AbuuMaryam
JF-Expert Member
- Dec 26, 2015
- 2,653
- 4,758
Ndugu zangu habari kwa mara nyingine wakuu.
Nilileta bandiko hapa kama wiki 3 zilizopita, lakini Alhamdulillah walijitokeza baadhi ya watu wachache kwenye bandiko wakaniambia niwatumie CV na cover letter, nikafanya hivyo.
Lakini kimya, kiasi kwamba imepelekea mpaka watu wenginee wakiliona bandiko atahisi tayari keshapata kazi kumbe bado kabisa.
Katika sifa kubwa niliyo nayo ni uchapakazi na ubunifu, halafu napenda sana kuuliza niweze kujua ili niepuke au nisirudie makosa.
Naomba yule ambaye nimemtumia CV alafu akakaa kimya nilikuwa naomba kwa msaada tu aniambie baadhi ya makosa labda yaliyopo kwenye CV ili niyarekebishe na kama kuna sifa imekosekana nijue niitafuteje.
Lakini naomba tu mjue bado sijapata nilichokiomba humu.
Kingine nachomshukuru Allah ni ucha Mungu alionipa ambao umezaa uaminifu, jambo ambalo ukifanikiwa kuwa nami utalishuhudia.
Mimi kwangu hata Sh. 50/- isiyo ya haki hainistahili utaikuta pale pale endapo ukiniweka kwenye biashara yoyote ya halali utakayohitaji nikusaidie kusimamia.
Napatikana Dar es salaam muda wowote ukiniita inshaa allah nitakufikia.
Uzi niliopost mwanzo ni huu:-

Hizo zilizo kwenye kichwa cha habari ni miongoni mwa Professions ambazo naweza kuzifanya kwa ufanisi mkubwa kwenye tour company, hotel au travel agency, au hata kitengo cha marketing department kwenye industry yoyote.
Nikiwa na Bachelor Degree of Commerce (Specialized in Marketing and Tourism & Hospitality Management) from University of Dar es salaam Business school.
Nipo tayari kukutumia CV endapo ungehitaji mtu kama mimi.
Nipo tayari kwa mazungumzo na kuanza kazi muda wowote kuanzia sasa.