Babu na Bibi Suphian: Tafsiri ya kifo, raha na makwazo ya dunia

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
133
546
BABU NA BIBI SUPHIAN; TAFSIRI YA KIFO, RAHA NA MAKWAZO YA DUNIA.

Kifo nini? Kwangu mimi ni kumbukumbu ya ndugu, rafiki na jamaa zangu ambao tuliwahi kucheka, kuuziana, kufurahiana, kujengeana dunia bora ama shubiri ya kuishi. Darasa la kuwa mtu mwema.

Vitabu vya dini kwangu mimi naona ndio nguzo kuu itoayo faraja ya machungu ya kuwapoteza tuwapendao mno chini ya jua. Msahafu na Bibilia husema kila Binadamu lazima afe, halafu kuna siku atafufuliwa na hatimaye kusomewa hukumu ya maisha yake ya dunia na kuamuriwa na Mungu aende Peponi au Motoni. Mungu atubariki sote tuwe na mwisho uliojaa maisha ya raha na furaha pale peponi jamaan daah!!

Kwa muda mrefu nimekuwa najikuta nataka ku-share simulizi halisi ya maisha yangu na experience yangu juu ya furaha na huzuni ya kifo kupitia Babu na Bibi walionizalia Baba na Mama yangu wazazi walionizaa mimi na kuitwa Suphian mnijuao sasa. Leo changamoto ya muda nimeizidi maarifa kwa uwezo wa Maulana.

Babu na Bibi zangu ni zaidi ya Kitabu cha hadithi za kweli zilizojaa mafundisho, furaha, machukizo na matumaini ya kuishi duniani. Tangu mwaka jana wakati Bibi yangu mzaa Baba akiwa hai nilijaribu kuandika hadithi hii ila sikuimaliza, nikaamua kuihifadhi kwa draft ya barua pepe (e-mail) yangu ila mwaka huu baada ya kufiwa na Bibi yangu aliyeugua miaka takribani 3 akiwa kitandani, kuja kuangalia nikakuta draft imefutika, hivyo Leo imenibidi nianze upya.

Babu na Bibi zangu wazaa Baba na Mama zangu walikuwa 'washikaji' mno. Walikuwa zaidi ya wapenzi, marafiki na ndugu wa kuzaliwa tumbo moja. Hili nimelishuhudia kwa macho yangu, maana Allah amenijalia kuwaona wote kwa macho yangu na kuishi uchungu na zaidi u-peremende wa ulezi wa maisha yao.

Ilikuwa Asubuhi ya saa 1 mwaka 2006 katika kijiji cha Minyughe, Wilaya ya Singida Kijijini (Kwa sasa Ikungi) Mkoani Singida NILIPOZALIWA, nikijiandaa kwenda Singida Mjini kulala kwa ndugu zangu, ili kesho yake nipate kuwahi kupanda basi la Saa 12 Alfajiri Kuelekea Morogoro na kuunganisha basi la kwenda Mkoani Mbeya nilipopangiwa kusoma Kidato cha Tano na Sita, ndipo nilipojikuta napata wazo lazima nikawaage kwanza Babu na Bibi yangu ambayo walikuwa wakiishi mita zisizozidi 100 kutoka boma letu.

Wazo la awali lilikuwa ni kuondoka bila kuwaaga. Ila ghafla ilinijia hisia kwamba nisipomuaga Babu (aliyekuwa anaumwa miguu kwa miaka kadhaa) basi nisingemkuta tena. Hiki kitabia cha kuhisi vifo vya watu au matukio muhimu maishani wakati huo na hadi sasa kilinitawala sana, na hadi sasa sijui ndio mtabiri au vipi maana kuna mengi nimeyahisi na yakatokea hivohivyo ingawa huwa siri yangu na huwa siwezi kusema kwa yeyote yule kabla ya matokeo kutokea. Nadhani ni Karma ya Mungu, msije sema mlozi bure....hahaha

Basi nikamwamsha Kaka yangu Idrissa aliyezaliwa kabla yangu (maana mimi wa Pili) tukamwage Babu, naye akakubali. Kabla ya kwenda likanijia wazo "hivi katika ukoo wetu kuna mwenye picha ya babu yetu Mzee Nkuwi?" nikagundua hakuna hata mmoja aliye na picha yake kwasababu kuu tatu; moja wengi hawakuona umuhimu huo, pili teknolojia ya kupiga picha kama mjuavyo kijijini ilikuwa mtihani na ghali kiasi na tatu aisee Babu alikuwa 'mtata balaa' maana hakutaka kabisa kupigwa picha, kwake picha ilikuwa 'taboo' kama ilivyo kula 'nyamafu' kwa ndugu zangu Waislam ha ha ha ha

Nikawaza hivi ukali wake ule niutii tusipate kumbukumbu yake kabisa au tufanye 'mitikasi' apigwe kwa udi na uvumba? Basi na kaka Iddy (wanamwita Baba D hapo kijijini) tukapata wazo tumtafute Mpiga picha wa kijiji (wa wakati huo) Bwana Langu Mpuju aje apige kwa kushtukiza... Ila wakati huohuo sina hata thumni ya kumlipa ingawa nilimwambia bro Iddy nina hela yake kumbe uwongo tu, Ha ha ha ha

Cameraman Langu Mpuju akaja home na sisi wawili pamoja tukaenda kwa boma la Babu. Tuka-mpanga Langu akae nje tuingie kwanza aje kwa 'suprise' hahhaa. Kuingia tu kupitia geti la miti na Kaka Iddy bahati nzuri kama ilivyo desturi yake Babu yetu Mzee Nkuwi huwa anatoka barazani kuota jua, basi tukamkuta na fimbo yake ambayo huwa haiachi pembeni anaota jua nayo.

Tukamsalimia, na kuanza kuongea nae mara nyingi alipendea Kiswahili na Kinyaturu mchanganyiko ingawa Bibi alipenda kujibu kinyaturu tu ingawa alisikia na kuelewa mtu akimuongelesha Kinyaturu ama Kiswahili.

Tukipiga soga (kinyaturu tunaita "Sayu"), Langu akaja ghafla (kama tulivyomwelekeza kwenye "Script" ya muvi yetu, asisalimie hahaha) hivyo akapiga picha chap chap kama tatu hivi (si mnajua wakati huo hapakuwa na sijui nikae vizuri au nikae pozi fulani, yaani ukipigwa umefumba jicho moja au yote kama kipofu ndio itatoka hivo hivo na hela utalipa tu hakuna mjadala hahhh).

Picha ikapigwa kama inavyoonekana pichani Kaka yangu Idrissa (First Born kwa Mzee Juma Nkuwi), Babu yetu Mzee Nkuwi Muna (Katikati mwenye X usoni) then mimi Suphian Juma kulia niliyechuchumaa (hivi mbona kama nakataa kuzeeka miaka karibia 15 sasa? Hahha napenda sifa utafikiri Mhaya) na pembeni anayekamua ng'ombe ni Bibi yangu 'Nyamunthi' (Nyayaya). Picha ambayo hadi Leo hii ndio picha pekee walio nayo ukoo mzima hadi Leo kama kumbukumbu ya Babu na Bibi yetu wazaa Baba na wengine wazaa mama zao.

Nilipoingia kidato cha 5 Lufilyo High School Mbeya tu, miezi michache, nikiwa nimelala bwenini mwaka 2006 kupitia simu yangu ya mkononi simu ya 'Motorola', simu ya kwanza kutumia (ukaingia ujumbe wa ndugu yetu Said (majina ya utani Majani au Bonge) kwamba Babu yangu amefariki dunia. Niliumia mno. Machozi yalitiririka kama chem chemu ya maji, Niliwaza ile siku niliyolazimisha kupiga picha na Babu ilimradi tu kumbukumbu yake isifutike daah....na hamuwezi amini hata hela sikulipa kwa mpiga picha ingawa nilikuta picha kwa Baba Mdogo Mpondo na Baba wadogo wengine ingawa hadi Leo sijui nani alimlipa-ga Langu. Asante Kaka Shemeji Langu (shemeji kwakuwa kamwoa mtoto wa Baba Mkubwa Joel Mlagwe).

Babu yangu Mzee Nkuwi alikuwa mkali mno. Alikuwa hashindwi kukuchapa na fimbo yake iwe uwe mjukuu wake ama mtoto wake mwenye watoto. Alikuwa Mzee wa 'principles', hakujali wewe sijui unasifika kwa uchawi kijiji kizima, sijui kiongozi wa Serikali ama una manguvu kiasi gani ilmradi ukimwendea kwa Shari au bila busara basi usitegemee atakuogopa au kukunyenyekea. SAHAU.

Ila kama ilivyo watoto wake 11 (Wa Kwanza Shangazi Yaya, Juma (Babu yangu mzazi), Muna, Mwalingi, Nyamusa, Khangalu (alifariki 1997, kaburi la kwanza kushoto), Kiteu, Asi, Mpondo, Nyatandu na Kitinda Mimba Mdumi) kama inavyoonekana kwa picha ya 3, wote ni watu wapole, waliojaa utu, upendo na umoja ila wakorofi mno ukiwachokonoa....(ulizeni kijijini Minyughe wanajua timbwili lao hahhah) na hivo hivyo hata kwa sisi wajukuu, vitikuu na vilembwe vyao mziki ni ule ule ila sema wengine akina Suphian huwa tunavunga tu hata tukionewa ila tunajijua moyoni kwamba huwa hatuna-ga nidhamu za woga.

Jaaman katika maisha yangu yote naamini mno msemo usemao " Kila Mbabe ana mbabe wake" au "Mapenzi hayana Komandoo", yaani hamuwezi amini Ukali wote wa Babu wa hata kumsema vibaya au hata kumcharaza viboko mchawi fulani anayeogopwa kijiji kizima na asifanywe wala kukutwa na zuruba yoyote ila neno moja la " wewe acha" la Bibi yangu humnyamazisha Babu.

Yaani Bibi ndiye zipu Kuu ya mdomo wa Babu... Ha hah ha ha yaani ukionewa na Babu nenda kwa Bibi, Bibi akisema acha kuonea wajukuu zangu, Babu anaufyata, loh hahhahhhhahh.... Imagine siku ile mpiga picha alipotupiga picha Babu ali-mind kichizi akataka kumpiga fimbo ingawa fimbo na kaka Idrissa tuliidhibiti asimrushie (kama inavyoonekana pichani) ila humuwezi kuamini mkwara wa Bibi wa "Hebu waache watoto wapige picha, kwani utapungukiwa nini" ulimpooza Babu hahhahha Mapenzi yaacheni yaitwe mapenzi jamaani kwi kwi kwiiiiiiiii....

Babu yangu mzaa Baba alikuwa Baba wa familia yenye nidhamu ya hali ya juu mno. Familia ambayo hadi leo imetutengenezea ukoo wa "Unyamwendo" ambao hukutana Mara kwa Mara na kujadiliana maendeleo ya ukoo, kutatua matatizo yetu wenyewe na kusaidiana wenyewe kwa wenyewe kabla ya kushirikisha familia/koo/jamii nyingine ya nje.

Imagine si Babu ama hata Baba yangu au watoto wa Babu yangu licha ya kukerwa, kuonewa, kunyimwa haki kwa namna moja ama nyingine, ila mimi tangu utotoni hadi sasa sijawahi kuona imemshtaki yeyote katika ngazi yeyote ya Serikali iwe ya kitongoji ama juu yake. Kesi zote aidha tumalizane kwa viboko hahhaha au kwa wazee kuamua mhanga kupewa mchuzi ("mahuri", yaani unachinjiwa mfugo iwe kondoo au mbuzi au faini ya hela, mbuzi, kondoo au ng'ombe) yaani hakuna habari ya kupelekana mahakamani.

Wakati wa uwepo wa Babu yangu ilikuwa raha jamaani... Sometimes huwa nakumbuka najikuta naumia sana moyoni na wakati mwingine chozi hunitoka bila habari. Basi ile jioni saa moja hivi unakuta pale barazani ("ugianja", kwa lugha ya kinyaturu) tunakutanishwa watoto wa Babu (Baba wadogo, maana Baba yangu Juma ni mkubwa wao wa kiume ukiachana ma wa kwanza wa kike Shangazi Yaya (Nyamzee), so Baba yangu yaani ni kaka yao) na wajukuu tunaota moto hapo, yaani ni full ma-story.... mara kuna stori ya yule nyoka mkali Koboko, shujaa yule (hapa Babu zaidi anahadithia), raha na karaha za maisha ya mjini (kwa wale waliofika mjini, wakati huo Tabora na Arusha zaidi, hapa vijana zaidi, Baba wadogo) hahaha full full kucheka na kufuhi yaani mixture hahhhahh

Wakati huo Bibi na shangazi zangu na baadhi ya wajukuu zake wa kike wakipika jikoni. Ila walikuwa hawapitwi na soga za "ugianja" za wanaume, maana mara kwa mara kwa mara tuliwasikia wakicheka.

Ninavyovikumbuka zaidi kwa Bibi yangu aliyefariki mwaka wa 2021 ni kwamba Bibi Nyayaa ukiachana na ucheshi wake alikuwa Mtu pekee kwa ukoo ambaye sijawahi kumsikia akiongea Kiswahili hadi umauti unamfika baada ya kuumwa nadhani magonjwa ya uzee. Yaani tulikuwa tunamsemesha kiswahili ila anajibu kifasaha kwa lugha ya kinyaturu hahahahha. Yaani alikuwa Mkalimani akijikalimani mwenyewe hahhahahhhh

Bibi hakutaka kabisa kupikiwa na yeyote enzi zake toka nimjue hadi miaka ya juzi alipozidiwa na ugonjwa. Alikuwa Mpishi mzuri sana. Yaani alikuwa na gubu balaa akipikiwa na mtu. Utasikia mara mboga hazijaiva vizuri mara ugali huu mdebwedo.

Bibi alitupikia boma zima tunakula hata kama kuna mgeni sote tunashiba na kusaza wanawake nao wanakula na kubakiza kiporo. Utaratibu ulikuwa Chakula (mara nyingi ugali wa uwele na mlenda au majani na nyama mwitu) kinapikwa na kuletwa kwa wanaumme kwanza then unarudishwa kwa wanawake. Nawaza sijui kwanini wanawake walishindwa kujikatia Chakula chao dooh.... (Eti sasa hivi ndio nawaonea huruma kwasababu ya utandawazi) ingawa wao walikuwa wanaona kawaida tu.

Bibi yangu alikuwa hajui miaka yake ya kuzaliwa. Basi siku moja namuuliza umezaliwa lini akaniambia "jumlisha miaka ya baba na shangazi zako utapata miaka yangu " haha haha she's was so really charming...na ukimsimulia jambo anatulia na kukusikiliza kwa umakini na mara kadhaa anachombeza stori yako hadi raha yaani.

Kwa upande wa Babu na Bibi wazaa Mama yangu mzazi, Swahiba Chanyera nao hutofautiani sana na upande wa Babu na Bibi mzaa Baba yangu.

Baba na Mama wa mama yangu kikabila walikuwa Wapare kutoka Makanya huko ingawa wote wamekulia na hata mimi tangu utotoni nimewakuta wanaishi na hadi wote mauti kuwakuta wakiwa Kijiji cha Manga Mikocheni, kata ya Mombo, Wilaya ya Korogwe Tanga.

Mimi sikukaa nao sana kama ilivyokuwa kwa Babu na Bibi zangu Wanyaturu upande wa Baba huko Singida. Huko Tanga tulienda tu mara moja moja tu kusalimia wakati huko wazazi wangu wakiishi Arusha, na baadae kuhamia Singida ambapo ndipo watoto wao tulipokulia zaidi na kuanza shule za Msingi na hata Sekondari.

Babu yangu mzaa Mama, Mzee Said Chanyera alikuwa Mzee mcheshi sana, Mwenye busara, Mcha Mungu ila ukimchokoza utakiona cha mtema Kuni. Nakumbuka Mwaka mmoja tukaenda na Kaka yangu Idrissa na Mama kuwatembelea nilipomaliza Kidato cha NNE, asubuhi tukaamshwa tukaenda kulima mpunga, hamadi nikajikata na jembe, kaka Idrissa kuona damu ghafla akadondoka...weweeee... Kilimo kiliishia hapo, sote Bibi, Babu, mama, mama wadogo na wajomba tukarudi nyumbani...

Timbwili lake lilikuwa balaa... Haha Babu alipiga mkwara kila mtaa na kijiji kizima kwamba "aliyewaloga wajukuu wangu awaponye haraka, lasivyo nitachinja mtu" hahaha basi bana tukapewa dawa za kienyeji tukapona. Hapo hakuna cha Panado wala Qwinini he he he he

Basi hapo Bibi anampiga mkwara Babu kwa lugha za kizingua mixture kipare kwamba "wewe tabia zako za kuwatembeza wajukuu kila nyumba kusalimia wakija ukome, ona watoto wamepigwa zongo" hahaha maana juzijuzi tu Babu alituvusha na ngalawa Mto Ruvu kidogo tudumbukie na kumbukeni mto Ruvu una mamba balaa lol nisingekwepo dah tulinusurika kidogo.

And kuna watu huniuliza vipi jina Suphian nililichukulia wapi? Jina hili nililichukua kwa Babu Mdogo (yaani Mdogo wake Babu mzaa Mama) aliyeitwa Suphian huko Tanga. Babu Suphian alikuwa mpole sana, mcha Mungu sana, alitangulia mbele mapema sana yaani mimi nikiwa Mdogo sana hata sura siikumbuki ingawa niliona picha, na kupanda simulizi zake mkewe (Bibi yangu) ambaye yupo hadi leo na ananipenda mno loh haishi kunitaja na kuniita ita... Salaams zake nazipata.

Babu na Bibi mzaa Mama walipenda uchapakazi, upendo na umoja. Bibi alitangulia kuaga dunia mwaka 2007 na mwaka mmoja baadae 2008 Babu akafuata. Mungu awarehemu aisee daah!! Kifo hakina huruma hakika.

UMEJIFUNZA NINI KUPITIA BABU NA BIBI SUPHIAN HAWA?

Ewe Mwenyezi Mungu awaondolee Babu na Baba zetu wote waotangulia mbele ya haki; adhabu za kaburi na aendelee kuwalaza pahala pema peponi, Amina!!

Mjukuu,
Suphian Juma Nkuwi.
suphianjuma-20210403-0001.jpg
IMG_20210403_120210.jpg
suphianjuma-20210403-0002.jpg
 
Mihadithi mirefuuuuu
Halafu hakuna chochote kile cha maana! Eti machozi yalitiririka kama chemchem ya maji! 😁😁😁😁

Huyu Dogo atakuwa na msongo wa mawazo baada ya kumsaliti Bosi wake Zitto na kujifanya kuunga mkono juhudi! Mwisho wa siku ameishia tu kuangukia pua kama yule msaliti mwenzake Benson Mramba !

Waliyemtegemea kuwakumbuka hayupo tena! Kwa sasa hawana namna, itawabidi waishi maisha ya stress tu na kujaribu bahati yao ya kukumbukwa kwenye uteuzi na Rais Mpya.
 
Halafu hakuna chochote kile cha maana! Eti machozi yalitiririka kama chemchem ya maji! 😁😁😁😁

Huyu Dogo atakuwa na msongo wa mawazo baada ya kumsaliti Bosi wake Zitto na kujifanya kuunga mkono juhudi! Mwisho wa siku ameishia tu kuangukia pua kama yule msaliti mwenzake Benson Mramba !

Waliyemtegemea kuwakumbuka hayupo tena! Kwa sasa hawana namna, itawabidi waishi maisha ya stress tu na kujaribu bahati yao ya kukumbukwa kwenye uteuzi na Rais Mpya.
Mi sijasoma nimecomment tu 😂😂😂😂 nimeona upuuzi tu
 
Alichelewa kuhama 😂😂😂
Njaa imeanza kupanda kichwani kiasi cha kumkumbuka Babu badala ya Mfadhili wake aliyemtoa porini Zitto Kabwe!!

Hesabu za kuhama zimemkataa kabisa! Hana tofauti na mwenzake Benson Mramba! Anakula tu malimao kwa sasa! Haeleweki yuko chama gani! Hakuna anaye mjali!
 
Njaa imeanza kupanda kichwani kiasi cha kumkumbuka Babu badala ya Mfadhili wake aliyemtoa porini Zitto Kabwe!!

Hesabu za kuhama zimemkataa kabisa! Hana tofauti na mwenzake Benson Mramba! Anakula tu malimao kwa sasa! Haeleweki yuko chama gani! Hakuna anaye mjali!
😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom