Bado ananipenda kweli?

Kaazi kweli kweli...

Huyo hana lolote nae anakuzimia lakini ana mambo ya kitoto na inaonekana hujajua hili bado..

Cha kufanya mwache na fanya mambo yako bila kinyongo nae,onesha una furaha na usimtafute subiri mpaka yeye aanze kukutafuta...

Atakurudia tu na akifanya hivyo jiangalie kama bado wakati huo utakuwa unamhitaji,kama utakuwa unamhitaji mwambie wazi kuwa unahitaji msimamo na akikuelewa endeleeni kula raha ya dunia

Asipokurudia shukuru Mungu endelea na maisha yako...

Ukiwa unafanya zoezi hili utapata upinzani wa hisia,usirudi nyuma na usizisikilize hisia zako maana hutakufa kwa kukosa raha kwa muda,hii ndio njia ya kukua,endelea tu na utaweza....

Kila la kheri...
 
Haaaa dada pole wanaokushauri wengi ni ME,wanajua walivyowenyewe,nakushauri ufuate wanayosema jamaa amekuwa mkweli
 
We ushaambiwa kila kitu sijui bado unang'ang'ania nn..Endelea na maisha yako huyo jamaa achana nae..Na nakushauri kaa nae mbali..Mana kadri unavyozidi kuwasiliana nae we ndo unazidi kudevelop feelings kwake wakati ye hana habari..
 
Ushaachwa ila hujaridhika nankiasi cha maumivu ukichopata



Kukujibu


Hapana...hakupendi
 
We ushaambiwa kila kitu sijui bado unang'ang'ania nn..Endelea na maisha yako huyo jamaa achana nae..Na nakushauri kaa nae mbali..Mana kadri unavyozidi kuwasiliana nae we ndo unazidi kudevelop feelings kwake wakati ye hana habari..

Watu wengine sijui waambiwe kichina......
 

huyu hakupendi ila wewe unaonekana unampenda sana hadi ukawa kipofu wa kuliona hili, nakushauri jikaze baada ya muda utamsahau na utaendelea kufurahia maisha
 

Nyie bado mnapendana ila jamaa anakupima wewe na binti mwingine na hajaamua bado awe na yupi hasa.

Halafu Acha Matusi yanakupunguzia kama sio kukuondolea heshima.
 
Mpendwa father superior, waswahili wanasema ukweli wa mtu upo moyoni mwa mtu. Nadhani hilo swali lako ungemuuliza huyo mpenzi wako Yeye pekee ndieye anayeweza kukuambia ukweli kama bado anakupenda au la endapo ataamua kukueleza ukweli.
 
Anaona furaha ma amani mkiwa kama marafaki. Anakupenda kama rafiki na siyo vinginevyo. Keshoaona akuachie mapema kabla hamjaanza kusema mmepotezeana muda.
 

Kukupenda huyu bado anakupenda sio kimapenzi ila kama kirafiki tu, Kwanza nampa pongezi huyu jamaa kuwa open kwako kuliko kukupotezea muda ukadhania una nafasi kumbe laa. Jamaa ana tabia kama zangu kuachana na mtu kwa matusi kwangu no amekuja kuomba penzi kistaarabu na amekuwacha kistaarabu. ukiwa na rafiki kama huyu utajifunza mengi kwenye maisha ya mapenzi na ya kawaida. kuna story nimemaliza kuisoma alieposti anaitwa Natafuta yaani huyu mtu nimemuona wa maajabu sana.
 
Haya ndo madhara ya kuwa kwa mahusiano mda mrefu eti wanasomana, kama anataka kusoma si aende shule? Bi zeya weitingi utapoteza bahati kwa wanaokulilia.
 
Mpendwa father superior, waswahili wanasema ukweli wa mtu upo moyoni mwa mtu. Nadhani hilo swali lako ungemuuliza huyo mpenzi wako Yeye pekee ndieye anayeweza kukuambia ukweli kama bado anakupenda au la endapo ataamua kukueleza ukweli.

Ninapomuuliza jibu analonipa ni kwamba bado ananipenda sana. Hata kuna muda anakuja akiwa amelewa na anadai ananipenda lakini matendo yake siyaelewi.
 
Watu ambao kweli walikuwa katika mahusiano hawawezi tena kuwa marafiki, hii nilijionea hata kwangu. Huyo mtu wako bado anakupenda ila inawezekana sasa hivi anahitaji nafasi ya kufanya jambo fulani ama anakupima nini tu kutaka kukujua vema. Vumilia tu, anaweza kurudi endapo utafaulu mtihani wake. Mpe nafasi, acha kumtafuta wala kumtukana.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…