Bado ninalia na ndoa za bluetooth!

Bado ninalia na ndoa za bluetooth!

belionea

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2014
Posts
1,053
Reaction score
923
BADO NINALIA NA NDOA ZA BLUETOOTH!
(ZILE ZA MUME YUPO SONGEA MKE ANAISHI TANGA)
--Memo hii, Ikiisha somwa, yafanyike maombi na dua maalumu---

NAKALA KWA:-

-Maparoko wote,
-Mashehe wote
-Mapasta wote,
-Maaskofu wote,
-Mnaotarajia kuingia kwenye ndoa.

DANGER! DANGER!

Hii ni memo ngumu sana inayoweza kukuudhi maana nimejifunga MABOMU kuyasema ambayo hungependa kuyasikia ukweli.

SASA TWENDENI......

Ndugu wanandoa,
Mnaomiliki ndoa za Bluetooth,
Nawasalimu salamu za kimakinikia!

Mahusiano ya wanandoa wanaoishi sehemu tofauti kwa kigezo cha kazi au masomo ni hatari Sana kwa ustawi wa ndoa yako,ni sawa na mtu anayelima shamba Iringa yeye anaishi dar ,yeye anapiga simu tu na kutegemea kuvuna mavuno kedekede.

Mme unaishi Mwanza mke anaishi mtwara halafu mnasema mmeoana.Ninakupa tahadhari kwa nguvu ya Roho Mtakatifu aliyeko ndani yangu. Eva alikuja kurubuniwa na nyoka baada ya kuona kuwa Adamu ameondoka,nina uhakika kama Eva angekuwa na mme wake nyoka asingethubutu kumsogelea Eva na kumdanganya.

Kuna mambo mengine mkiwa mnaishi pamoja mke na mme shetani hawezi kuthubutu kuyaleta ila ile kutengana shetani anapata hapo mwanya wa kuja kuwajaribu.Nimeshuhudia ndoa nyingi ambazo zimepigwa kwa jinsi hii.Ninawaonya binti zangu BHM na wale mlio kwenye ndoa tayari kuepuka jambo hili kwa garama yoyote.Msije kusema sikuwambia.

ELOI! ELOI!

Mimi nina pointi 10 nilizokuletea ili ikiwezekana uokoe hili janga lililokuzunguka

1). Kinachosababisha kufika hali hii sio serikali kukataa kuhamisha watumishi, bali ni wafanyakazi wenyewe kukataa kuhamisha akili. Shida ya kwanza kwa wengi ni kuamini kwamba ajira ni kila kitu. Shida ya pili ni vipaumbele. Ukiona unaacha mke Dar unaenda kufanya kazi Mtwara, na mke nae akawa mwajiriwa na miongoni mwenu hakuna alietayari kuacha kazi kumfuata mwingine, mjue kwamba wote wawili hakuna ambae ameweka ndoa kama kipaumbele cha kwanza!

2). Nioneshe mtu aliewahi kuthamini ajira kuliko ndoa halafu ndoa ikabaki salama kwa muda mrefu. Mnaweza kusema ohooo, tunaaminiana, mara ohooo, mke wangu/mume wangu hawezi kunisaliti, sikatai! Enhee, akishakuwa hajakusaliti what is next? Nyie ni watu wazima bana, naomba niwaeleze kwamba kuna mambo ambayo maombi yanaweza kuhamisha, lakini kuna mambo yapo mwilini huwa hayahami kwa maombi ng'oooo. Ukiamua kubisha shauri yako mwenyewe! Wewe umekomaa na ajira yako huko Mwanza mume umemuacha Dar, halafu unategemea maombi ya kwa Nabii Malisa, eti Mungu amlinde mumeo kule Dar? Subiri uvune mabua, ndio utaelewa!

3). Halafu aliewaambia kwamba mmoja akiacha ajira kumfuata mwingine, eti mtakufa na njaa nani? Shida yenu ni kwamba tukiwaelekeza ujasiriamali mnaona as if hauwahusu, ndio maana ajira mnazitetemekea kiasi cha ku-risk ndoa zenu. Aliekudanganya kwamba ukiwaachia liajira lao wanalokulipa "vilaki nane", ukamfuata mke/mme na kupiga ujasiriamali, utakosa kuzalisha zaidi ya laki nane, ni nani huyo? Unajua ninawamaindi kwa sababu, nilishawaelezaga kwamba kwenye ajira mnalipwa asilimia chini ya kumi ya mnachozalisha, sasa kinawashinda nini kuzitoa sadaka ajira ili mkaokoe ndoa? Nakuona tu unavyonibinulia midomo, na kunifyonya, lakini huu ndio ukweli.

4). Haya basi! Tuseme ninyi ni wa kisasa, so, ishu ya ndoa ya bluetooth haiwasumbui, je, hayo malezi ya watoto inakuwaje? Mke Kigoma, mume Arusha, watoto wako boarding Tabora! What a wastage of parentalhood! Shida yenu mlio wengi mnadhani ni sifa kupeleka watoto wa chekechea boarding in the name of kutingwa ama in the name of ajira. Laiti mngekielewa ambacho Mtume Paulo alimweleza Timotheo kuhusu watoto (2Tim 3:15), msingekubali mtindo huu, ama mtindo wa baba kusubiri miezi sita ama mwaka ndio akawaone watoto kwa mkewe, maana watoto wanalelewa na mama Songea baba akiwa kazini Dodoma!

5). Hadi hapa najua nimeshawakorofisha watu, maana ndoa za masafa siku hizi imekuwa ndio fasheni, kwamba mke na mume wakikutana ni spesho kwa ajili ya ujauzito na from there huyu kule mwingine huko. Hivi aliewaeleza kwamba ndoa ni just ijulikane umeoa ama umeolewa ni nani? Kwani haijaandikwa kwamba mmeoana ili muishi pamoja?

Hata hizo hela mnazotafuta (if ni nyingi kihivo) mnawezaje kuzipangia matumizi na maendeleo ya familia? Au ndio mnategemea bando la halichachi na jazwa ujazwe na WhatsApp kujadiliana kuhusu familia? Hivi mnajua kwamba kuna nguvu kubwa kupanga mambo ya ndoa na familia mkiwa mnatazamana kwa macho na mwenzi wako? Mkoje, nyieeee? Kwani maparoko, mapasta na mashehe hawawaelezi haya?

Wakinga huwa wanasema vyungu viwili huwa vinamaliza kuni haraka. Mume uko Tanga una bajeti ya nyumba, mke yuko Geita nae ana bajeti ya nyumba, hee, kwa mishahara hii ya chini ya milioni mbili, lini mtafanya maendeleo ya maana?. Ni ujinga mkubwa wa kiwango cha utoroshaji wa makinikia, wanandoa kuishi mbalimbali na ku-risk ndoa eti kwa mishahara ambayo inaishia kwenye matumizi!

By the way, who told you kwamba hata muajiriwe ajira tatu-tatu eti ndio mtakuwa na financial freedom? Wengine wananiuliza, "Je, kwa waliopo masomoni inakuwaje?". Haaa! Haaa! Mie leo naongelea mnaofanya kazi, mengine msinipangie!

6). Mmeambiwa kwamba kisiwepo cha kuwatenganisha isipokuwa kifo. Hamuoni kwamba ajira zimeshakuwa vifo? Mnapata wapi ujasiri wa kuishi na kifo mkingali hai? Nyie mnaujasiri sana. Yaani kifo kinazunguka zunguka, mpo tu mwaka wa kwanza, mwaka wa pili, mwaka wa tatu mnakitazama tu???!!!?? Kweli? Mbona mna hatari namna hiyo!

7). Pointi hii yaweza kuwa ngumu zaidi. Unajua wanaume huwa wanasisimka kwa kuona(kutazama), right? The fact is, asipokua anakiona anachokipenda mara kwa mara (yaani mke wake) ataanza kuona mibadala, hata kama ni "mlokole masalia". Mwanamke anasisimuliwa kwa kusikia (with physical expression). Ndio maana hata mke ukimuangalia usoni na kumwambia, "Nakupenda", anasisimka zaidi kuliko ukimpigia simu na kumwambia, "Nakupenda".

Mpo? Mwanamke anaihesabu "care" kwa kupima ukaribu, (yaani muda unaokua nae physically). Wanawake ni kama watoto, sio kiakili bali kwa hitaji lao la kuwa cared to the maximum. Mwanamke yeyote unaweza kumpata kiurahisi ikiwa kuna factor mbili:- mosi, ikiwa mumewe amezembea kum-care. Pili, ikiwa muwindaji utatumia sayansi ya ku-care. (Mliooa shikeni pointi hapa mnafanya uzembe halafu nyani wanakula mahindi yenu).

So, mwanamke alieolewa anapokuwa mbali na mumewe, huwa anakuwa na gepu fulani, hata kama awe anajikaza. Kuna two things hapa:- gepu hilo likiwepo ndio anaweza kuendelea kujikaza lakini ikizidi sana atakuwa anaumia na itamuathiri. Akiwa anavumilia ashukuriwe Mola. Pili ni kwamba anaweza kutafuta mbadala.

Wanaume ukiona ametafuta mbadala automatically huwa ni kwa ajili ya ngono lakini wanawake huwa wanatamani just care, baasi. The question comes, wanaume wangapi wanaweza kuwa karibu na wake za watu kwa extend ya ku-care that much halafu wawaache pasipo kuwakula? Ndio ile unakuta mke wa mtu ameshaliwa halafu anasema, "Wewe kaka Abdul nilikuwa nakuchukulia kama kaka yangu lakini umenifanya tumefanya hivi, basi iwe siri yetu".

Usidhanie ninakutisha, lakini ukatae ubishe, ni kwamba huko aliko mumeo ama mkeo ambako kuonana ni mpaka likizo hadi likizo, uwezakano wa wewe kula makombo ni mkubwa (hope mnanielewa). Jifariji uwezavyo, muone mkeo ni mlokole uwezavyo (in fact kuwa mlokole hakufuti hisia na mahitaji ya kike), mie ninakwambia fanya juu chini muishi pamoja, maana usalama ni mdogo. Sijasema usalama haupo, hapana, ila nimesema ni mdogo.

By the way (kwa wewe unaebisha) wacha tu-assume kwamba mkeo ama mumeo ambae uko nae mbali yupo salama asilimia zote kwa hiyo naomba hata usinicharukie, sawa enhee? Maana hukawii kujenga hoja unipige mawe kuhofia kujihami na uwezekano wa mali zako kuliwa hulo ziliko. We uchune tu, simuongelei mke wako/mume wako, mie nawasemea wengine. Si umenielewa etiii?

8). Baadhi ya wanawake mlioolewa katika ndoa hizi za bluetooth mnanichekeshaga sana. Unakuta unabana kabisa pua eti, "Siwezi kuacha ajira, coz wazazi hawatanielewa maana walinisomesha", heee! Unataka kueleweka kwa wazazi ama unataka kueleweka kwa mumeo? Shida yenu (baadhi yenu), vielimu vyenu vimeshawapotezea utii na unyenyekevu kiasi kwamba mnaamua ya kwenu ndani ya ndoa as if bado mko mabachela. Mie ni mmoja ya wanaume wanaosisitiza wanawake wafanye kazi (akiwemo mke wangu), lakini niko aggressive sana linapokuja suala la mke kuthamini maslahi ya ndoa na familia kwa MAJADILIANO. Ukishabana pua yako na kuanza kuwasikiliza wazazi maana yake ni kwamba hamuwezi kufikia muafaka na mumeo kwa suala hili la ndoa ya bluetooth! OLE WAKO NIKUKUTE, maana bakora za mgongo zitakuhusu!

9). Sisemi kwamba ni lazima mmoja wenu aache kazi kumfuata mwingine, la hasha! Ila ninashauri kwamba muanze kufikiria uhamisho if upo, mkikosa kabisa alternative ya uhamisho, fikirieni mmoja anaemfuata mwingine akatafute kazi anakohamia, na hilo likishindikana ndio kufuatie KUJILIPUA, yaani kuacha ajira na kwenda kulea ndoa. Ninachofahamu ni kwamba, kama mkikomaa na Mungu na mkaziweka akili zenu kufikiri, mnaweza kuishi pamoja na kipato chenu kisiathiriwe. Ninacholilia mie ni ile watu mmekaa mbalimbali mwaka wa kwanza, mwaka wa pili, mwaka wa tatu, n.k halafu hakuna bidii za kujitoa sadaka zinazofanyika ili mkaishi pamoja. Hapa ndipo ninapomaindi zaidi!

10). Kuna kitu kwenye ndoa kinaitwa Marriage Culture (utamaduni wa ndoa) ambacho hujengwa ndani ya miaka mitatu hadi mitano baada ya kuoana. Marriage culture hutengenezeka mnapokuwa pamoja. Marriage culture ni kama msingi wa ndoa, usipojengwa siku za kwanza za ndoa you are finished maana kuna uwezekano ndoa kukosa dira. Mmetoka honeymoon, mke karudi Katavi kazini mume umeenda zako Bukoba kazini. Huu ni mwaka wa tatu, mnakutana likizo hadi likizo! Siwafichi, mnampa shetani wakati mgumu kudhani kwamba ataiacha ndoa yenu salama.

Na nyie ambao ndoa ina zaidi ya miaka mitano mkiwa pamoja then mkatawanyika mama Urusi baba, Tanzania, mna hatari kubwa maana kuna kitu kinaitwa marriage bond (muunganisho wa ndoa), kinakuwa kinasagika na ipo siku kitakatika na .mtakutana uso kwa uso na divorce hata kama mmeshaoza na kuozesha wana! Enewei siwaingilii, just nawaeleza kiaina.

HEBU TUOMBE....

Eemola wetu/mungu wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukikemea na kukomesha ndoa zote za bluetooth maana zimekuwa kiota cha michepuko na kuathirika kwa malezi ya watoto. Kabla mwaka huu haujaisha, ndoa nyingi za bluetooth zisiwepo hasa kwa huyu alienisoma na kunielewa, Ameeeen!

Baada ya maombi haya ENENDA KWA AMANI UKAJILIPUE!

MAANA....

Kuna wengine mnapolia kuhusu ndoa, kumbe inabidi tukemee tu kifo, ili mpoteze ajira mkaokoe ndoa! Naomba mtu yeyote asinimaindi kwa hii memo hata kidogo. Ingawa najua HUU NI UJUMBE MGUMU kwenu, naombeni mnivumilie na muupokee hivo hivo. Safari hii siwadai soda maana najua nimewachefua nyongo, japo ndio ukweli wenyewe! #Faida potea kijana wa mwanza NINALIA NA NDOA ZA BLUETOOTH!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu anipe summary... Siwezi soma habar inayohusu mapenzi ndefu kiasi hiki.
 
Wenye Ndoa wanatafakari,,Ila hivi vitu Ni tatizo kubwa Sana. Hata uwe bize vipi,,mwili nao unamatamanio yake.

Swali hayo matamanio unayafanya wapi kama mwenza hayupo karibu na wewe!?

Bila Shaka hata wachumba wakiwa katika zile siku huwa ni kivumbi kwa wanangu wa show show,,sasa sembuse mtu akiwa mbali!!!
Ila yooote yatokee usiletewe damu si yako ndani ya nyumba!!!!!
 
Naona umetambaa na ukali muhun

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dunia ndivyo ilivyo kwa sasa.
Usione huko Ulaya kuna Mpaka Mshoga na Wasagaji lakini wazungu wanaongoza kwa kuishi karibu mke na mume. Sasa tatizo nini?? Ni imani na Roho zao zimetoka kwa Mungu na kujiweka kwa Shetani na tamaa za miili yao kuwatawala. Amini amini amini nawaambia kama mtu anashindwa kuongoza nafsi yake kuushinda mwili hata mke angeishi na mume kama matako mawili yanavyogusana bado michepuko ingekuwepo mana wangechokana sana. Ndo nyingi zinazoyumba sio wale wanaokaa mbali Bali wale waliochokana kwa kuzoeana. Kuna watu wengi wanaishi pamoja lakini hawana mawasilano kabisa mana wamechokana. Mapenzi hua yanachuja hasa kwa maisha ya sasa mana watu wanakua na majukumu mengi lakini pia kama MTU hawezi kuilinda nafsi yake dhidi ya tamaa hata kama mke na mume wanafanya kazi ofisi moja watakorofishana kwa kuotea michepuko kwenye ofisi moja.

Wakati sheria ya kuwapiga mawe wanawake wazinzi ilipotungwa hapakua na mambo ya uhamisho wa kazi wala kukaa mbali kwa wanandoa. Shiria ilitungwa wakati huo kutokana na wanawake kuzaa nje ya ndoa na kuingiza vizazi viovu kwenye familia.

Adamu na Hawa waliishi pamoja lakini Hawa kuna mambo aliyatamani nje ya ndoa yao. Hakuna Hawa alitaka Uhuru. Nyoka alijua kuwa Hawa anapenda maisha mazuri na yenye Uhuru na awe juu ya Adam. Adamu alikua mtiifu sana kwa Mungu . Hawa akaona wivu kuwa Adamu ampenda Mungu kuliko yeye. Akaona akiwa kama Mungu basi mapenzi na utii wa Adam kwa Mungu utahamia kwake.
Akadanganyika na kuanguka.
Suala la Ndoa ni gumu sana. Karne hii ni lazima wawepo watu Committed watakaojitolea kuwatumikia wengine kwa gharama ya kuzikana nafsi zao. Ndio maana kuna wengine hawaoi wala kuolewa .Yote ni ujenzi wa dunia inayotawalika na inayoendelea mbele kiteknolojia. Wasomi sana na Watawala katika dunia ya kisasa Mara nyingi ndio waathirika wakubwa wa haya. Ndio maana wenzetu wenye Teknolojia kubwa muda mwingi wako bize sana hata ndoa zao zinayumba lakini wanaficha. Hata hizi simu zinayumbisha sana ndoa za watu siku hizi na hata malezi ya watoto. Watu wapo bize na simu masaa 24.
Ni mabadliko ya kidunia. Dunia itafikia Mwisho wa haya soon na watabaki wanye imani ya kiroho na wenye uwezo wa kuziongoza nafsi na roho zao. Wenye kuweka mbele mambo ya Mwilini watapata tabu sana mana wataumizwa na yale wasiyoweza kuyatimiza kwa maamuzi yao.

Hata watoto siku hizo wanalelewa mashuleni tangu wakiwa na miaka 3 mpaka chuo kikuu. Wakihitimu hapo wanakua wako vizuri sana kitaaluma lakini kijamii ya kiafrika wanakua hawaeleweki kabisa labda kimataifa au kizungu zaidi.

Nafaikiri wanasaikolojia na washauri kama Mleta mada wanapaswa kuiandaa jamii kisaikolojia namna ya kukabiliana na hali hii ambayo bado jamii yetu kubwa inaishi maisha ya Chini na maendeleo yapo duni kwa serikali kuweza kuweka mazingira ya familia zote kuishi pamoja.
Mfano Usafiri wa miji na miji ni mgumu. Kama kuna Treni ya Mwendo kasi na Ndege bei Rahisi hakuna umbali ya kutoka Mbeya kurudi Mwanza hata kila siku na kulala nyumbani.
Hata ndani ya miji kama Dar es salaam kuna watu wanafika nyumbani saa tano au sita kila siku na kuondoka nyumbani sa kumi alfajiri. Kama Mwanamke au Mume sio mfanyakazi ataona ni kero kubwa sana . Hapo mchepuko unaweza kuingizwa ndani SAA moja asubuhi kama hakuna uwezo wa kuiongoza nafsi na mwili. Mana mwanaume au mwanamke anayerudi kazini SAA sita usiku na kuamka SAA kumi atakua hana uwezo wa kufanya vizuri kitandani.

Mungu awaepushe na majaribu tuu lakini dunia ipo kwenye wakati mgumu sana. Na Corona tena ndio inaharibu kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesema kweli aslimia 99 ubarikiwe utafikiri umenisema mimi hata sikioni ninacho kitafuta kwa kweli
 
Jukwaa la MMU unaandika utadhani uko la Intelegence!?

Alosoma anifupishie tafadhali
 
Back
Top Bottom