bado miaka minne kuufikia mwaka wa mavuno.........mwaka wa kuwa baba mie

mnyikungu

JF-Expert Member
Jul 26, 2009
1,960
2,464
kila binadamu ana malengo yake katika maisha, tumetofautiana sana katika malengo yetu, kuna wengine wanapendaga malengo ya muda mfupi mda mrefu hawataki, wengine wanapenda ya mda mfupi wanachanganya na ya mda mrefu, lakini lengo ili litimie mtu anahitaji kuwa na mbinu na mikakati...

sasa basi katika maisha ya kuwa baba mwenzenu nilijiwekea malengo ya muda mrefu huku nikijipa muda wa kujiandaa kuyafikia malengo hayo, mpaka sasa bado nachakalika ili lengo litimie na mission isifail. wakati wa wote wa ujana wangu nimejifunza mengi mazuri na mengi mabaya, lakini kwenye maisha ya mahusiano hasa ndoa nawalaumu sana wale waliokuwa wananisirikisha katika kutatua migogorao yao. kipindi chote nilichokuwa natatua hiyo migogoro kuna vitu vilikuwa vinajijenga kichwani, mwisho wa siku nikazichukia ndoa, nikajikuta tu nimejiapiza kuwa siji kuoa. wakati najiapiza nikajikuta pia napenda watoto, hapo ndo mikakati ikaanza.

nimepanga kuwa na watoto saba maishani MUNGU AKIJAALIA, najua mtanishangaa mtasema ni wengi ila hao ndo kwangu naona naweza kuwamudu kwa kila kitu watachotaka katika maisha yao, lakini hawa watoto saba sitaki wawe wa ndoa maana sitaki kuoa, pia sitaki wapishane saana. maana yake nataka wawe wote wamezaliwa ndanI ya mwaka mmoja tu(MUNGU AKIJAALIA) kwa mama tofauti.
baada ya kuwa na malengo hayo niliamua kuwekeza kwenye miti ya mbao, nikanunua mashamba nikapanda miti ambayo itakuwa baada ya miaka kumi, japo hata miaka saba yaweza kuvunwa, faida itayotokana na hii miti ndo hiyo ambayo itaweka misingi kwa wanagu, nauhakika nitaweza kuwafungulia acount bank nikawawekea akiba, nauhakika nitawalisha na kuwasomesha na kila kitu kupitia miradi hiyo. nje ya hapo pia najituma mno ili miti ikishidwa niwe na njia nyingine ya kuwalea watoto wangu.
sasa ni miaka sita tangu nianze mikakati, bado miaka miine kuufikia ule mwaka ambao nimeamua kuuita wa mavuno.... ndiyo ni wa mavuno maana ndani ya huo mwaka nitahakikisha nimewazalisha wanawake saba ambao kwa kadirio la chini watanizalia watoto saba (MUNGU AKINIJAALIA)kama kati yao asipozaa mapacha.

hawa watoto nitawalea mimi mwenyewe kwa makubaliano maalumu ya wazazi wenzangu, lakini kama wakitaka kukaa nao nitawaruhusu ila wakifikisha miaka kumi watanisamehe bure, nitachukua watoto wangu na kuwaweka pamoja kwenye nyumba yangu ili kuwaunganisha kama familia.

nikiwapata hao watoto, sitakuwa na habari za kutafuta watoto tena, nitajishughulisha kutafuta pesa tu ili kuendelea kuwalea wanagu. bila shaka watanipa furaha na faraja ya kutosha mimi baba yao. jamani ndoa nimeona zinakera, saa nyingine hata wanachogombana nilikuwa sikioni ila wanagombana tu... maisha hayo mi siyawezi, nina mambo mengi uwa sipendi kero. nina hasira sitaki kesi mimi. ndoa ni majanga jamani, nimesuluhisha ndoa nyingi mno nimegundua ndani ya ndoa hakuna amani. kuna jamaa mmoja ilikuwa inamlazimu achelewe kurudi kila siku na awahi kuondoka kila siku.. kisa mkewe mgomvi balaa. kuna mzee mmoja alijikuta kaanza tu kuwa mlevi kisa ndoa chungu kwahiyo akaamua apoteze mawazo kwa mtindo huo. nimeshuhudia watu wanajinyonga na kunywa sumu, nimeshuhudia watu wanajipiga risasi. YOTE HAYO MI SITAKI YANIFIKE KWA KWELI

KAMA MKAKATI WANGU HUU NI MAKOSA BASI MUNGU ANISAMEHE BURE ILA NDO NIMEAMUA NA SITORUDI NYUMA. NAMUONEA HURUMA MAMA ANGU AMBAYE KILA KUKICHA ANANIBEMBELEZA NA KUNILALAMIKIA KUWA ANATAKA MKWE.
 
Mmmmmh!!!!!!!!! mwaka wa mavuno utanitafuta nikupe mapacha,,,,,,,,,,,,
Sipendi kulea so after two month utachukua watoto wako.

ha ha ha haa, nitakutafuta usijali, nitalea mwenyewe usipate tabu, we nizalie mengine nitamalizia....
 
Hamna hata sehemu ambapo nimesema nimepanga kutomheshimu mungu, kwanza nitakuwa natekeleza lile agizo lake la "enendeni duniani kote mkaijaze nchi"
 
kumbuka kuna HIV mkuu,omba Mungu sana akubadilishe mawazo hayo ujitafutie Mwanamke mmoja tu alie salama na mtakae Heshimiana
 
kila binadamu ana malengo yake katika maisha, tumetofautiana sana katika malengo yetu, kuna wengine wanapendaga malengo ya muda mfupi mda mrefu hawataki, wengine wanapenda ya mda mfupi wanachanganya na ya mda mrefu, lakini lengo ili litimie mtu anahitaji kuwa na mbinu na mikakati...

sasa basi katika maisha ya kuwa baba mwenzenu nilijiwekea malengo ya muda mrefu huku nikijipa muda wa kujiandaa kuyafikia malengo hayo, mpaka sasa bado nachakalika ili lengo litimie na mission isifail. wakati wa wote wa ujana wangu nimejifunza mengi mazuri na mengi mabaya, lakini kwenye maisha ya mahusiano hasa ndoa nawalaumu sana wale waliokuwa wananisirikisha katika kutatua migogorao yao. kipindi chote nilichokuwa natatua hiyo migogoro kuna vitu vilikuwa vinajijenga kichwani, mwisho wa siku nikazichukia ndoa, nikajikuta tu nimejiapiza kuwa siji kuoa. wakati najiapiza nikajikuta pia napenda watoto, hapo ndo mikakati ikaanza.

nimepanga kuwa na watoto saba maishani MUNGU AKIJAALIA, najua mtanishangaa mtasema ni wengi ila hao ndo kwangu naona naweza kuwamudu kwa kila kitu watachotaka katika maisha yao, lakini hawa watoto saba sitaki wawe wa ndoa maana sitaki kuoa, pia sitaki wapishane saana. maana yake nataka wawe wote wamezaliwa ndanI ya mwaka mmoja tu(MUNGU AKIJAALIA) kwa mama tofauti.
baada ya kuwa na malengo hayo niliamua kuwekeza kwenye miti ya mbao, nikanunua mashamba nikapanda miti ambayo itakuwa baada ya miaka kumi, japo hata miaka saba yaweza kuvunwa, faida itayotokana na hii miti ndo hiyo ambayo itaweka misingi kwa wanagu, nauhakika nitaweza kuwafungulia acount bank nikawawekea akiba, nauhakika nitawalisha na kuwasomesha na kila kitu kupitia miradi hiyo. nje ya hapo pia najituma mno ili miti ikishidwa niwe na njia nyingine ya kuwalea watoto wangu.
sasa ni miaka sita tangu nianze mikakati, bado miaka miine kuufikia ule mwaka ambao nimeamua kuuita wa mavuno.... ndiyo ni wa mavuno maana ndani ya huo mwaka nitahakikisha nimewazalisha wanawake saba ambao kwa kadirio la chini watanizalia watoto saba (MUNGU AKINIJAALIA)kama kati yao asipozaa mapacha.

hawa watoto nitawalea mimi mwenyewe kwa makubaliano maalumu ya wazazi wenzangu, lakini kama wakitaka kukaa nao nitawaruhusu ila wakifikisha miaka kumi watanisamehe bure, nitachukua watoto wangu na kuwaweka pamoja kwenye nyumba yangu ili kuwaunganisha kama familia.

nikiwapata hao watoto, sitakuwa na habari za kutafuta watoto tena, nitajishughulisha kutafuta pesa tu ili kuendelea kuwalea wanagu. bila shaka watanipa furaha na faraja ya kutosha mimi baba yao. jamani ndoa nimeona zinakera, saa nyingine hata wanachogombana nilikuwa sikioni ila wanagombana tu... maisha hayo mi siyawezi, nina mambo mengi uwa sipendi kero. nina hasira sitaki kesi mimi. ndoa ni majanga jamani, nimesuluhisha ndoa nyingi mno nimegundua ndani ya ndoa hakuna amani. kuna jamaa mmoja ilikuwa inamlazimu achelewe kurudi kila siku na awahi kuondoka kila siku.. kisa mkewe mgomvi balaa. kuna mzee mmoja alijikuta kaanza tu kuwa mlevi kisa ndoa chungu kwahiyo akaamua apoteze mawazo kwa mtindo huo. nimeshuhudia watu wanajinyonga na kunywa sumu, nimeshuhudia watu wanajipiga risasi. YOTE HAYO MI SITAKI YANIFIKE KWA KWELI

KAMA MKAKATI WANGU HUU NI MAKOSA BASI MUNGU ANISAMEHE BURE ILA NDO NIMEAMUA NA SITORUDI NYUMA. NAMUONEA HURUMA MAMA ANGU AMBAYE KILA KUKICHA ANANIBEMBELEZA NA KUNILALAMIKIA KUWA ANATAKA MKWE.

Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
kumbuka kuna HIV mkuu,omba Mungu sana akubadilishe mawazo hayo ujitafutie Mwanamke mmoja tu alie salama na mtakae Heshimiana

hata ukiwa na mmoja unaweza pata pia, ukiingia tu kwenye uhusiano wewe HIV risk taker.... cha msingi kuomba mungu tu atuepushie na hii dhahama
 
Ni mtizamo mzuri lakini hatar sana wenye risk za kila aina,madhara ni mengi kuliko faida,anyway hatuombei hayo yatokee kikubwa unatengeneza familia ambayo cjui itakuwaje kumbuka ww peke yako huwez umuhimu wa mwanamke ni mkubwa sana akisaidiwa na ww baba,just imagine umepata watoto wote wa kike hivi utaweza peke yako wakifika umri wa kupevuka?pili hata wakiwemo wa kiume peke yako hutaweza na kumbuka watoto hao wanatoka tumbo saba tofaut,zenye tabia tofaut,mtazamo tofaut,mioyo tofaut acha kabisa! Hayo mambo ya kulelewa na wazaz tofaut yanatesa sana acha yatokee kwa sababu maalum c ya kujitakia km hii.
Fikiria tu watoto wanaotoka tumbo moja wanakuwa watu wa kutoelewana sembuse tumbo saba zenye tabia tofaut! Safar ya malez ni ndefu sna na haiishi,jiulize imetokea Bwana kakuita kabla ya wanao hawajafika miaka kumi uliyopanga uishi nao je nn kitatokea????
Tatu badilisha unavyofikir ili ubadilishe unavyosema....Ndoa yangu kamwe haiwez kuwa kama yako...,km sisi tunagombana si kwmb na ww utagombana,kila mtu ana maisha yake,kwann usifikiri positive kwmb utakuwa na mke mwema ktk ndoa bora? Kwann unawaza magomvi tu huwaz furaha? Nina mashaka hata ktk ubaba wako kwa hao watoto wako wajao!km umeshindwa dogo tu hili la kukiri kuwa na ndoa bora usitazamie la kuwa na watoto bora!matunda mazur hutoka ktk mti mzur. Furaha yako haitokan na kuzaa watoto tu kuna kitu kingine cha ziada.
 
Back
Top Bottom