Bado ninalia na ndoa za bluetooth!

Bado ninalia na ndoa za bluetooth!

Mtoa mada ameongea kwa jazba sana...anawananga wanandoa
 
We mtoa mada achana na ndoa za watu. We komaa na mkeo huko ndani mjambiane kila siku.

Ndoa ya kwangu, mke wa kwangu, raha ama dhiki za kwangu, we unawashwa nni?

Haya maisha kila mtu ana kipaumbele chake. Wengine pesa ndio kipaumbele kuliko hiyo ndoa.
Hakuna maisha bila pesa ila kuna maisha bila ndoa.

Ukiwa na pesa ndoa zipoooo tu jomba.

Tafuta pesa hayo mandoa weka pembeni kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo watu anafunga ndoa kabla ya kuwa stable.

Mtu una miaka miwili kwenye ajira unaoa, huna bado career stability ya kuhakikisha kuwa utakuwa kwenye ofisi hiyo miaka 5 ijayo.

Tulia kwanza settle your life ndio uoe.
 
Hata urafiki wa bluetooth nao ni changamoto kubwa mnooo
 
Mkuu....umesema ukweli mtupu.....huo ndio huwa ni ugomvi wangu kwa jamii......kwani matokeo yake ni kumsingizia shetani bure......
Hata maandiko matakatifu yanazungumza kuwa,
"Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja"

Lakini cha kushangaza watu wanaambata na ajira na siyo wenza wao.......hapo lazima kuwe na tatizo....
 
Back
Top Bottom