Badala ya sh 40 napendekeza sh 2 kwa lita

Mr Equalizer

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
611
726
Hatua ya kuondoa road licence ni nzuri kwani kodi hii ilikuwa ni kero sana. Kwa mfano gari umepaki huendeshi kwa sababu nyingi labda umesafiri nje ya nchi kimasomo , lakini bado eti wanakudai hii kodi.

Pamoja na wazo hili kuwa zuri ,kiasi cha sh 40 kwenye kila lita ya mafuta ni kikubwa mno . Kuna watu hawajapiga hesabu ndio maana wanashangilia. Lakini ukikaa chini na kupiga hesabu utagundua kuwa watu tunaenda kulipa pesa nyingi kuliko hapo awali. Na zaidi sana pesa hii inaenda kulipwa hata na wale wasiokuwa na magari.

Hivyo napendekeza badala ya sh 40 iwe sh 2 .

Haya ni mawazo tu niko tayari kukosolewa.
 
Natumia lita nane kwa siku.sasa nipigie mahesabu kwa shilingi arobaini nitalipa shilingi ngapi kwa mwaka, na kwa hiyo shilingi mbili yako unayopendekeza nitalipa shilingi ngapi kwa mwaka?
 
Hesabu zangu zinaonyesha sitalipa zaidi ya laki1/year, ww unazungumzia hesabu gani
Mkuu hebu piga hesabu ya gari linalofanya safari zake dar mwanza, haya magari hutumia lita 300 kwa siku hvyo basi

Lita 300 x 40 kisha zidisha kwa siku 30 yaani mwezi baadae zidisha mara 12 kwa mwaka uone hyo hesabu yake
 
Mkuu hebu piga hesabu ya gari linalofanya safari zake dar mwanza, haya magari hutumia lita 300 kwa siku hvyo basi

Lita 300 x 40 kisha zidisha kwa siku 30 yaani mwezi baadae zidisha mara 12 kwa mwaka uone hyo hesabu yake
hakuna gari ya mikoani inayofanya kazi siku 30 kwa mwezi, ikijitahidi saana ni siku 20-25(top)
 
Mimi naona imekaa poa tu tena nimefurahi mno! na si kweli kuwa itawanyonya maskini
kwani kama hawa wapuliziaji wa kawaida wa mikorosho hutumia si zaidi ya lita 10
hivyo watachangia Tsh 400. Tusidanganyane kwa kukuza mambo haihitajiki digrii ya uchumi
kutambua hilo hata elimu ya kawaida ya std 7 inatosha.
 
nilikuwa nalipia gazi zote, ila kwa ss ntalipia pale nnapotumia tu.
Nimekusoma mkuu ,lakini naomba usijifikilie wewe tu , tazama kwa mapana , kodi hii inaenda kulipwa na watu wangapi?
Pili haitasababisha kupanda kwa bidhaa za mhimu pamoja na nauli za mabasi?
Unapojadili haya mambo yatazame kwa mapana ndipo utaelewa maana yake.

Mimi naona hata sh 2 kwa lita bado serikali itapata pesa nyingi tu. Lengo ni kuwapunguzia mzigo wana nchi siyo kuwazidishia ugumu wa maisha.

Wafikilie watanzania wa vijijini mafuta yakipanda hali itakuwaje?
 
Mimi naona imekaa poa tu tena nimefurahi mno! na si kweli kuwa itawanyonya maskini
kwani kama hawa wapuliziaji wa kawaida wa mikorosho hutumia si zaidi ya lita 10
hivyo watachangia Tsh 400. Tusidanganyane kwa kukuza mambo haihitajiki digrii ya uchumi
kutambua hilo hata elimu ya kawaida ya std 7 inatosha.
Unajua impact yake katika mfumuko wa bei?Watu wengine hamuamini bila kuona!Nauli lazima zipande!
 
Itabidi waweke viwango kuendana na aina ya matumizi ya motor vehicles na ujazo wa injini.
 
Huwezi tumia lita 300 kwa mwezi kama huna shughuli inayokuingizia kipato kikubwa.mm naona ni sawa tu kila mtu achangie kodi maana barabara hakuna asiyeitumia.hii imekaa kama luku lipia kadri utumiavyo.sasa hivi hata stj ,dfpa zitalipia hii ni sawa kabisa.kuna bodaboda ngapi nchini na zilikuwa hazilipi road license.sasa hivi nazo zitalipia indirect.
 
Kimsingi hata zile mashine za kusaga nafaka zinazotumia mafuta nao watalipa iyo shilling 40 per litre pamoja na wenye majenereta
 
Shida yenu mnahesabu hasara ya kuendesha gari moja tu,

Huyo mwenye kampuni anaweza kuwa na magari 10, halafu sometimes yanatembea ma2 au ma3 tu mengine yoote yako juu ya mawe. na hii mnaichukuliaje?
Na vp je mwenye magari hayo 10 na yote yako kila siku yako barabarani?
Nauli lazima zipande!;
 
Hesabu zangu zinaonyesha sitalipa zaidi ya laki1/year, ww unazungumzia hesabu gani
Nadhani watu wengi wanaona hawatalipa zaidi na inaweza kuwa kweli hawatalipa zaidi ukipigia kwa mafuta wanayotumia kwa mwaka...ila kama ukiangalia indirect costs...gharama za chakula,usafiri wa ndege,usafiri wa mabasi bei zitapanda, bei ya chakula itapanda,inflation juu...
 
Back
Top Bottom