Baba Yangu Amebaka Housegirl-Mama Anataka Kuondoka!




Ila kwenda polisi bila evidence ndo inakuwaje? akifika kituoni aseme nilibakwa last ... days? si watamcheka?
 
watanzania mnawaza kiajabu sana,hayo so mambo ya kuomba ushauri halafu unashauri nini anghhhhhhhh
 

Chupaku, poleni sanaa kwa dhahama na fedhea iliyowasibu, natafakari nitarudi...
 
Pole mtoa maada, i have high respect and love for a FATHER... ila baba huyo duh.........sina ushauri wakutoa!!

Pole
 
wazee wengine nao 70+ bado anataka afanye mambo ya kihuni! Huyo anatakiwa apewe :ban: ya kuishi uraiani.
 
Unaongea mara waende kwa wazee, kisha unasema waende polisi. Kwahiyo unataka nikafungue kesi? You are just bluffing. Ila sishangai msimamo wako ktk maswala haya nauelewa sana
Mkuu hizo zote ni moja za hatua ambazo mlipaswa kuzifuata, na si kuleta ilo tatizo humu JF.

Ungekuwa unasoma kwa kuzingatia tangia nilipoanza kuchangia thread yako ungekwisha nielewa, lakini si kuchukua majibu niliyo mjibu mtu mwingine na kuyafanya ndio yako.

Sidhani kama unauelewa msimamo wangu...!

Haya mkuu tufahamishe basi mpaka sasa ushapata ushauri gani ambao wewe unauona ni mzuri kuufanyia kazi.
 
Huyu baba atakuwa na ukwasi wa kutisha, au ni skills zipi za kumzuzua binti kigoli hadi aingie laini?! I think 18yrs si umri mdogo wa kudanganywa kwa pipi, palikuwa na mazingira aliyajenga na yeye
 
Huyu baba atakuwa na ukwasi wa kutisha, au ni skills zipi za kumzuzua binti kigoli hadi aingie laini?! I think 18yrs si umri mdogo wa kudanganywa kwa pipi, palikuwa na mazingira aliyajenga na yeye
Mizee kama hii huwainatisha msichana kwa kisu au bastola
 

Pole sana, mimi wala sishangai kwani kuna ndugu yangu wa karibu sana (sitataja uhusiano wangu nae) yuko aged around late 70's lakin kila siku mke wake analalamika mzee hajatulia na huwa anakimbizana tu na dogo dogo hadi anawahonga kile anachopewa na wanae.

La muhimu ni kwamba jaribuni kutomtenga huyo baba yenu kwani mkizidi kumtenga anaweza hata kujinyonga kwa sababu ya msongo. Hakuna lisiloisha, kaeni nae msuluhishe mambo. Kumpeleka baba yako mzazi polisi inataka moyo. Tuongee mambo ambayo ni viable na yanatekelezeka. Kwa upande wangu siwezi. hata kama iweje nnachoweza kufanya ni kumchukia tu.

Kuhusu house girl, mpeni chochote akaanzie maisha. Kumbuka mkono mtupu haulambwi, yani nyie mnampa pole tupu na kumtaka anyamaze?? JF wenyewe wanakubali mkono mtupu haulambwi. Penye udhia penyeza rupia.
 

Pole sana kwa yaliyowakuta,but ingekuwa kwa mila yetu au kabila,ishu kama hizi zinapelekwa kwa wazee wa kimila na wazee wanaimaliza,na huwa ikipelekwa kwa wazee wa kimila ina mana haiendi tena kwenye sheria za serikali ila wazee watajua jinsi ya kumpiga faini na adhabu anayostahili bila kufunguliwa mashtaka,but mila zinatofautiana mana mnaweza mkapeleka kwa wazee but wao wakapeleka kwenye sheria.Ila kama wazee wa kimila hawana tatizo basi heri iende huko mana wana uwezo wa kusolve tatizo pande zote tatu,yaani baba,mama na huyo house girl
 
Wana JF,

Kabla hata sijaanza kuandika niwaombe radhi wale wote ambao kwa namna moja au nyingine wameumizwa hisia, moyo, wametishika, wamekasirishwa na habari hii (hususani X Paster...).

Taarifa zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya Housegirls either wanabakwa au wanaamua kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wenye nyumba. Ni idadi chache sana ya wale wanaobakwa wanatoa taarifa katika vyombo vinavyohusika. Nimetafuta sababu za kufanya hivyo kama sehemu ya utafiti wangu ulio rasmi. Kwa kiasi kutokana na michango yenu nimepata kujua sababu za kutosha kujumuisha na nyingine nilizonazo na kuandika ripoti yangu. Ukisoma michango katika thread hii utaona jinsi ambavyo jamii inayachukulia masuala haya, na hasa nafasi ya housegirl katika nyumba na jamii kwa ujumla. Kwa niliyoyapata katika utafiti wangu ndani na nje ya JF, nashawishika kusema kuwa mabinti hawa waongezwe katika list ya "Vulnerable Groups" katika jamii. Kundi hili linahitaji uangalizi na ufuatiliaji maalumu. Singependa kutoa taarifa zote hapa jamvini katika muda huu, labda hapo baadaye.

Naomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na nawashukuru kwa kunielewa.

CHUPAKU.:A S 103::A S 103::A S 103:
 
Mkuu, nami kwa nihaba yangu binafsi naweza kusema napokea na kukubali kwa kuomba kwako radhi, ila swali linakuja, je hii habari ina ukweli au ilikuwa ni ya kutunga tu. Kwani kwa maelezo yako haya inaonyesha ulikuwa katika harakati za kufanya utafiti, au ulihamua kufanya utafiti baada ya tukio kutokea?

Mimi binafsi si kama niliumizwa na hii habari, ila niliona kuwa haikutumika busara kwa kuanika hadharani ilo tukio, wakati vyombo vya sheria vipo na vimewekwa kwa jili ya wale wote wanao fanya uhalifu wa aina yoyote ule yakiwemo haya ya ubakaji.

Mimi napinga udhalilisha wa aina yoyote ule na haswa kama muhathirika ni Mwanamke au mtoto mdogo, huwa inaniuma sana watu wanaposhindwa kuyafikisha haya masuhala kwenye vyombo husika.

Basi nami nichukue nafasi hii, kukutaka radhi kwa yale yote ambayo kwa namna moja ama nyingine yalikukwaza, yote hii ni katika kuwekana sawa na kufikisha kile ambacho nimeona kuwa kinafaa kwa jamii kukielewa.
 
Haiyumkini mnaweza kunishangaa kwa kumtumia mhusika ambaye nimemtumia. Wafanyao vitendo hivyo ni watu wa karibu sana nasi - baba, kaka, mjomba, binamu, nk nk. Niliamua kumtumia mhusika huyo ili kuweza kuibua hisia nzito na kupata reaction mbali mbali juu ya suala hili. Haikuwa nia yangu kumchafulia jina mtu yoyote.
Nawatakia kila la kheri katika ujenzi wa Taifa.
 



MKuu nimekusoma. Asante kwa mchango wako.
 
Duh poleni sana. Muwekeni baba yenu katika maombi naamini Mungu atawaonyesha njia sahihi ya kuhandle tatizo.

Binti wa kazi mtafuteni 4 medical check ups na ushauri nasaha.
 
Kudadadadaaaaaaaaadeki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…