Babies Plagiarism

JF2050

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Posts
2,085
Reaction score
45
Tunajua wote kuwa plagiarism ni serious academic offence! Lakini hili swala sasa limesambaa na kwenda mbali zaidi hadi kwenye jamii ngazi ya familia. Unakuta mke wa mtu ameolewa, halafu sijui kwa makusudi au kwa nia gani anaamua kupigwa "force king", matokeo yake ndio hivyo anaplagiarise mtoto.

Jana nilipita karibu na mlango wa jirani fulani, sasa ndani kulikuwa na akina mama na akina dada kibao. Bahati nzuri au mbaya kuna dada mmoja tumezoeana hapa mtaani, akawa ameniita, njoo uone mtoto jamani, mama fulani amejifungua.

Anyway, huyo mama sijazoeana naye kihivyo, lakini kama unavyojua kumwona mtoto hasa sisi vijana na kumnyanyuanyanyua kisanii hata kama hujisikii kivile, inakuwa kama kusafisha nyota kimtindo. Kwa hiyo mie nikamwibukia mtoto, nikambeba na kumrusharusha kidogo (taratibu, si unajua bado mchanga!).

Huko nyuma nilisikia huyo mama jirani anacheza faulu kibao! Nilipomshika tu mtoto, akina mama:

" Toto, toto, toto; ghii, ghii, ghiii, dume, dume, dume hiloooooo, handsome kama baba yake, ............"

Mama mwingine "Masikio hayo, kichwa jamani hicho, miguuuuu! Huyu ni baba yake kabisaaaaa, kajizaa"

Sasa mama mmoja, ghafla akaguna, "MMMmmh, mbona hata hafananii kabisa na baba yake, sema labda huu weupe ni wa mama yake!"

Mie fasta fasta, nikawa namtafuta mmama wa kumkabidhi mtoto nisepe, ndio mama mwingine "alimrebuke" yule aliyesema mtoto hata hafananii na baba yake, "Utasutwa mwanamke, heheeeeeeee, mjini hapa!"

Kidogo jamaa, mme wa mke mwenye mtoto mchanga, kaibuka kutoka chumbani, kaanza kunisalimia "Mambo vipi Simplicity., karibu sana mkuu, tupo bwana,........."

Aliwapotezea kabisa akina mama wote waliokuwepo hapo, badala yake tukawa tunabadilishana salamu mimi na yeye.

Ghafla mama wa mtoto naye kaibuka, na kumwambia mama mmoja ambaye nilikuwa nimemwachia mtoto "Nipe mtoto nikamwoshe", huku akiwa amekunja uso na kuonekana kutokufurahia!

Kuona hivyo, mie "kwa herini jamani, ahsanteni, nawahi sehemu", huyoooooooooo, mtaa wa kati.

Kilichoendelea sijui, ila jinsi hao akina mama walivyokuwa wanatumiana signals kishambenga huku wengi wao wakiwa macho juujuu, kuna uwezekano waliditect plagiarism!

Jamani hili swala la akina mama kuplagiarise watoto na wapambe wao kujaribu kuwanusuru kwa kuwapa watoto fake brands mbona linakua kwa kasi sana siku hizi?

Mtu ukianzisha bima ya kupakaziwa mtoto si utapiga hela ndefu sana au mnaonaje wadau? Hasa kama unaweza kumudu kununua vifaa vya kupima DNA na kuajiri wataalamu huku ukitangaza "widely" ili watu waje kupata huduma?

CC: lara 1 MadameX Madame B madameA Kongosho Nazjaz Kaunga Smile Sista sister charminglady christine ibrahim Cynthia Chriss mimi49 Heaven on Earth mwekundu watu8 Mashaxizo Himidini HorsePower farkhina King'asti mzabzab etc.,
 
Last edited by a moderator:
Vp lkn huyo mtoto unamuonaje?? wa jamaa au ndio..
 
Hospitali zetu ni chanzo pia cha tatizo hili..

mtoto wa Madame B kapewa lara 1 na wa lara 1 kapewa Lady doctor.. yule wa Lady doctor kapewa Heaven on Earth..

kwa hii cycle unategemea nini?

Hii ya hospitali nilishawahi kusikia mkuu, mama mjamzito akihisi au akijua mtoto wake aliyetumboni (au baada ya kumzaa) ana matatizo, kuna possibilities tatu:

1. Akishajifungua anamfanyia timing mama mwingine mwenye mtoto mchanga na kumbadilishia

2. Anaongea na wakunga wamsaidie kufanya exchange

3. Pia kuna wale ambao watoto wao kwa bahati mbaya wanafariki wakati wa kujifungua au tumboni, wanaaply no. 2 hapo juu

Nasikia kuna hospitali imefunguliwa hapa mjini, kazi yake ni kama xchange point (XP), wale wadada ambao wanapata mimba wasizozitarajia wanaenda hapo na kujifungua, halafu mtoto anachukuliwa na mama mwenye uhitaji. Kuna mama mmoja alikuwa hawezi kuzaa, lakini sijui alikula nini tumbo likawa kubwa, alilibeba hivyohivyo kwa miezi tisa, na baadaye alienda hiyo hosp. na kujichukulia mtoto. Itapunguza kasi ya wadada kutupa watoto.
 
Vp lkn huyo mtoto unamuonaje?? wa jamaa au ndio..

Mkuu sina utaalamu wa kutosha kutambua watoto hasa wakiwa wachanga, lakini inawezekana kabisa ni plagiarised!
 
nimeipenda hii! the system should be adopted.. utupaji wa watoto utapungua sana!
 
Eiyer anaamini atampata mwanamke bikira amwoe, akikutana na hili tango, mbona atajinyonga! Mzee wa Ngololo The Boss na Mtambuzi wanaweza kushtukia maana hawa jamaa inaonekana wanajua sana kusoma hisia za wanawake.

Hivi Humu Jf kuna watu wamekwepa kweli hili? - snowhite, SnowBall.
 
Last edited by a moderator:
nimeipenda hii! the system should be adopted.. utupaji wa watoto utapungua sana!

Hii hata mie nimeipenda, tena hiyo hosp mie naona watangaze kabisa wala wasifanye siri, watanusuru watoto wengi mno, ingawa wanaume kulea watoto ambao sio wao nayo itakuwa njenje, nanjilinji wewe umekwepa kweli hili?
 
Last edited by a moderator:
Hahaha...hiyo inaitwa kuuziwa kanyaboya na kuna wanaume unakuta wanalea si mtoto mmoja tu bali watoto lukuki ambao hawana hata chembe ya damu ya baba...

Unadanganywa kirahisi tu kuwa leo tufanye ndio siku ya hatari kumbe wapi kuna mkware alishapewa jana yake mwanamama anaokoa tu jahazi...
 
watu8 sasa utamfanya Eiyer na jamaa zake wakasomee upadri kabisaa, maana ni kama unawatisha!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu sina utaalamu wa kutosha kutambua watoto hasa wakiwa wachanga, lakini inawezekana kabisa ni plagiarised!

mtoto anabadilika sana miezi 2 ya mwanzo, mara sura ya mjomba, miguu ya baba kisha tabasamu la mama sura ya babu kidole gumba kama jirani... n.k. Labda familia muwe na utambulisho shababi ndio unaweza kumtambua kwa muda huo. Subira inavuta kheri, kama sio utamjua ukubwani >5yrs.
 
Hiyo hospitali ifanyayo hivyo ipo karne gani tena? mtoto anapozaliwa huwa anavishwa kitambulisho mkononi kinacholingana na mamaye...

wanaowavalisha si ni manesi? basi pia hao ndio wanao wavua! these things are happening mr watu8
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin na Ablessed hamjawahi kukutana na hili?
Unajua nilikua sijaelewa nilipofika mwisho ndio nkaelewa. Swala hili tangu zamani lipo sema wazee wetu walikua wanalihandle kiutu uzima na ndio ule usemi usemao kitanda hakizai haramu ulikotokea. Naweza tu kusema jambo hili ni janga la taifa , shida ni kwamba hao wafanyayo hayo nadhani hawajui thamani ya ndoa. Nakumbuka kuna mmama mmoja yaani ukimuona huwezi kutegemea anatembea na mume wa mtu huku yeye naye ameolewa anang'ang'ania kuzaa na huyo bwana kila nikimtizama simmalizi aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…