Bado tuwe na imani na TAKUKURU?

DOMA

JF-Expert Member
Mar 17, 2011
944
365
Katika uchaguzi wa uwt ccm imeonekana rushwa kutia fora, na vyombo vya habari vimejitahidi sana kuripoti huku gazeti la Nipashe la jana limelipoti vizuri na kwa undani, lakini takukuru wako kimya hv tuendelee kuwa na imani na takukuru? Kwa nini tusikose imani kama tbc tulivyokosa imani nayo? Basi kama imeshindwa kazi si bora ikafutwa, kuliko kuiendesha kwa gharama kubwa huku ikiwa haifanyi kazi.
 
Ulitaka TAKOKURU wamkamate bosi wao?, si walienda pale Dododma kuhakikisha bosi wao (S S) anashinda kwa kishundo?!
 
serikali ya ccm ikubali kwambwa ni kinara wa rushwa.Chaguzi zake za ndani zimetawaliwa na rushwa ya njenje.Takukuru ipo,inaangalia na kushuhudia uchafu huo.Kwa kukaa kimya bila hatua kali kuchukuliwa ccm inajichimbia kaburi yenyewe.
 
TUKUKURU ipo chini ya nani ?
Watanzania mnachotakiwa kupigania ni marekebisho ya mfumo, ie Katiba.
Serikali, Bunge, na Mahakama visiingiline kwa namna yoyote.
Na vyombo muhimu kama Tume ya uchaguzi, NAO, TAKUKURU, nk vijiendeshe kitaasisi.
 
JK mwenyewe amekubali kuwa rushwa ilikuwepo hajachukua hatua, sasa Hosea afanye nini wakati bosi ametoa big thumb
 
Back
Top Bottom