Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Baada ya ukimya wa muda mrefu hatimaye Babu wa Samunge Loliondo, mchungaji Ambilikile Mwasapile ameibuka upya na kikombe chake cha tiba.
Mchungaji Mwasapile baada ya ukimya wa muda mrefu ameibuka na kuitaka kwa mara nyingine Serikali kuboresha miundombinu ya Loliondo kwa kuwa kuna mambo makubwa yanakuja kutokana na maono anayoonyeshwa.
Akizungumza nyumbani kwake katika Kijiji cha Samunge, Tarafa ya Sale jana, Mchungaji
Mwasapile alisema watu waliokuwa wanakwenda kwa wingi miaka iliyopita wamepungua sana na sababu ni kuwa idadi kubwa ya walipokea uponyaji wakati huo.
Mchungaji huyo mstaafu alisema wito anaoutoa kwa Serikali kuboresha miundombinu unatokana na mambo makubwa anayoonyeshwa yatakayokuja hivi karibuni.
Source: Mwananchi