Badala ya kulialia na kejeli upinzani uje na bajeti mbadala ikionesha mapato na vipaumbele

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Ndugu zangu,

Baada ya waziri wa fedha Dr.Philip Mpango kuwasilisha mapendekezo ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/20 yenye kuanisha vyanzo vya mapato na vipaumbele kwenye matumizi kwa kuzingatia maoni ya wananchi na ilani ya CCM.

Nawashauri wapinzani badala ya kulia lia,kukejeli na matusi watakuwa watenda haki endapo watatengeneza bajeti mbadala ikianisha vyanzo vya mapato na vipaumbele katika matumizi.

Vyama vya upinzani vyenye muundo wa kitaasisi hutengeneza mpango mbadala ili kuwa na hoja kwenye mjadala wa bajeti.Hii itawaepusha wabunge wa upinzani kuepuka kutoa kejeli kwa mtoa hoja na badala yake watajikita kwenye hoja.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom