Badala ya siku ya WANAWAKE; Tungekuwa na siku ya MWANADAMU DUNIANI Kama Mungu aliyopanga

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,752
5,497
Dunia imegawanyika katika vipande viwili. Sisi tunaoamini MwanadamU ni zao la Ufundi wa Mungu na kundi lingine wanadai mwanadamu aliibuka kwa bahati nasibu.

Yawezekana kungekuwa na siku ya MWANADAMU Duniani ingejibu swali kwa nini tuwe na SIKU YA MWANAMKE Duniani.

Kwa mtazamo wangu ninaeamini UUMBAJI wa Mungu, Mungu aliwawekea wanadamu wote Utaratibu wa Kukumbuka siku ya Mwanadamu angalau Mara Moja kwa Wiki yaani SABATO(Jumamosi kwa Mujibu wa wayahudi) au SIKU YA MAPUMZIKO. Lengo kuu ilikuwa ni kuwakumbushwa wao ni wakina nani na asili yao ni ipi na nini kiko nyuma ya yote yanayoendelea duniani.

Ndio maana katika Sehemu Mbili (naam TATU kwa tunaomini YESU ni Mungu)ambazo Mungu aliandika kwa Kidole chake mwenyewe Ni katika zile MBAO MBILI ZA MAWE na MAelezo Kuhusu Kukumbuka kuumbwa kwa mwanadamu ndio marefu(Kutoka 20:8-11) kuliko maelezo marefu kuliko maandishi yoyote yaliyowahi kuandikwa na Mungu. Cha ajabu Dunia karibu yote Sio tu ya Wasio amini uwepo wa Mungu bali wanaosema wanamwamini Mungu wanapinga vikali ukweli huu mwepesi kueleweka.

BADALA YA SIKU YA WANAWEKA, NAPENDEKEZA SIKU YA MWANADAMU DUNIANI AMBAYO NI MARA MOJA KWA MWIKI .

Hii ndio ingekuwa sikukuu kubwa kuliko zote duniani ambayo inafikirisha mwanadamu anatoka wapi anaenda wapi na kwa nini yote haya yanawapata wakazi wa dunia hii.
 
walionzisha hii siku walikuwa na yao,ni mwendelezo wa Mind Control and Manipulation,ila kama huwezi tumia akili utahisi kama ni kitu murua sana ila ni usanii tu kuleta mgawanyiko katika jamii,Mwanamke,mwanaume,Mtoto nk kila mmoja ana umuhimu wake kwenye jamii na huhitaji kuwa na siku maalum kuonyesha umuhimu wa mmoja wao,wana saikolojia wanaamini muda mwingine hata vilema wameshindwa kuonyesha vipaji na uwezo wao smply tu kwa kuwa jamii imeamua kuwaaminisha kuwa wao ni vilema ni watu wasio weza chochote (japo sipingi au kubeza hali walizo nazo) wakati kila mmoja Mungu alivyo Muumba kuna kazi amempatia au kipaji anachoweza kuwafanyia wengine,kama ni kuimba, kuwashauri wengine nk
 
Haina shida mkuu tumeamua kugawana hz siku 365 za mwaka mzima wanawake wamejichukulia hyo siku moja na zilizobak zote ni za wanaume..
WANAUME EEE.... EEEEE!!!
 
Back
Top Bottom