Bado nampenda mpenzi wangu, naomba ushauri nifanyaje?

Bado nampenda mpenzi wangu, naomba ushauri nifanyaje?

Kama mambo ndo hayo ni bora umwoè huyo unayempenda kuliko kuoa usiyempenda wakati unajua unayempenda yupo. Utakuja kumtesa mtoto wa watu bureee sababu utaendelea kuwa na huyo. Angalia upendo upo wapi achana na mambo mengine kaka.
 
Kabisa Honey Faith bora tu aamue kivyake vyake na wafunge pingu za maisha na Mama gagulo. Ndoa ambayo haina mapenzi haina maisha marefu.Watu wanapendana kiasi hiki ila dini ndio kikwazo, wengine huwa wanabahatika dini huwa hawazipi kipaumbele kihivyo na hivyo kuendelea na penzi lao.

[video
=youtube;Mr8SUf8oTk4]https://www.youtube.com/watch?v=Mr8SUf8oTk4[/video]



Sasa baba gagulo kwanini uoe sehemu ambayo moyo haujaridhia???
 
Mapenzi ni hisia za ndani kabisa ya moyo ulizo nazo juu ya mtu fulani aliye muhimu ndani ya nafsi zetu..hisia ambazo zinatufanya tujione kama tupo peponi kwa raha mara tuwaonapo wapendwa wetu,hisia ambazo zinatufanya tuonyeshe tabasamu la raha kila tushikwapo na wapendwa wetu...hisia ambazo zinamfanya mtu aonekane kama mwendawazimu mbele ya kadamnasi mara tu amuonapo kipenzi cha moyo wake.

Ni vigumu sana kuwasahau wapendwa wetu kwani tayari wameshachukua sehemu kubwa ndani ya nyoyo zetu na kuwafanya kila siku kuishi ndani yetu popote tuwapo,jambo la busara si kukinzana na hitaji la mioyo yetu bali kuupatia kile ambacho moyo unakihitaji kama kipo tusichokijua ni kwamba kwenye ulingo wa mapenzi kila mtu anakuwa na ulimwengu wake wa hisia ambao auhusiani na mtu yoyote hata wawe wazazi wetu wapendwa kwa kuwa hisia za upendo tunazihisi sisi wenyewe na sio mtu mwingine sasa kama hisia ni zako kwanini maamuzi ya hisia zako akuamulie mtu mwingine.?

Kwa hakika ni jambo lisilopatana na akili hata kidogo kwani maumivu ya moyo unayapata wewe na sio mtu mwingine busara iliyokuu ni kukaa na wazazi wako na kuwaambia katika uso unaomaanisha kile ambacho unakinena kutoka kinywani mwako kwamba huyu ninayetaka kumuoa sio chaguo langu hata kidogo huku hekima ikitawala kuliko kuendelea kutenda dhambi ya uzinzi hali ya kuwa umeshaingia kwenye ndoa kwa kuchepuka na yule umpendae ni bora uoe yule ambaye ni chaguo la moyo wako,kwani moyo utamfurahia siku zote na utaiona ndoa kama pepo ndogo kwa raha utakazo pata.
 
Perry
Dini ina impact kubwa sana katika maisha ya wanandoa hasa ambao wameyapa maisha ya kiroho kipaumbele. Hata kama mmependana kiasi gani itafika kipindi mmezoeana saaaana na watoto mnao, hapo ndipo mtakapoanza kutembea na beat tofauti. Ila kama mambo ya kiroho siyo ishu kwako basi kigezo cha dini hakina maana yoyote hata kidogo.

Unaweza usielewe kwa sasa kwa sababu ya kujifikiria saaana binafsi ila baadae utagundua kuwa maisha ya ndoa ni pamoja na familia. Familya yako kwanza, kisha ndugu na jamii kwa ujumla. Hivyo mzazi akikuahauri juu ya hili usipuuze bali lifikirie ili ukiamua uwe umeamua juu ya kitu unachokijua na umejitoa kukikabili kwa namna yoyote. Wazazi wana haki na jukumu la kukuongoza japo si kukuamlia kama ushakuwa mtu mzima.
 
Last edited by a moderator:
Huyo mama Gagulo tayari ana ngoma ndio maana karudi kwako na anataka mfe wote,kuna wakati inafaa uelewe kuwa maisha sivyo unavyopanga bali ndivyo wengine wanavyopanga.
 
Oa wote wawili; MamaGagulo utafaidi utamu wa ki movie movie. Mchumba mtarajiwa utafaidi family status, jitahidi usije wakosa wote.

Onyo:Changanya na zako.
 
Back
Top Bottom