Babu ameniusia Kuowa mwanamke Anayenipenda na Si nnayempenda...

Nyoka_mzee

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
3,695
5,522
Habar zenu wakuu

Naomba Tusaidiane katika kudadavua hili,
Nilikuwa na mazoea Ya kwenda kumuona Babu enzi za uhai wake, na kila mara alikuwa akiniusia kuowa mwanamke anayenipenda na Si nnayempenda ....
Nilijaribu sana kumdadisi sana anifafanulie lakini Hakuwai kato aliishia hapo ,na paka anakaribia umauti aliniita tena na kunisisitizia Tena juu ya hilo,
Mpaka leo sijawahi mwelewa babu hasa alikusudia nini, maana aliniacha njia panda na hakuwai kunifafanulia mpaka umauti unamkuta,
wakuu ebu Tusaidiane mawazo ,alikuwa na hekima gani kuniambia maneno haya??

Msaada kwenu wadau...
 
Alikuwa sahihi kwa asilimia mia ukioa unayempenda wewe itakuwa rahisi kukusaliti ila kama alikupenda wewe na alikutokea kabisa basi huyo ni hadi kufa.ndoa itadumu sana na hata ukifa bado uzao utakao uacha atauthamini kwani kila akiwaona watoto atakukumbuka ww yote hii ni kwasababu alikupenda ww.ila kama we ndo ulimtongoza akakukubali tu ukamuoa hapo ni wewe na yeye ukiondoka basi na yeye anaondoka hakuna anayejali kilichobaki upendo wa mwanamke unanguvu kubwa sana lakini pia kuwa makini usije ukapata wale wanaotafuta kwa kujishkiza tu hawana tofauti na Malaya.babu yako aliongea kitu cha maana sana.
 
sawa mkuu ila nimejaribu kutafakari ili jambo sawa utaowa mwanamke anayekupenda je huwoni mkuu ntaishi kwenye mazingira magumu maana nafsi yangu haipo kwake huwoni kama niko gerezaniii
 
Usijidangany uowe mke usio mpenda angalia usije mtesa mtt Wa watu,je siku ukikutana na yule umpendae huoni unaweza kumsaliti mkeo,ndugu owa kitu ulichoridhia kutoka moyoni,
Ndomana mkuu nikata mawazo ya watu umu maana mimi mwenyeww bado naona haijakaa kichwani vzuriii
ndomana najaribu kupata michanganuo kwenu
 
sawa mkuu ila nimejaribu kutafakari ili jambo sawa utaowa mwanamke anayekupenda je huwoni mkuu ntaishi kwenye mazingira magumu maana nafsi yangu haipo kwake huwoni kama niko gerezaniii
Ni kweli mkuu utakuwa hauna furaha hata kama anakupenda sana na wewe humpendi,ila mkuu sidhani kama wewe humpendi tu ghafla ninauhakika unastandard zako ambazo unazihitaji kutoka kwa mwanamke unayempenda,haimaanishi akikupenda tu basi ndo huyo, hapana hata kama kakupenda ila pia angalia kama anafikia viwango ulivyovitaka kama hafikii basi achana nae watakupenda wengi.ila mkuu pia huo upendo anaouzungumzia babu yako ni ule upendo ambao mwanamke amekupenda wewe kama wewe na sio kakupenda wewe kwasababu Fulani labda et kisa we ni mzuri au et unapesa uzuri na pesa vinaweza kupotea ila utu wako huwezi kupotea na pia mkuu angalia sana standard zako kwa mwanamke unayemtaka siku hizi utaskia et mtu anataka mwenye makalio makubwa, mwingine anataka mwenye degree,mwingine anataka mweupe nashauri vigezo vyako viwe ni vile vyenye ulazima sana mfano mimi napenda mwanamke wa kisasa,mwenye elimu ya kawaida au zaidi,anayenipenda na kinijari,mrembo full stop,tena kukupenda iwe ni moja ya vigezo vyako.hapo nauhakika utampata mwanamke ambaye wote mtapendana na kuishi kwa amani na furaha.
 
mbona utaoa wengi kama ndo hivyo, wanawake kipindi hiki wanapenda balaa....
anyway,,;

√Uzuri wa kitu upo machoni kwa MTU anayekiangalia na sio kitu chenyewe
 
Babu yako ana busara sana, mwanamke anaekupenda ataridhika na hali uliyonayo, atakuheshimu na kukuthamini. Wewe usiombe kupenda usipondwa, hata jehanam kuna nafuu.
Sasa mkuu ikitokea na mimi nikaja kumpenda mwingine apo pamekaaje napo mkuu ?
maana haya maamuzi yanahitaji utulivu na kuangalia kila pande faida na hasara....
 
Habar zenu wakuu

Naomba Tusaidiane katika kudadavua hili,
Nilikuwa na mazoea Ya kwenda kumuona Babu enzi za uhai wake, na kila mara alikuwa akiniusia kuowa mwanamke anayenipenda na Si nnayempenda ....
Nilijaribu sana kumdadisi sana anifafanulie lakini Hakuwai kato aliishia hapo ,na paka anakaribia umauti aliniita tena na kunisisitizia Tena juu ya hilo,
Mpaka leo sijawahi mwelewa babu hasa alikusudia nini, maana aliniacha njia panda na hakuwai kunifafanulia mpaka umauti unamkuta,
wakuu ebu Tusaidiane mawazo ,alikuwa na hekima gani kuniambia maneno haya??

Msaada kwenu wadau...
Kwahiyo uoe usiyempenda kabisa??. Mmm! Furaha na aman utakua nayo kweli..me naamini wanaopendana wapo..kwahiyo omba tu upate umpendaye naye akupende!
 
Mke anaye kupenda alimaanisha yule ambaye haelewi wala asikii pasipo Wewe...yaani anakujali, muda wote Ana kufikiria Wewe na pia anakupenda ulivyo sio kwa unacho miliki.
Asante mkuu napata picha ,endelea kufunguka kuna vitu nakusanya unavyotiririka...
 
Ni kweli mkuu utakuwa hauna furaha hata kama anakupenda sana na wewe humpendi,ila mkuu sidhani kama wewe humpendi tu ghafla ninauhakika unastandard zako ambazo unazihitaji kutoka kwa mwanamke unayempenda,haimaanishi akikupenda tu basi ndo huyo, hapana hata kama kakupenda ila pia angalia kama anafikia viwango ulivyovitaka kama hafikii basi achana nae watakupenda wengi.ila mkuu pia huo upendo anaouzungumzia babu yako ni ule upendo ambao mwanamke amekupenda wewe kama wewe na sio kakupenda wewe kwasababu Fulani labda et kisa we ni mzuri au et unapesa uzuri na pesa vinaweza kupotea ila utu wako huwezi kupotea na pia mkuu angalia sana standard zako kwa mwanamke unayemtaka siku hizi utaskia et mtu anataka mwenye makalio makubwa, mwingine anataka mwenye degree,mwingine anataka mweupe nashauri vigezo vyako viwe ni vile vyenye ulazima sana mfano mimi napenda mwanamke wa kisasa,mwenye elimu ya kawaida au zaidi,anayenipenda na kinijari,mrembo full stop,tena kukupenda iwe ni moja ya vigezo vyako.hapo nauhakika utampata mwanamke ambaye wote mtapendana na kuishi kwa amani na furaha.
Ni kweli mkuu maana umetiririka katika njia zake,
Ila unaweza ukaka na mtu ambaye kweli kuna vitu ambavyo vikakuvutia na kujipa moyo ipo siku utampenda ngoja niishi nae maanq yeye anamapenzi ya dhati ,lakini mwisho wa siku ukajikuta umeshindwa kumpenda na ukajikuta una fall kwa mwingine ,
huwoni apa mkuu unacheza bahati nasibu kupata au kupatwa???
 
Asante mkuu napata picha ,endelea kufunguka kuna vitu nakusanya unavyotiririka...

Ahahahahaha tofauti na yule ambaye ukimpigia simu isipo patikana au asipopokea, Wewe gari linawaka...kazi haziendi yaani full mvurugiko

Yaani unakua Kama mtumwa kwake.

Hapo Upendo upo ila Wewe ndio umempenda zaidi...ndio ile mkikwaruzana Wewe hauna furaha full stress, Mwenzio Hana Habari coz anajua haupindui
 
mbona utaoa wengi kama ndo hivyo, wanawake kipindi hiki wanapenda balaa....
anyway,,;

√Uzuri wa kitu upo machoni kwa MTU anayekiangalia na sio kitu chenyewe
Dah sasa mkuu Tunafanyeje hapo maana Bado hujanisaidia ,yaan umenitoa njiani umenitupa porinii
 
Aisee, Fanya litakaloufurahisha moyo wako hadi kufa.....mm binafsi nilipendwa sana na ninapendwa sana na watu ambao hata chembe ya kuwapenda sina.....nawaangaliaga tu mpaka kesho......hatari dunia!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom