Baba unawapa watoto wako muda wa kukaa nao?

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,421
Reaction score
5,024
Baba unawapa wanao muda wako ili wakufurahie kama baba yao? Au ndio mtoto siku akikuona anajiuliza huyu leo mgonjwa au ana shida gani maana ni ajaabu kukuona akiwa macho.

Wanaume, jitahidi kujenga mahusiano mazuri na watoto wenu wakiwa wadogo, jitahidi kuwahi kurudi mapema muonane na watoto wenu wakiwa bado hawajalala.

Kuna wakinababa hata wakiwahi kutoka kwenye majukumu hawarudi nyumbani, wanapitia kwa marafiki au bar kupiga stori nk wanasahau kuna jukumu la malezi ya watoto wanatakiwa kulitimiza.

Mtoto unapoonana naye, wakati mwingine kumpa zawadi kwa mikono yako, kumsaidia kazi zake za shule, kumsikiliza anachosema na kama kinahitaji utatuzi kumtatulia, kucheza naye, kumwambia ubora alionao kunafanya akuamini, akupende na akuone wewe ni mtu unayejali uwepo wake na kukufanya kuwa mtu wa karibu kwake.

Unakuta kuna baba hajawaona watoto wake wakiwa macho ndani ya mwezi mzima, anaondoka wamelala anarudi wamelala sio kwamba hawezi kupata muda hapana ila hajaona umuhimu, anaamini jukumu pa malezi ni la mama yake tu yeye jukumu lake ni kutoa hela kwa mama yake ili mtoto ale, avae au aende shule, hayo mtoto hajui anachojua ni kile anachoona unafanya.

Mbaya zaidi siku akionana na watoto wake unakuta wanafanya kosa, anawaadhibu, hapo mtoto anatengeneza chuki kwa kiwa huna wema uliomtendea moja kwa moja akakuona( umemlisha ila hajui) ili kumfanya mtoto aone upendo wako inabidi auone ukimtendwa jambo linalompa furaha, linamuweka karibu yake.

Wengi wanasema oooo ningerudi nyumbani ila nakwepa maneno, mara makelele, jua kuna 'bond' muhimu sana ambayo ukifanikiwa kuijenga kwa mtoto wako akiwa mdogo haitavunjika hata ukiwa mzee naye akiwa mkubwa.

Wababa tutimize majukumu yetu nje ya kuhudumia watoto kifedha tutenge muda wa kuwa nao ili waone kuwa tunawajali kwa kunawapa muda.
 
unajua kwa nini tunajichimbia kwenye vijiwe vya mipira baada ya majukumu
 
Feminist. Lini mwanaume ameumbiwa kuwa mlezi wa watoto? Wewe tekeleza majukumu. Ukibaki kibibembeleza kwa watoto utaishia kukojolewa tuu.
 
Pole sana kwa watoto wako ulionao au utakao kuwa nao kwa kuwa na baba mwenye fikra kama zako. Nawahurumia sana
 
Baba unawapa wanao muda wako ili wakufurahie kama baba yao? Au ndio mtoto siku akikuona anajiuliza huyu leo mgonjwa au ana shida gani maana ni ajaabu kukuona akiwa macho.

Wanaume, jitahidi kujenga mahusiano mazuri na watoto wenu wakiwa wadogo, jitahidi kuwahi kurudi mapema muonane na watoto wenu wakiwa bado hawajalala.

Kuna wakinababa hata wakiwahi kutoka kwenye majukumu hawarudi nyumbani, wanapitia kwa marafiki au bar kupiga stori nk wanasahau kuna jukumu la malezi ya watoto wanatakiwa kulitimiza.

Mtoto unapoonana naye, wakati mwingine kumpa zawadi kwa mikono yako, kumsaidia kazi zake za shule, kumsikiliza anachosema na kama kinahitaji utatuzi kumtatulia, kucheza naye, kumwambia ubora alionao kunafanya akuamini, akupende na akuone wewe ni mtu unayejali uwepo wake na kukufanya kuwa mtu wa karibu kwake.

Unakuta kuna baba hajawaona watoto wake wakiwa macho ndani ya mwezi mzima, anaondoka wamelala anarudi wamelala sio kwamba hawezi kupata muda hapana ila hajaona umuhimu, anaamini jukumu pa malezi ni la mama yake tu yeye jukumu lake ni kutoa hela kwa mama yake ili mtoto ale, avae au aende shule, hayo mtoto hajui anachojua ni kile anachoona unafanya.

Mbaya zaidi siku akionana na watoto wake unakuta wanafanya kosa, anawaadhibu, hapo mtoto anatengeneza chuki kwa kiwa huna wema uliomtendea moja kwa moja akakuona( umemlisha ila hajui) ili kumfanya mtoto aone upendo wako inabidi auone ukimtendwa jambo linalompa furaha, linamuweka karibu yake.

Wengi wanasema oooo ningerudi nyumbani ila nakwepa maneno, mara makelele, jua kuna 'bond' muhimu sana ambayo ukifanikiwa kuijenga kwa mtoto wako akiwa mdogo haitavunjika hata ukiwa mzee naye akiwa mkubwa.

Wababa tutimize majukumu yetu nje ya kuhudumia watoto kifedha tutenge muda wa kuwa nao ili waone kuwa tunawajali kwa kunawapa muda.
Nashinda nao saana nikiwa Dar nawapeleka sehem za kucheza na kuogelea watoto wakati mi napiga mvinyo taratiiiiiibu.

Nawapenda sana basi tu Magu alinikimbiza Dar kunileta Dom. Ilibidi wabaki kusimamia projects.
 
Baada ya kumtimua mama yake binti yangu nipo nae huu mwaka wa tatu sasa .
 
Feminist. Lini mwanaume ameumbiwa kuwa mlezi wa watoto? Wewe tekeleza majukumu. Ukibaki kibibembeleza kwa watoto utaishia kukojolewa tuu.
Ha ha ha umenikumbusha baba yangu mkubwa watu walikuwa wakimuuliza "una watoto wangapi" yeye anajibu "mimi sina watoto, watoto ni wa mwanamke, kwani umewahi kuniona nina mimba?" na hapo anaongeza "wapi uliwahi kuona jogoo anatembea na vifaranga" maana yake ni kwamba yeye kazi yake ilikuwa kuzalisha tu kutoa matunzo. Pumzika kwa amani baba yangu though ulikuwa mtata sn kwa mambo mengi ila ulikuwa jembe kwelikweli na ngumi uliwatembezea vyema waliokuletea ujinga. Big up.
 
Hatari
 
Baba unawapa wanao muda wako ili wakufurahie kama baba yao? Au ndio mtoto siku akikuona anajiuliza huyu leo mgonjwa au ana shida gani maana ni ajaabu kukuona akiwa macho.

Wanaume, jitahidi kujenga mahusiano mazuri na watoto wenu wakiwa wadogo, jitahidi kuwahi kurudi mapema muonane na watoto wenu wakiwa bado hawajalala.

Kuna wakinababa hata wakiwahi kutoka kwenye majukumu hawarudi nyumbani, wanapitia kwa marafiki au bar kupiga stori nk wanasahau kuna jukumu la malezi ya watoto wanatakiwa kulitimiza.

Mtoto unapoonana naye, wakati mwingine kumpa zawadi kwa mikono yako, kumsaidia kazi zake za shule, kumsikiliza anachosema na kama kinahitaji utatuzi kumtatulia, kucheza naye, kumwambia ubora alionao kunafanya akuamini, akupende na akuone wewe ni mtu unayejali uwepo wake na kukufanya kuwa mtu wa karibu kwake.

Unakuta kuna baba hajawaona watoto wake wakiwa macho ndani ya mwezi mzima, anaondoka wamelala anarudi wamelala sio kwamba hawezi kupata muda hapana ila hajaona umuhimu, anaamini jukumu pa malezi ni la mama yake tu yeye jukumu lake ni kutoa hela kwa mama yake ili mtoto ale, avae au aende shule, hayo mtoto hajui anachojua ni kile anachoona unafanya.

Mbaya zaidi siku akionana na watoto wake unakuta wanafanya kosa, anawaadhibu, hapo mtoto anatengeneza chuki kwa kiwa huna wema uliomtendea moja kwa moja akakuona( umemlisha ila hajui) ili kumfanya mtoto aone upendo wako inabidi auone ukimtendwa jambo linalompa furaha, linamuweka karibu yake.

Wengi wanasema oooo ningerudi nyumbani ila nakwepa maneno, mara makelele, jua kuna 'bond' muhimu sana ambayo ukifanikiwa kuijenga kwa mtoto wako akiwa mdogo haitavunjika hata ukiwa mzee naye akiwa mkubwa.

Wababa tutimize majukumu yetu nje ya kuhudumia watoto kifedha tutenge muda wa kuwa nao ili waone kuwa tunawajali kwa kunawapa muda.
Yes hii kuna ukweli flani hivi
 
Back
Top Bottom