Baba yake Dk Ulimboka atoa ya moyoni

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
BAADA ya kimya cha muda mrefu, baba mzazi wa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Stephen Ulimboka, amekubali kuzungumzia sakata la mwanaye kutekwa, kuteswa, kutibiwa na hatimaye kurejea nchini akisema kwamba kupona kwake ni neema za Mungu, huku akiishutumu Serikali kuwa imewatelekeza Watanzania.Hii ni mara ya kwanza kwa baba huyo, Ulimboka Mwaitenda kuzungumza tangu mwanaye alipotekwa, kuteswa na baadaye kutupwa katika Msitu wa Pande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

"Naishangaa Serikali hii ambayo wananchi wanapigwa na kuuawa bila makosa. Nakumbuka kiongozi aliyeipenda Tanzania ni mmoja na ameshatangulia mbele za haki," alisema akimaanisha Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Mwaitenda alitoa kauli hiyo jana baada gazeti hili kumtafuta ili azungumzie habari zilizoenea nchini kwamba mwanaye, amepata kazi nje ya nchi.

Kuhusu madai hayo, Mwaitenda alikanusha akisema kuwa mtoto wake hawezi kwenda nje ya nchi bila yeye kufahamu... "Pengine ana mipango hiyo, lakini mimi sijui wala sijasikia, lakini atakwenda nje ya nchi kufanya nini? Hizi habari hizo ndiyo nazisikia kwako kwa mara ya kwanza eti Ulimboka anataka kwenda nje ya nchi? Akafanye nini alichokosa hapa Tanzania!"
Wakati mwandishi akiingia nyumbani kwa Mwaitenda, Ubungo Kibangu, Dar es Salaam, alipishana na Dk Ulimboka akiwa kwenye gari na wenzake, wanne. Hata hivyo, hakufanikiwa kuzungumza naye.

Kuhusu tukio la kutekwa, kuteswa na kutupwa katika Msitu wa Pande, Mwaitenda alisema: "Mpaka sasa, tumeiona kazi ya Mungu, ile ni neema ya Mungu kwa sababu wewe uliona wapi mtu akapigwa namna ile halafu akapona kama si kwa neema tu."
Alisema alimkanya mtoto wake huyo aachane na masuala ya migomo na siku chache baada ya onyo lake ndipo akatekwa na kujeruhiwa vibaya.

"Nilimkanya kabisa kuhusu mambo ya migomo hasa baada ya kuniambia kuwa amechaguliwa kuwa msemaji mkuu wa madaktari wenzake na kwa bahati mbaya ndiyo yakatokea hayo yaliyotokea," alisema.
Alielezea kushangazwa kwake na watu waliompiga mtoto wake akisema, hajui walikuwa wanataka nini. Alisema hakuwa na uhasama na mtu yeyote kuanzia kazini kwake hata kwa marafiki zake. "Mpaka sasa nashindwa kuelewa kwa nini waliamua kumpiga, kwa sababu kwa ninavyomjua Steven, hajawahi kuwa na ugomvi na mtu tangu anasoma shule ya msingi mpaka anamaliza chuo kikuu. Sijawahi kupata mashtaka kuwa amegombana na mtu. Nashangaa haya yanayotokea leo."

Akitoa wasifu wa mwanaye huyo alisema tangu utoto wake, daktari huyo alikuwa mtulivu na mwenye upeo wa hali ya juu. Alisema anasikitishwa mno na yaliyompata akisema kwamba siku moja ukweli utawekwa wazi kwani siku zote kazi za Mungu na kazi za shetani haziwezi kuchangamana. "Kama mafuta na maji, ukiyachanganya... mafuta yatakuwa juu na maji yatabaki chini. Najua siku moja Mungu ataweka wazi ukweli," alisema.

Kuhusu afya ya Dk Ulimboka, Mwaitenda alisema ingawa yeye si daktari, lakini anamwona mtoto wake kuwa yu mwenye afya na kuongeza kuwa hata mwanaye huyo amekuwa akisema kwamba sasa ana afya njema.

Hali nyumbani kwa Mwaitenda
Baada ya kufika nyumbani kwa mzazi huyo wa Dk Ulimboka, mwandishi alikaribishwa vyema na mzazi huyo ingawa alimtahadharisha kwamba endapo angekutana na daktari huyo hapo au ndugu zake, wangemfukuza.
"Una bahati ungewakuta hapa watoto wangu tusingezungumza. Hata hawa mabinti zangu wakikukuta, hatutaendelea na mazungumzo...."

Hivyo ndivyo ilivyotokea kwani baada ya kuelezea hayo, mabinti wake wawili walitokea na mmoja akaanza kwa kusema... "Shikamoo Baba, umesharudi? Huyu nani?"
Mzee Mwaitenda, kwa bashasha aliwatambulisha mabinti hao... " Huyu ni Florence... mwandishi wa Mwananchi..." Hata kabla hajaendelea binti huyo na mwenzake walimshika mkono na kumwamuru atoke nyumbani hapo mara moja.
"Haya dada toka, toka, mmeshindwa kuandika kuhusu mwandishi mwenzenu aliyekufa (Daudi Mwangosi), mnakuja kutufuata mpaka huku Kibangu.... mtazame miguu ilivyomchafuka kwa vumbi kwa kushadadia ya watu, toka kabla sijakupiga makofi," alisema mmoja wa mabinti hao.

Madai Dk Ulimboka kutoweka

Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Namala Mkopi ambaye alikuwa karibu na Dk Ulimboka wakati wa mgomo wa madaktari nchini, alisema tangu waonane aliporejea nchini kutoka Afrika Kusini, hajawasiliana tena.
"Hatujawasiliana naye," alisema Dk Mkopi na kusema kulingana na ukubwa wa tatizo lililompata, hakuwa na mpango wa kumsumbua, bali kumwacha apumzike hadi atakapokuwa amejisikia mwenyewe kurejea kazini.
Aliyekuwa kiongozi wa jopo la madaktari waliomhudumia, Profesa Joseph Kahamba alisema, hajawahi kuonana wala kuwasiliana na Dk Ulimboka tangu alipopelekwa Afrika Kusini, Juni mwaka huu.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz
 
Huyu dada ulimboka kadata kweli.......
Waandishi mmeanza kuzodolewa sasa,,,,,ENDELEEN KUJADILI SUALA LA MWANGOS
 
Ni sawa mnahitaji habari, but be patient hivi unafikiri tatizo lililompata ni dogo? Unahisi familia yake ilijisikiaje kwa yaliyompata japo ameshapona? Hebu mpuzisheni kwanza.
 
Kweli waandishi walitakiwa kuandika na kuhamasisha sana jamii kusaidia kuhusu suala la Mwangosi si la Uli tena!
 
Hivi ni lini ataweka mambo bayana kama alivyoahidi mara alipotua nchini au ndo kishawekwa mfukoni maana kila mtu ana bei yake
 
Dr. Mkopi & Prof. Kahamba; inakuwaje tangu mpiganishaji wenu tangu atoke SA hamjataka hata kujua maendeleo yake ya kiafya; mnathubutu kujisema et mmeamua kumuacha apumzike, ndio anahitaji kupumzika lkn hata kumjulia hali na kumpa faraja?
Hata alipoondoka kwenda kwenye Matibabu aliwaachia wosia kuwa damu yake ilomwagika iwe chachu kwenu ktk kupigania haki zenu kwa kuendeleza kusimamia madai yenu ya msingi je mlifanya hivyo?
Nachelea kusema kuna kilicho nyuma ya pazia et enyi Madaktari, Igwondu ni mwenzenu?
 
hebu tuwe wakweli jamani, sasa hapa kuna habari gani hapa? mi sioni jipya hapo, hiyo ni filler tu kwenye hilo gazeti.
 
Upendo wetu kwa dr. Ulimboka ulikuwa wa bure, tulijisumbua kusikitika pamoja na familia ya mzee ulimboka kwa ajili ya kutekwa kwa dr. Ulimboka

Ama kweli tenda wema uende zako. Na siku atakayoongea huyu dokta atafananishwa na karunguyeye tu! Hana tena ile thamani aliyokuwa nayo before.

Biblia husema kweli daima; "mkopeshapo msitarajie kurudishiwa"
 
Alitakiwa atuambie nini kilichompata ili umma ujue. Kuna maneneo mengi yaliyokuwa yakisemwa kuhusu kitendo cha kikatili alichofanyiwa. Hata kuna taarifa kuwa hata yeye binafsi alikuwa akitoa kauli za kuihusisha Ikulu na tukio hilo. Aidha Polisi walihusishwa pia. Sasa kwa vile anasema anaendelea vizuri; kwa nini asijitokeze na kusema wazi kilichotokea ili tujue kama tuliyokuwa tunaambiwa dhidi ya Polisi na Ikulu yana ukweli wowote au ni porojo? Kuendelea kukaa kimya kutasababisha hisia nyingi ambazo zinaweza kuwa za kweli au la dhidi yake.
 
Hiyo familia imeishawekwa sawa na Serikali hakutakuwa na jipya tena hapo, Cha muhimu tulitunze vizuri lile gazeti la Mwanahalisi kwani ndo lenye taarifa yote juu ya ufedhuli wa serikali hii, na kwa jinsi Dr. Uli alivyokamatika na waliomsurubu atakuja ikana kauli yake kabla ya kwenda South na pia atalikana hata ili gazeti hapo baadaye.
 
Dr. Mkopi & Prof. Kahamba; inakuwaje tangu mpiganishaji wenu tangu atoke SA hamjataka hata kujua maendeleo yake ya kiafya; mnathubutu kujisema et mmeamua kumuacha apumzike, ndio anahitaji kupumzika lkn hata kumjulia hali na kumpa faraja?
Hata alipoondoka kwenda kwenye Matibabu aliwaachia wosia kuwa damu yake ilomwagika iwe chachu kwenu ktk kupigania haki zenu kwa kuendeleza kusimamia madai yenu ya msingi je mlifanya hivyo?
Nachelea kusema kuna kilicho nyuma ya pazia et enyi Madaktari, Igwondu ni mwenzenu?


Mchochezi, unajuaje labda wako nae karibu ila tunayoyaona juu ya Ulimboka ni mkakati wa pamoja wa yeye, familia na madaktari wenzie?
 
SUBIRI SUBIRI HUUUMIZA MATUMBO!
Bora aweke wazi kuwa amesamehe yote na katu
hatodai tena alichokuwa anapigania!!
 
achen hbr zisizo na msing mna2letea mamb ya ajabu ulimboka tumechoka nae hebu weken thread zeny ujazo hapa jf 2na mamb meng ya kuzungumzia na si maisha ya m2 1! DZAIN UMEBOA SANA!
 
Mchochezi, unajuaje labda wako nae karibu ila tunayoyaona juu ya Ulimboka ni mkakati wa pamoja wa yeye, familia na madaktari wenzie?

Sasa najuaje namna gani wakati mwandishi ameweka kauli zilotoka baada ya mahojiano yao?
Kama wako naye pamoja kwani kuna athari gani kukiri kuwa huwa wanawasiliana japo kumtakia hali na kujua maendeleo yake kwani hilo nalo ni tatizo?
 
SUBIRI SUBIRI HUUUMIZA MATUMBO!
Bora aweke wazi kuwa amesamehe yote na katu
hatodai tena alichokuwa anapigania!!
Wale madaktari waliofukuzwa kazi wako wapi?na huduma katika hospitali zetu zikoje?yale madai yao yaliishia wapi?kuna mufaaka wowote ulifikiwa kati ya madaktari na serikalai.Mwenye kujua lolote atujuze.
 
Hivi ni lini ataweka mambo bayana kama alivyoahidi mara alipotua nchini au ndo kishawekwa mfukoni maana kila mtu ana bei yake

hivi mnataka aweke bayana kitu gani hasa si alishaongea mara baada ya kuokotwa na mwanahalisi walishaiandika ishu nzima ilivyokuwa; Sisi WATZ ni wababishaji sana dk ulimboka alivyokaa kimya hata mimi namsapoti kwani hakuna jipya la kuongea kila kitu kina julikana
 
Back
Top Bottom