Babu Tale - Kaburi la Muziki wa HIP HOP Tanzania

me1

JF-Expert Member
Jan 24, 2015
367
422
Kwa kila industry kuna watu ambao ndo ma-Godfather wa industry hiyo.

Mfano,ujasiriamali lazma umtaje Mo,Mengi na akina Ngowi.Vivyo hivyo kwenye mitindo kuna akina Flavy,jojo,Kadinda n.k.

Straight kwenye mada,tunapoongelea wadau wa muziki wetu ni watu kama akina Ruge, Fella,Tale,Misifa na wengine kadhaa.

Nimekuwa nikimfatilia sana babu Tale kwenye mahojiano tofauti na vyombo vya habari na amekuwa akinisikitisha mara zote anapokuwa anajibu kwa ujasiri na kishujaa kabisa kwamba yeye haamin katika mziki wa hip hop.

Babutale,ni kweli wew ndie uliemfanya Madee aache kuchana na aanze kuimba kama wasauzi,hongera! Wew pia ndo uliemfanya Raymonnd aamini kwamba Hip Hop ni kichekesho,sawa Raymond kawa mkubwa kwa sasa,ni hatua nzuri japo hana identity yake...hongera pia kwa hili!

Kikawaida kushindwa kwa mtu mmoja hakutakiwi kuchukulia kama general conclusion.Labda wew ndo huwez kupika mastar wa hip hop lakin haimaanishi kwamba mziki wa hip hop haulip lahasha!
A.K.A,Casper,Sarkodie,Phyno na wengine wanafanya hip hop na wana impact kubwa tu Africa,hiv juz nilikuskia unadai Diamond ana wimbo ambao kachana lakin atautoa kama zawad tu kwa vile kibiashara hauwez leta impact.Nani kasema?

Naomba kubali kwamba hujui mziki wa hip hop ili wanaojua wajitokeze wapike wasanii wa hip hop mana mashabiki wa hip hop tupo na muziki wao ukiwa serious tutanunua kama unavyoamin katika hizo pigo zingine.

Wasalaam, Chundabadi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom