Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,310
Dawa hii ni lazima unywee hapa hapa na si mahala pengine na mtu anayetakiwa akunyweshe ni mimi tu
Mchungaji Masapila pia alisema kazi ambayo amekuwa akifanya kwa saa zaidi za 13 kila siku, haimsumbui akidai kwamba tayari alikwishamuuliza Mungu kwamba atawezaje kutoa tiba kwa watu wengi ilihali ni mzee na akaelezwa kuwa ataongezewa nguvu.
Naishukuru Serikali maana naona wananiunga mkono, hii ni dawa kutoka kwa Mungu na wala sio mti pekee na nilijua wakipima hawatakuta madhara yoyote kwani Mungu alikwishanieleza kuwa watapima wataalamu wa ndani na nje ya nchi dawa hii na watakuta haina madhara
Hakuna madhara kwa mgonjwa kuendelea na dawa zake za awali hata baada ya kunywa dawa yake na kwamba si vyema kuacha ghafla kutumia dawa hizo
Mimi nilimuuliza swali: Kwa mfano nimekuja hapo nina ukimwi, nimekunywa dawa na kupona, nimerudi nyumbani lakini kwa bahati mbaya nikapata kisukari, je naweza kuja kunywa dawa mara ya pili kwa ugonjwa huu mpya? Alisema "sina jibu" Kwa kadri nilivyooteshwa mtu atakunywa dawa hii mara moja tu; kwamba sasa uje mara ya pili kwa ugonjwa tofauti - sina jibu. Lakini Mungu si wa hivyo - yaani leo uje na ugonjwa sugu unywe dawa upone halafu upate tena ugonjwa mwingine sugu? Hakika Mungu si wa hivyo - ila ikitokea hivyo - sina jibu!
eti tiba ya Mungu isiporatibiwa na viongozi wa serikali haitakuwa endelevu!! tafakari huyu ni Mungu gani?"Nawaomba muwaheshimu viongozi wanaokuja hapa kwani mbali ya kuja kupata tiba wanafika kuona namna ya kuboresha hali ya mazingira ili tiba hii iweze kuwa endelevu," alikaririwa Babu akisema.
simshabikii sana babu lakini kama source ya hizi quotes ni magazeti, then sina uhakika na credibility ya hizi quotes. for obvious reasons...
kama kuna video clips, zinaweza kusaidia zaidi....ziweke hapa ili tuzijadili.
simshabikii sana babu lakini kama source ya hizi quotes ni magazeti, then sina uhakika na credibility ya hizi quotes. for obvious reasons...
kama kuna video clips, zinaweza kusaidia zaidi....ziweke hapa ili tuzijadili.
{QUOTE=Miss Judith;1797201]kazi ipo!
source:https://www.jamiiforums.com/jf-chit-chat/119766-hoja-ya-shossi-juu-ya-sh-500-ya-babu-17.html
eti tiba ya Mungu isiporatibiwa na viongozi wa serikali haitakuwa endelevu!! tafakari huyu ni Mungu gani?
source:Waziri Simba aonja joto ya jiwe kwa Babu}
Kumbuka kuwa ya kaisali mpeni kaisali na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu, Lakini pia haiishii hapo tu tunahimizwa kuzitii mamlaka zote zilizopo duniani kwani mamlaka hizo zimewekwa na Mungu. Kwa mantiki hiyo sioni kama babu alikosea chochote.
Hili eneo linakuwa finyu sasa kutokana na wingi wa watu wanaofika kupata tiba. Lazima tuhame na Mungu ameshanionyesha eneo ambalo huduma hii itahamia, ila nasubiri tangazo lake kujua ni lini nitahama
"Hapo kale wenyeji wa eneo hili hawakuwa na utamaduni wa kufanya maziko ya wafu, hivyo watu walipokufa walitupwa kwenye bonde hili," alisema.
Akijibu swali kwamba ni nini maoni yake kuhusu tiba hiyo kuhamishiwa eneo la wafu, Mchungaji Masapila alijibu kwa kifupi akisema; "Lilikuwa ni eneo la wafu, lakini Mungu anataka sasa pawe ni mahali pa ufufuo.
Babuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
hahah, babu bado tu anaendelea kuota?
siku ile itakuja kama mwivi
Jamani wana JF. Mimi ninafanya kazi hapa Halmashauri ya Wilaya Ngoro2, makao makuu yake ni Loliondo. Kutoka hapa kwenda Sami=unge ni km 56Km hivi
Mi naomba tu niwaondoe dukuduku maana nyie mpo mbali na hapa.
Ni hivi, Hapa tulipo tulio wengi hatujaenda kwa babu kwa maana ya ule usemi "Nabii hakubaliki kwao". sisi tunaendelea kuwashangaa tu wapitaji wanaotokea kanda ya ziwa kwenda kwa babu maana njia ni hapa kwetu.
cha ajabu zaidi ni kwamba watu tunaendelea kugawanyika kila uchao maana kila siku tunasikia na kuona baadhi ya mabo mapya maana kila mtu anasema la kwake.
wengine wana mashaka na namna alivyoanza; kwamba, Wakuu wa makanisa hasa yale wanayojiita "makanisa ya kiroho" huko mijini kwenu DSM, Mwanza nk karibu wote wanatoka Mbeya (kasoro Rwakatare nk) wengine wote wanatokea Mbeya. watu wanahoji, je MBEYA tu ndiko Mungu anakoona kuwa kunafaa sana watu wa maajabu watokee?(ukizingatia babu naye ni mtu wa mbeya)
Je Mungu haoni mahala pengine??
Pili, babu haishi na familia yake hapo samunge, kaiacha Babati miaka mingi, mh, hii nayo ni sawa??
Tatu, babu ni mch.mstaafu, uliwahi kuona wapi manabii wa Mungu wote walioandikwwa kwenye Biblia wamefanya maajabu lakini kwa malipo? (hata kama ni kidogo?) walipewa bura lakini wakatoa bure pia, babu yeye analipisha kidogo 500/= ni sawa kibiblia? au ndo mambo mapya ya Mungu?
Nne, Babu anasema asipo kupa yeye dawa huponi, mbona kwenye biblia hata Yesu, nabii Elisha nk wenyewe walisema tu neno na mtu akapona hukohuko alipo?? hii ya babu ni mpya??
Tano, kama ni Mungu kweli, mbona ameruhusu na wengine wajitangaze kuwa wanatoa dawa kama ya babu?? Si angeacha tu babu aendelee kugawa dose??
Tutawatambuaje???????
Sita, saba nk, ngoja niishie hapo nisije nikawaondolea imani wana JF ambao walikuwa na mpango wa kuja!
kwa ujumla hili suala bado lina utata sana, niwaombe tu kwamba msome Mathayo 7, Luka 21, na Mathayo 24 mtaona namna Yesu mwenye alivyotahadharisha watu wake juu ya mabo haya hasa ukizingati hizi ni "siku za mwisho"
Nitaendelea kutoa ufafanuzi kadri mtakavyohitaji.