi kufuga ... endelea kutoweza
 
BADO UNAZUNGUSHA BAHASHA YENYE VYETI NA CV?

Pengine ni vigumu sana kutenganisha suala hili na siasa, lakini si nia yangu hapa kuzungumzia siasa! Lengo ni kukuamsha wewe uliye ndotoni kwamba siku moja utapata ajira!

Hebu kazia macho/hisia katika haya:

1. 70% ya watanzania milioni 55 ni vijana wa chini ya miaka 25
2. Wahitimu wa shule/vyuo ni kati ya 800,000 hadi 1,000,000 kwa mwaka!
3. Idadi ya wastaafu katika mfuko wa PSPF pekee mwaka 2017 walikuwa ni 9,552 (nisaidie kutafuta katika mifuko mingine)
4. Jumla ya watumishi hewa walioondolewa serikalini 2016/17 ni 17,201 (kwa mujibu wa gazeti la HabariLeo)

BADO UNALO TUMAINI LA KUPATA AJIRA?

Mnamo Dec 17, Sekretarieti ya Ajira imebainisha kwamba watanzania 587,746 sawa na asilimia 98.89 walioomba ajira serikalini tangu mwaka 2015 wamekosa ajira hizo. Ni watanzania 6,099 peke yake ambao wamefanikiwa kupata ajira serikalini!

Nisaidie kukokotoa ni asilimia ngapi ya uwezekano wa kupata ajira kwa takwimu hizo... Je, unajiona kuwa miongoni mwa wa asilimia hiyo 1%?

NI LINI UTAKUBALIANA NA UHALISIA KWAMBA DUNIA IMEBADILIKA?

RAI YANGU...

Kwa yule mwenye AJIRA... na aishikirie vema maana huko nje kuna mamilioni ya watu wanaitolea macho!
Kwako wewe ambaye hujapata... FUTA KABISA mawazo hayo akilini mwako na badala yake anza kufikiria ni kwa namna unaweza kutengeneza ajira kwa watu wengine!
Mwanafunzi uliyeko chuoni... kama ulichagua kozi kwa kigezo cha ajira basi ujue kwamba upo hapo kwa ajili ya kukua, kujenga network, kujifunza jinsi ya kuishi na watu, n.k. dhana ya kupata ajira iondoe akilini mwako. Anza kujipapasa mapema ujue qualities zako ni zipi!
Kwa mzazi... mwacheni kijana wako afanye kile anachodhani ni sahihi kwake! Hata kama yuko shule bado, kama anahitaji kuanza biashara yake... m-support. Ile lugha ya subiri umalize chuo kwanza, hachana nayo kabisa. Kumbuka hii ni karne nyingine kabisa.

DEAL KWA WAJASIRIAMALI!
Kwa wale ambao wameshabahatika kujenga systems na kupata customer base, basi huu ni wakati mzuri wa kupata cheap labor na hivyo kujilimbikizia faida kubwa.

SULUHISHO!!??
Matumizi MAZURI ya technolojia! Kwa imani yangu... teknolojia ndo zao pekee linaloweza kupunguza ombwe hili la ajira kwa takribani zaidi ya asilimia 70% endapo utaamua kuwa SERIOUS! Uzuri kuhusu Tech ni kwamba ina uwezo wa kutengeneza ajira nyingi sana lakini pia huo ndo ubaya wake #1... Inaondosha AJIRA katika speed ya mwanga.

Swala la msingi hapa ni kwamba ni unaitumiaje! Hapo ndo SIRI ilikojificha...

Swali ni Je, unawezaje ku-unlock hiyo SIRI?
Tafakari..
Facts zako zimebeba maumivu makali ambayo baadhi yetu tusingependa kusikia au kuona lakini ndo ukweli,enzi za kusoma huku priority ikiwa ni kuajiriwa imepitwa na wakati

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka interview moja ya Jackma founder wa alibaba aliwahi kusema haya. Kuwa itafika hatua watu hasa vijana inabidi wafikiri nje ya ajira na hii inatokana na kasi ya kukuwa kwa teknolijia, tupo kwenye information age na sio industry age tena elimu ni muhimu yes lakini inabidi vijana tuwaze zaidi ya elimu ili tuweze kumudu kasi teknolijia inavyokuwa.Tatizo la elimu yetu haitufundishi namna ya kutumia mind zetu vizuri.Vijana tumebaki kama walalamikaji na watazamaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ajira zipo ila zinakuja bila interview baada ya kuonesha uwezo wako

binafsi nina workshop ya kutengeneza custom tshirt..

mwaka jana tu kampuni 3 kubwa za printing zimenitafuta zinipe ajira.. nikaongoze team ya tshirts printing kwao.. ambazo nilikataa baada ya kuona mishahara midogo kuliko kazi nayoenda kuifanya. mimi nilikuwa naprint tu za wateja wadogo wadogo nazipiga picha napost insta.. kumbe kuna mabosi wanaona kazi zangu huko

page yangu insta ni hii

your mind tshirt (@tshirt_garage_mabibo_hostel) • Instagram photos and videos

kuna moja delfina mpaka leo inanihitaji... sema dau hawajafika nalohitaji..

bosi mhindi amekuja mpaka kwangu alijifanya mteja.. aone ubora wangu... akapagawa sana...

sijawai kuandika barua wala kuwaomba kazi . mi tshirt nafanya for fun tu wekend na jioni nipate hela ya mboga na mafuta ya gari.. maana nina ajira nyingine ya taaluma niliyosomea chuo kikuu

na kote huko mishahara ni zaidi ya 1m ila kazi unayoenda kuifanya ni kubwa sana.

ningekuwa sina mchongo ningeenda...

sio kama najisifia nilitaka waonesha vijana ajira zipo na zinakufuata bila interview ukionesha uwezo wako au ujuzi wako vizuri
Niliwahi kuandika siku moja ... wenye kazi ndo wanafanya kazi zingine za ziada; wasio na kazi hata za ziada hawafanyi.
 
BADO UNAZUNGUSHA BAHASHA YENYE VYETI NA CV?

Pengine ni vigumu sana kutenganisha suala hili na siasa, lakini si nia yangu hapa kuzungumzia siasa! Lengo ni kukuamsha wewe uliye ndotoni kwamba siku moja utapata ajira!

Hebu kazia macho/hisia katika haya:

1. 70% ya watanzania milioni 55 ni vijana wa chini ya miaka 25
2. Wahitimu wa shule/vyuo ni kati ya 800,000 hadi 1,000,000 kwa mwaka!
3. Idadi ya wastaafu katika mfuko wa PSPF pekee mwaka 2017 walikuwa ni 9,552 (nisaidie kutafuta katika mifuko mingine)
4. Jumla ya watumishi hewa walioondolewa serikalini 2016/17 ni 17,201 (kwa mujibu wa gazeti la HabariLeo)

BADO UNALO TUMAINI LA KUPATA AJIRA?

Mnamo Dec 17, Sekretarieti ya Ajira imebainisha kwamba watanzania 587,746 sawa na asilimia 98.89 walioomba ajira serikalini tangu mwaka 2015 wamekosa ajira hizo. Ni watanzania 6,099 peke yake ambao wamefanikiwa kupata ajira serikalini!

Nisaidie kukokotoa ni asilimia ngapi ya uwezekano wa kupata ajira kwa takwimu hizo... Je, unajiona kuwa miongoni mwa wa asilimia hiyo 1%?

NI LINI UTAKUBALIANA NA UHALISIA KWAMBA DUNIA IMEBADILIKA?

RAI YANGU...

Kwa yule mwenye AJIRA... na aishikirie vema maana huko nje kuna mamilioni ya watu wanaitolea macho!
Kwako wewe ambaye hujapata... FUTA KABISA mawazo hayo akilini mwako na badala yake anza kufikiria ni kwa namna unaweza kutengeneza ajira kwa watu wengine!
Mwanafunzi uliyeko chuoni... kama ulichagua kozi kwa kigezo cha ajira basi ujue kwamba upo hapo kwa ajili ya kukua, kujenga network, kujifunza jinsi ya kuishi na watu, n.k. dhana ya kupata ajira iondoe akilini mwako. Anza kujipapasa mapema ujue qualities zako ni zipi!
Kwa mzazi... mwacheni kijana wako afanye kile anachodhani ni sahihi kwake! Hata kama yuko shule bado, kama anahitaji kuanza biashara yake... m-support. Ile lugha ya subiri umalize chuo kwanza, hachana nayo kabisa. Kumbuka hii ni karne nyingine kabisa.

DEAL KWA WAJASIRIAMALI!
Kwa wale ambao wameshabahatika kujenga systems na kupata customer base, basi huu ni wakati mzuri wa kupata cheap labor na hivyo kujilimbikizia faida kubwa.

SULUHISHO!!??
Matumizi MAZURI ya technolojia! Kwa imani yangu... teknolojia ndo zao pekee linaloweza kupunguza ombwe hili la ajira kwa takribani zaidi ya asilimia 70% endapo utaamua kuwa SERIOUS! Uzuri kuhusu Tech ni kwamba ina uwezo wa kutengeneza ajira nyingi sana lakini pia huo ndo ubaya wake #1... Inaondosha AJIRA katika speed ya mwanga.

Swala la msingi hapa ni kwamba ni unaitumiaje! Hapo ndo SIRI ilikojificha...

Swali ni Je, unawezaje ku-unlock hiyo SIRI?
Tafakari..
Mkuu hii imetoka akilin mwako??? Kama n hivyo basi wewe ni mgodi unaotembea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu wanafundisha jinsi ya kuanza kufanya biashara bila mtaji wowote ule . Vijana muwe makini sana na hizi fursa mnazoitiwa ,

Fursa ni kitu kilicho jificha inahitaji jicho la tatu kuweza kuivumbua na kuitumia kujipatia kipato .

Vijana fikirieni kujiajiri haswa ,,

Asante Mkuu kwa hii thread muruwa
 
Back
Top Bottom