Babu na serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu na serikali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Najijua, Apr 28, 2011.

 1. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Najiuliza serikali ina ajenda gani na babu wa Loliondo, ifike wakati apewe Ulinzi na kutumia magari ya serikali?
  Wataalamu wangapi na wakuu wa idara nyeti za nchi hii hawapewi hudma na unyeti anaopewa babu?

  Au serikali imeoteshwa kumlinda na kumbeba? Nasema haya kwa kuwa jana amepelekwa Babati kuhudhuria msiba wa mtoto wake kwa gari la Halmashauri akiwa chini ya Ulinzi wa wana usalama na polisi kuelekea Babati.
   
 2. J

  JABEZ Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndoto zingine zinalipa, we acha tu!
   
 3. Mhadzabe

  Mhadzabe JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 1,648
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Sio vibaya pia kujua ni fedha kiasi gani, Halmashauri inavuna kutokana na Babu kufanya huduma ndani ya wilaya hiyo.
   
 4. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2011
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mzee, suala la Babu lazima uliangalie kutoka pande mbalimbali. Kwa wengine babu ni mganga-mponyaji, kwa wengine babu ni chanzo cha mapato/ uchumi. Nadhani uhusiano wa babu na serikali uko zaidi kwenye uchumi. Halmashauri na wenyeji / wafanya biashara wa maeneo hayo wanajipatia mapato ya kodi kwa njia ya babu. Huyu ni wa muhimu sana. Lazima alindwe kwani ni investment kubwa. Ni chanzo cha ajira na mapato.
   
 5. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Babu ni zaidi ya hao ulio wataja kazi yake inaonekana na imeigusa serikali
   
 6. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wangapi wana investements za kuingizia nchi mapatao makubwa kama TCC na TBL mbona hawapewi ulinzi?wangapi wanafanya uponyaji na utabibu na hawathaminiki?wako wapi Tz Heart Institute na Dr. Masau, serikali inapeleka wagonjwa wa moyo nje bado?au ni sera ya serikali na babu kwa sekta ya Afya?
   
 7. d

  ded2010 Member

  #7
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  amini usiamini babu ni tofauti inabidi apewe ulinzi madhubuti hawajakosea.
   
 8. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #8
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  utofauti wake ni upi?
   
 9. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  .
  Babu ni kitega uchumi cha serikali bila kuwekeza mtaji.
  .
   
 10. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Bruker peleka hoja yako PCCB kuwa serikali inatumia vibaya rasilimali fedha ambazo ni kodi ya watz then jibu lake litakuwa hivi kila raia ana haki ya kulindwa na kuhakikishiwa usalama na serikali hasa pale inapoitajika kwa lazima kama hutak kuamin kasome katiba. kama umechukia babu kupewa ulinzi nenda kwa sheikh yahya amroge.
   
 11. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #11
  Apr 28, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  shk yahya hamuwezi Ambilikile kwa uchawi! Unajua babu ndie mkuu wa wachawi EA. Babu anajini mkubwa sana huwa anamjia usingizini, mwenyewe anamwita Mungu.unaona hata serikali kairoga! Inafanya anavyo taka. Sijawahi kuona serikali inayo support ushirikina duniani, kama chazo mapato mbona kina nengi na bakharesa hawajapewa ulinzi.
   
 12. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #12
  Apr 28, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  jamani huyu babu ananivutia ile mbaya. Lazima nifanye mchakato niwe mamsap wake maana sijamsikia bibi tangu nianze kumsikia babu
   
 13. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #13
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0

  Biashara kubwa inafanywa na vigogo huko Loliondo hasa ya usafiri. Uwanja wa ndege wa Arusha daima una chopper za faster za kwenda Loliondo. Unazani ni wamachinga wenye hizo chopper? Lazima wamlinde. Viongozi wenye Landcruzer nao zote wameziamishia kwenye trip za Loliondo!
   
Loading...