Babu wa Miaka 97 Ashinda Bahati Nasibu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu wa Miaka 97 Ashinda Bahati Nasibu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 8, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,772
  Likes Received: 4,914
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Babu aliyepigika na umaskini maisha yake yote ameuaga umaskini akiwa na umri wa miaka 97 baada ya kushinda bahati nasibu ya mamilioni ya pesa. Babu mmoja wa nchini Vitenam aliyeteseka na maisha ya umaskini miaka nenda miaka rudi, amegeuka tajiri ghafla baada ya kushinda bahati nasibu na kujipatia dola 400,000 (Zaidi ya Tsh. Milioni 500).

  Taarifa zimesema kuwa muda mfupi baada ya babu huyo kushinda bahati nasibu mzozo mkubwa umezuka baina ya ndugu zake wanaowania angalau urithi wa mali zake.

  Jirani mmoja wa babu huyo wa mji wa Ho Chi Minh kusini mwa Vietnam alisema kuwa ilimbidi aingilie kati kumzuia babu huyo asiendelee kuzigawa pesa zake kwa mamia ya watu waliojazana kwenye nyumba yake.

  Pesa zake zote zilizobakia zilipelekwa kuhifadhiwa benki, liliripoti gazeti la Thanh Nien la Vietnam.

  Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Nguyen Van Het alishinda bahati nasibu hiyo baada ya kununua tiketi ya bahati nasibu kwa kutumia pesa alizopewa siku ya mwaka mpya kama zawadi.

  Het amejishindia kiasi cha dong za Vietnam bilioni 7.6 ambazo ni sawa na dola za kimarekani laki nne.

  Afisa mmoja wa serikali ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kuwa ilibidi wazizuie pesa za Het na kumwekea benki baada ya mamia ya ndugu na jamaa kujazana kwenye nyumba yake wakiomba pesa.

  "Tutasubiria wiki kadhaa ili aweze kutulia ndipo tutakapomuuliza anataka kuzifanyia nini pesa zake", alisema afisa huyo.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...