MKEHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 716
- 1,144
Mwezi uliopita nilibahatika kwenda kutembelea wazee wangu Kigoma kupitia Nyakanazi Kagera. Ni njia niliyipita miaka mitatu nyuma. Wakati napitia njia ile tayari ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ilikwisha kuanza kwa ujenzi wa madaraja na Calvert. Cha kushangaza miaka mitatu baadae hali bado ni ile ile. Tena nafikiri imekuwa mbaya zaidi kwani kuna vumbi la hatari.
Barabara bado inasuasua chini ya mkandarasi wa ndani kampuni ya Nyanza Road Works. Sijui nini kinaendelea pale kwani hakuna dalili ya ujenzi kuendelea. Kigoma to Kasulu nako kuanzia Kidahwe hali bado tete japo ni miaka zaidi ya mitano toka madaraja kuanza kujengwa. Ukifika kule ni kama shughuli zimesimama.
Hapa ndo huwa najiuliza mikoa hii ya Magharibi mwa Tanzania sio productive kiasi kwamba hakuna haja ya kuharakisha miundombinu ya barabara? Lakushangaza na kusikitisha sana ni pale unapoana barabara ya kuanzia Himo kwenda mpaka Rombo wilayani iko poa sana. Barabara ya kuanzia Boma kwenda Masama mpaka Machame ni mkeka.
Je, wakandarasi hawapendi hawaendi kujenga barabara za Kigoma na Kagera? Au ni gharama kubwa sana kujenga barabara Kigoma, Kahuku, Kakonko, Buhigwe na Biharamulo?
Naona kama kuna double standards kwenye ujenzi wa miundombinu nchini vile. Iweje wilaya ipate barabara ya lami kabla ya makao makuu ya mkoa?