Bado siku chache watumishi wa umma kuanza kuugulia maumivu

MahedeMkorofi

Member
Jul 12, 2016
74
123
Wakati wa sikukuu ya wafanyakazi ya Mei Mosi Mheshimiwa Rais aliahidi kupunguza kodi ya mshahara kwa wafanyakazi wote, jambo ambalo naamini litatekelezeka sababu alilisema mwenyewe mbele ya hadhara. Kuhusu mishahara hakusema kama ataongeza.

Lakini jambo la ajabu kuna ka ujumbe kanatembea kwa kasi kuhusu scale mpya za mishahara, kiasi cha kwamba wafanyakazi waliowengi wameshaanza kuamini kwamba mshahara wa mwezi huu utakuwa mkubwa kama ilivyoonyeshwa kwenye ka ujumbe hako. Tena wanasema kabisa kwamba serikali huwa inaongeza mshahara kimya kimya.

Wapo ambao tayari wameshapanga mipango yao baada ya kuona ujumbe ule, wapo ambao wameshakopa kwa watu kwa kutarajia kuongezeka kwa mshahara.

Sasa bado siku chache tu , tuanze kushuhudia wafanyakazi wakianza kuugua pressure kwa suprise watakayokutana nayo kwenye akaunti zao.

HAKUNA NYONGEZA YA MSHAHARA, MKUU ALISHASEMA.
 
Unafikiri ukiongezwa mshahara ndo maisha yako yatakuwa mazuri ? , maisha mazuri yanaanza na wewe mwenyewe ,,,
 
Back
Top Bottom