Bachelorette usije sema hatujakukumbusha

Bachelorette usije sema hatujakukumbusha

Zemanda

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2021
Posts
10,664
Reaction score
22,843
Tunaishi kwenye ulimwengu ambao tuna wanawake wanaoamini wana machaguo ya wanaume yasiyokuwa na mwisho. Wanascroll from from left to right wanapopata connection za ukweli za kimahusiano sababu ya kukwepa commitment kwa kisingizio cha red flags za kusadikika. Wanaendekeza tabia ya kukwepa wanaume kwa kuwakalia kimya na kuona ni aina ya kukua/maturity, growth (ghosting growth), ujanja, au validation ya kupiga hatua kama mwanamke anayesonga mbele kimafanikio.

Wanachanganya “kuwa huru” na kukwepa majukumu au kukwepa kufanya maisha kwa kuamini wapo huru kipindi wanachokitumia kufanya usichana na shughuli ambazo miaka 10 ijayo hizo shughuli hazitakuwa na maana wala mchango wowote katika ubora wa future zao.

Lakini jambo wasilofahamu ni kwamba katika kukwepa commitment na wanaume kipindi hiki cha usichana sio tu kwamba wanakwepa majukumu ya kiutu uzima ambayo ni sehemu ya makuzi ya ujana na kuingia utu uzima ila wanatengeneza na kuuandaa mfumo wa akili ambao utakuwa unakwepa majukumu na kukubali kushindwa kwenye mambo mengi hata binafsi siku za mbeleni.

Kutafuta sababu ya kukimbia mapema pale changamoto ndogo za kimahusiano zinapojitokeza badala ya kutafuta njia na namna za kurekebisha mahusiano especially pale muhusika upande wa pili anapokuwa ana changamoto za kimaisha na si za kiuzembe ila anauhitaji uhuasiano na yupo tayari kuendelea,kuishi kingono na watu tofauti, kujidanganya kuwa muda wa kupoteza upo mwingi na usichana hauishi utakuwa mzuri kwa miaka zaidi ya 40, kuacha huyu haraka ili ukawe na mwingine mpya ukiamini utadumu nae badala yake unakuja kugundua hata mpya nae ana changamoto zake, hivyo kuacha na kuanza upya inaanza kuwa mchezo rahisi kufanya.

Kwako dada, endelea kufanya haya kwasababu umetaka usisingizie kuwa ni dunia au maisha yanakupelekea kufanya haya yote. Hii ndio itakuja kuwa utambulisho wako popote unapokwenda na hautaiona ila watu watakwambia ndio tabia zako.

Hasara unayoivuna sio tu ya kukosa mahusiano yatakayodumu muda mrefu hadi uzeeni bali pia unakosa nafasi ya kuiona nafsi yako katika ubora wake wa kuwa mtu real, genuine na anayependa kweli kutoka moyoni asiye mbinafsi kwa wengine.
 
Wanawake wapo walio tayari kuwa wake wakiwa na umri mdogo tu. Ukiacha kutazama hawa modern women na degree zao mjini, ukawakwepa masister doo na slay queens pamoja na wafuga kucha, wanawake wapo.
 
Wanawake wapo walio tayari kuwa wake wakiwa na umri mdogo tu. Ukiacha kutazama hawa modern women na degree zao mjini, ukawakwepa masister doo na slay queens pamoja na wafuga kucha, wanawake wapo.
Upo sambamba na mimi.
 
Wanawake wapo walio tayari kuwa wake wakiwa na umri mdogo tu. Ukiacha kutazama hawa modern women na degree zao mjini, ukawakwepa masister doo na slay queens pamoja na wafuga kucha, wanawake wapo.
Tunawajulisha kabisa ili siku za baadae wasije na story za kwamba hawakuwa wakijua chochote na jamii iliwakalia kimya. Saa hii wale wadada waliokuwa wanajishaua miaka ya 1970 na 1980 wapo kwenye joto ya jiwe wanalipia hesabu ya viburi vyao.
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom