Babu yangu hanithamini.

Babu yangu hanithamini.

mcoloo

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
918
Reaction score
1,402
Babu yangu ni mfugaji anaye ishi kando kando ya ziwa Victoria na sjui ni kwanini Babu aliamua kuwa mfugaji kuliko kuwa mvuvi wa samaki wanao patikana kwa wingi ziwani , naona hilo lisinisumbue kuna siku Lita bainika na kuwa wazi zaidi .

Turudi kwenye mada husika kwanini nasema Babu hanithamini.
Ukweli nikwamba nimeishi na Babu kwa muda mrefu sana na huku Mimi nikiwa ndiyo mchapa kazi hodari wa kazi za halo nyumba . Malishoni jua lilikuwa langu na mvua .

Karibu na kwa Babu yangu kulikuwa na familia moja ambayo ilipambana sana kupata maisha bora lakini mambo yakawa hawaendei vizuri japo jamii ya pale tulipo kuwa tuki ishi iliipenda sana familia hii kwa jinsi walivyo kuwa wapambanaji katika kutafuta maisha bora na wala si kwa ajili yao tu Bali kwa ya wana kijiji wote .

Kadri Siku zilivyo enda waligundua fursa ya uwezekano wa kupata maisha bora yako pale nyumbani kwa Babu , na kumbe cha ajabu sana waliisoma tabia ya Babu yangu kuwa alikuwa MTU kandamizi kwa watu nyumbani na kwamba alikuwa hapendi maendeleo kwa sana familia hiyo.
Hivyo kwa kutumia mwanya huo wakaanza kuja nyumbani kwetu kwa kisingizio cha kuja kumsaidia Babu kufanya kazi pia waka mlemba kwa sifa nyingi , na ukweli ni kwamba Babu alikuwa mpenda sifa. Basis babu alipo ona sifa zina miminika kutoka kwa familia hii ya wageni akaanza kututelekeza ,tulikuwa tukilala kwenye nyumbani nzuri Mara tukahamishiwa banda LA uani Sikh sinyingi tukamishiwa kwenye kibanda kinacho vuja mvua ikinyesha huku wageni wakichukuwa nafasi na kupewa kazi zilizo bora kuliko Mimi niliye sota na Babu kwa muda mrefu.

Jamani naomba msaada wenu nifanye mini ili Babu aweze kurudisha mapenzi yake kwangu na kunithamini ?
 
Huenda babu kashasahau pia kama upo apo nyumbani,uzee una mambo mengi,ebu mshtue kidogo mjukuu,ikibidi kama anamifugo mingi omba kidogo ukaanze maisha yako
 
mcoloo una miaka mingapi? tuanzie hapo kwanza na jinsia yako ni ipi? jibu hayo ili tupate picha ya jinsi ya kukushauri
 
Hama nyumbani, sio kwamba kwenu kupo vizuri ndo unganganie, katafute vyako
 
Sidhani kama una haki kwa babu yako, wanasheria watatujibu hill, lakini kama ulishagundua babu yako anapenda sifa c utumikie kafiri upate kuendesha mradi wako? namaanisha msaidie kazi na msifie!
 
anza kujitegemea, usimtegemee babu kwa kila kitu, ila muwe makini na hao intruders wasije wakajirithisha vitu vya babu yenu.
 
Babu haelewi kitu anazidi kuwamilikisha na anasema yeye ajaribiwi wala hashauriwi , kazi kweli kweli.
 
Hama nyumbani, sio kwamba kwenu kupo vizuri ndo unganganie, katafute vyako
Hilonalo wazo nategemea kusepa Ila nitahakikisha hawa wageni hawaji milikishi Mali nilizo zisotea .
 
Back
Top Bottom