Backup data zako!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Backup data zako!!

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Kang, Nov 13, 2008.

 1. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Katika dunia ya sasa watu tunategemea sana kompyuta na digital data, kwa hiyo kifaa chako kikiharibika/kupotea/kuibiwa unaweza kupoteza vitu vingi sana.
  Hivyo ni muhimu kutengeneza Backup (Yaani copy ya vitu vyako) mara kwa mara.

  Q:Nifanye back-up ya vitu gani?
  A: Hili linatofautiana na mtu, lakini kwa ujumla ni muhimu kubackup vitu ambavyo haviwezi kupatikana kabisa au hupatikana kwa shida sana vikipotea Kwa mfano:


  • Picha/video ulizochukua na digital camera. Kila ninayemjua ameibiwa laptop anakumbuka hizi kwanza! Irreplaceable!!
  • Document ulizoandika kama ni essays au thesis etc nishawahi kuona tangazo limebandikwa shule la mtu amepoteza thesis yake ambayo ilikua kwenye flash drive.
  • Kama kuna software muhimu ambayo hauwezi kuipata kirahisi.

  Vitu kama movies, music etc sio muhimu sana kutengeneza backup yake kwa vile vinapatikana kirahisi kutoka sehemu zengine.

  Q:Ni jinsi gani nitafanya backup?
  A: Backup ni copy tu ya data zako kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
  Njia rahisi ya kutengeneza backup ni kwa kutumia Recordable CD/DVD, kama una DVD writer basi mara moja moja unachukua DVD empty unadumbukiza data zako, jaribu kuweka backup copy mbali na original!! Haina maana kuweka backup copy kwenye begi la laptop! Likiibiwa vinaenda vyote!

  Kuna software pia ambazo zinaweza kufanya backup kila baada ya muda fulani automaticaly, kuna za kununua na za bure.

  Kama una data nyingi sana kiasi kwamba kuzichoma kwenye DVD inakua ngumu unaweza ukatumia external tape au harddrives.


  Pia unaweza kufanya backup kwa kuweka vitu vyako online, kuna services za kulipia kama Online Backup, Data Backup & Remote Backup Solutions from Mozy.com – Welcome (2GB free!!) amabapo unaweza kuweka data zako. Kutumia service kama hizi inabidi uwe na mtandao wenye unlimited au high data limit. Hawa jamaa pia wanakupa software ambayo inabackup files zako kila baada ya muda fulani.

  Njia nyingine ya kuweka vitu online ni kujitumia Documents mwenyewe, e.g kama una file moja unataka uibackup then itume kutoka email yako moja kwenda nyingine, tena siku hizi yahoo mail ina unlimited storage!

  Niishie hapo for now, kama kuna maswali msisite kuuliza!

  Kama unahitaji software jaribu Free Software Downloads and Reviews - Download.com unaweza kusearch za kununua au za bure ukikosa uliza humu ntajaribu kusaidia.

  P.S: Kuandika kwa kiswahili kuhusu IT ngumu sana!!!
   
 2. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2008
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pamoja mkuu nadhani ujumbe umetufikia tunashukuru sana......
   
 3. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135  Kazi yako nzuri mzee Kang
  .
   
 4. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndugu kang,

  asante sana kwa maelzo yako mazuri, nimehamasika kabisaa na mimi kufanya back up ya data zangu!

  Swali ni je, nitatumia sotware gani ya bure na ya uhakika katika backup ya vitu kama vile picha, documents and software zangu?

  je unaweza ukanrecommed a free software kwa ajili ya kufnayaia back up kwa ajili ya vitu kama hivo?

  nakuhsukuru sana
   
 5. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mkuu kang ni kweli...kuandika kuhusu IT ni ngumu kwa kiswahili...ila hata hapo umejihidi sana....Pili...kuhusu software wengine ni ngumu hata kutumia hizo software...nachoweza kukandamizia kwenye makala yako ni kwamba unaweza kuwa na External Hard drive mbili..hizi ni nzuri...moja unaweza kuwa unatembea nayo na nyingine inaweza kuwa nyumbani kwa maanaa keep orginal data away from back...hii ni sheria katika backup..huwezi weka tape za back kwenye server room...ambako ndio unafanyia backup.
  Mie ndio naona njia rahisi....kwa kuwa ni ku copy from one external to another.Kisha ukifanya marekebisho kwenye original data unaenda fanya marekebisho kwenye back vile vile....kuepusha kuwa na CD mia katika mwaka mmoja.

  Regards
  Buswelu
   
 6. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Njia simple na ambayo naitumiaga ni kuchoma data kwenye DVD, DVD recordable ni cheap na haziharibiki kwa mda mrefu sana. Program nzuri ya bure ya kuchoma:CDBurnerXP
  Link: CDBurnerXP: Features

  Kama unahitaji something more complex jaribu SyncBack Freeware
  Link: SyncBack Freeware - Free software downloads and reviews - CNET Download.com


  Pia Unaweza ukatengeneza Backup ya PC nzima!! Hii ni nzuri wakati umeinstall operating system mwanzoni, na umeshaweka kila kitu vizuri, compyuta ikibuma baadaye unakua una restore fasta badala ya kuanza kuinstall kitu kimoja kimoja.
  Link:Drive Backup Express (32-bit) - Free software downloads and reviews - CNET Download.com
   
 7. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Ni kweli external HD ni nzuri hasa kama data zinabadilika sana hakuna haja ya kuchoma CD nyingi.
  Lakini HD nazo zinakufaga, ndo maana nazichukia wakati mwengine.
   
 8. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  mkubwa sina la kuongezea ila naweza sema tunashukuru,umetumia lugha nyepesi na technolojia nyepesi ambazo kila mtu mwenye hata kaujuzi kadogo ataelewa,tunashukuru sana kaa.
  Haya ndio mambo ya watu wa IT tunayotakiwa kufanya,lazima tujitoe muhanga kwa maendeleo ya taifa kwani maendeleo hayaji bila ya technology.
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,174
  Trophy Points: 280
  Mkuu ulivyoiweka kiswahili umefanya vizuri sana, maana hizi articles ziko nyingi sana kizungu lakini si unajua wengine umande tulikimbia, tehe tehe tehe!
   
 10. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  Niongezee:
  Kinachofuata baada ya kufanya backup ambacho ni muhimu sana kuzidi hata zoezi lenyewe la ku-backup, ni kuzijaribu data toka kwenye kifaa chako cha backup (data restoration test).

  Isije ikawa unafanya backup siku nenda rudi, halafu sasa, ghafla umepoteza original data zako, ushindwe kusoma mafaili kwenye backup. Napendekeza kutoweka imani sana kwenye CD/DVD maana uwezekano kwamba utashindwa kuisoma DVD yako baadae ni kubwa.
   
Loading...